Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 23, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu;
  Tarehe: 23rd May 2011
  HABARI LEO

  MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba amemshutumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa amekuwa mtu wa kukimbia, kujificha na kutosema ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.

  Ngeleja anatupiwa shutuma kuwa kauli ya Serikali aliyoitoa bungeni juu ya hali ya umeme nchini ikiwemo kukodishwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 260 ifikapo Juni na Julai mwaka huu imeshindikana lakini Waziri yuko kimya.

  “Waziri alisema bungeni na akamwambia Rais (Jakaya Kikwete) naye akalitangazia Taifa kuwepo kwa umeme ifikapo Julai, lakini kwa taarifa nilizonazo biashara hiyo imekwama na Waziri yuko kimya anakimbia kusema ukweli,” alidai Makamba.

  January alidai kitendo cha Waziri kukimbia na kujificha, kinaonesha kuna ombwe la uongozi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na akaahidi kuwa Kamati yake itambana Waziri huyo aeleze utekelezaji wa mipango yote aliyoiainisha kwenye kauli ya Serikali.

  Gazeti hili lilimtafuta Waziri Ngeleja bila mafanikio kwa kuwa simu yake ilikuwa haipatikani.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo hawakupatikana kutoa maelezo.

  Kamati hiyo itakutana na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tanesco wiki hii na katika kikao hicho Kamati itahoji utekelezaji wa mapendekezo 30 waliyoyatoa kwa Serikali. “Tutawaita tuwaulize maswali magumu juu ya mapendekezo yetu.”

  Akielezea hali halisi ya kukodishwa kwa mitambo hiyo, January alidai Tanesco iliziomba kampuni 21 ziombe zabuni ya kuzalisha umeme wa mafuta kwa muda wa miezi sita lakini kati ya kampuni hizo, ni kampuni 17 tu zilichukua makabrasha ya kuomba zabuni hiyo.

  Aliendelea kudai kuwa kati ya kampuni hizo 17, ni kampuni nne tu ndizo zimeomba zabuni za kuzalisha umeme huo wa mafuta na kati ya kampuni hizo nne, ni kampuni moja tu iliyoomba kuweka mitambo katika maeneo manne yaliyoainishwa na Tanesco.

  “Nyingine hizi zilizobaki zimeomba kuzalisha eneo moja moja,” alisema January. Pia alisema kampuni zote hizo zimeomba kuiuzia Tanesco umeme huo sio chini ya Sh 1,000 kwa uniti moja wakati Tanesco yenyewe inamuuzia mteja chini ya Sh 300 kwa uniti.

  “Sasa unaweza kuona kuwa mradi huu haupo tena, lakini Waziri anajificha hataki kusema ukweli.” January alisema uzalishaji wa umeme kwa mafuta ni ghali ndio maana wawekezaji wengi wamegoma kutuma maombi ya kuzalisha umeme huo.

  Kiasi cha megawati 260 zinatakiwa kuzalishwa na wawekezaji watakaoshinda kuzalisha umeme huo wa dharura kwa kipindi cha miezi sita. Alidai Waziri Ngeleja alitoa tamko bungeni akiwahakikishia Watanzania kuwa mchakato huo utaenda kwa wakati hali iliyomlazimu pia Rais Jakaya Kikwete kulitangazia Taifa kuwepo kwa matumaini hayo ya kupata umeme wa dharura katika mwezi huo.

  “Tunaingia Juni hiyo mitambo iko wapi? Hadi sasa hakuna kampuni iliyopewa zabuni hiyo, nina uhakika hizo megawati 269 hatutazipata, cha ajabu kwa nini wananchi hawaambiwi ukweli?” Alihoji January.

  Mwenyekiti huyo alisema kwa hali ilivyo inaonesha wazi kuwa kuna uzembe mkubwa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco katika kufikiria na kupanga kuhusu umeme.

  Alisema Kamati yake safari hii itaibana wizara hiyo pamoja na Tanesco kuhusu tamko alilolitoa Waziri bungeni pamoja na mipango aliyoitaja ikiwemo mitambo ya Mwanza ya kuzalisha megawati 60 pamoja na mitambo ya Ubungo na Tegeta ya kuzalisha megawati 145.

  “Tumekuwa tukizungumza lakini hatukuwa na mahali pa kuwashika, safari hii tuna sehemu ya kuwakamata maana tunaenda kujadili bajeti ya wizara hii, kwa kweli niwahakikishie kuwa watapata wakati mgumu,” alisema Makamba.

  Meneja Mawasiliano wa Tanesco Badra Masoud mwishoni mwa wiki aliulizwa na gazeti hili juu ya zabuni hizo naye akajibu kuwa bado wanafanya tathmini ya waombaji na baadaye watatatoa majina ya waombaji wenye sifa ambao watachuana.

  Eneo lingine ambalo Makamba alisema Kamati yake itambana Waziri Ngeleja ni kuhusu kuzimwa kwa mtambo wa Songas ili kuruhusu ukarabati wa visima vya gesi.

  Mwenyekiti huyo alisema kuna jambo linafichwa kuhusu visima hivyo kwani ukarabati pekee hauwezi kusababisha mitambo yote kuzimwa wakati inafanywa kwa awamu.

  Alisema katika hilo pia kamati yake itahoji sababu ya mitambo iliyoko Ubungo Songas inayotumia mafuta yenye uwezo wa kuzalisha megawati 120 kutowashwa katika kipindi hiki ambacho Taifa linakabiliwa na mgawo mkubwa.

  “Pale kuna mitambo ya kutumia gesi au mafuta, lakini kwa makusudi haiwashwi, tunataka kujua sababu nini hasa?” Alisema.

  Eneo lingine ambalo alisema Kamati yake itahoji ni juu ya gesi ambayo alisema licha ya kuchimbwa nchini lakini wananchi hawajafaidika na rasilimali hiyo. Alisema bei yake bado iko juu ndio maana hata umeme wananchi wanauziwa kwa bei ya juu.

  Pia alisema watataka mikataba iliyofikiwa kati ya Serikali na wasafirishaji wa gesi ambayo ni Kampuni ya Songas ipitiwe upya ili miundombinu mikubwa kama bomba la kusafirishia gesi limilikiwe na Serikali iwe rahisi mwekezaji mmoja akikwama kusafirisha gesi wengine waendelee kutoa huduma.

  “Hili la kumwachia mwekezaji mmoja kumiliki hili bomba ni kuweka rehani nchi yetu, lazima hii mikataba iangaliwe upya,” alisema Makamba. (BRAVO January!!...you're now talking)
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Mbona kamati ya ulinzi na usalama haikupendekeza Sued Mwinyi kujiuzulu ama walimwogopa?ama yeye ni mwenzao?maana ccm ina wenyewe...mie naona wote wabovu tu,wapigwe chini fasta
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  JK kwa sasa anamasikitiko ya kifo cha mlinzi wake Sheikh mfuga majini YAHYA asisumbuliwe jamani
   
 4. K

  Karlmakeen Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni... Bwana Makamba ametoa maoni ya msingi sana. Tusubiri tuone matokeo ya huo mkutano. Hadi hapo alipofikia, nampa big up!!
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Ngeleja ni kijana wa ROsti tamu JK hana uwezo wa kumfanya lolote!!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Kwa hilo nakuunga mkono kabisa. Natamani maneno haya yaliyotamkwa na Makamba, Kikwete naye angekuwa na uwezo wa kuyatamka hadharani na kuyafanyia kazi, lakini kawekwa mfukoni kwa Rostam na mafisadi wenzake basi nchi inamshinda anahangaika na kutoa kauli ambazo anashindwa kuzifanyia kazi. Kama juzi juzi katamka, "Ndani ya Wizara nyingi kumejaa rushwa iliyokithiri." Ni Mtanzania yupi asiyelijua hili!! Miaka sita uliyokaa madarakani umechukua hatua zipi kupambana na hiyo rushwa iliyokithiri!!!! Mtu mzima hovyo kabisa!
   
 7. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ki ukweli makamba junior anajitofautisha sana na baba yake kwa mambo mengi . si shahbiki wa chama chake, lakn the man is potential. ngeleja hana na wala hatakuwa na jipya kwa sababu uwepo wake kwenye hiyo wizara una baraka za mafisadi
   
 8. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  people can talk sense sometime
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Kabisa Mkuu. Huyu January kama ataendelea kutoa kauli kama hizi na pia kuwa mbali na kundi la mafisadi ndani ya CCM na Serikalini basi anaweza kujijengea umaarufu mkubwa sana. Haingii akilini kabisa mtu kwenda kusaini mkataba ambapo TANESCO wanatakiwa wanunue uniti moja ya umeme toka Songa kwa shilingi 1,000 ambayo inatakiwa ilipwe in FOREX halafu TANESCO wanawauzia wateja wao kwa shilingi 300 kwa kila uniti tena kwa pesa yetu ya madafu! Mikataba kama hii ya kifisadi ndio inaua TANESCO taratibu.
   
 10. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtoto wa Nyoka ni Nyoka tu (hata kama baba nyoka akijivua gamba), maneno hayo ni ya kutafuta cheap popularity, uwepo wa January makamba katika hiyo moja ya rank za juu sana katika CCM Kwa haraka, Ni mwendelezo wa majaribio ya viongozi wa CCM kuandaa kiupendeleo watoto wao kushika Nyadhifa za Juu (Nepotism) Unless of course atuhakikishie beyond reasonable levels of doubt kwamba kupanda kwake kisiasa siyo sawa na kupanda kwa mtoto wa Mwinyi na Riz 1,
  Watanganyika tunapinga hizo slogan za bei rahisi toka kwa watu ambao pengine hawakustahili kuwa na access ya ''bull pulpit'' kama tungekuwa na uhakika wa level playing field katika kupanda kisiasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu wala usijisumbue! Kwa hilo hatakaa amfukuze! labda kamaameingilia anga zake za maloveeeeee segerea itamhusu na sio kufukuzwa kazi tu!
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nadhani watu wengi hawfhamu mhusiano yaliyopo kati ya huyu waziri wa nishati na Mkuu wetu na haya mambo ndio yanasababisha tushindwe kuwajibishana hata kama mtu atadanganywa

  namkubali Bwana makamba kwani amekuwa muwazi zidi na kiukweli kunakitu anataka kutufanyia watz ni swala la mda tu tumpe nafasi ya kutufanyia kazi

  Jannuari(a.k.a makaptula) chapa kazi tupo pamoja
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kikwete alikwenda nje ya nchi kwenye mkutano akiongozana na Ngeleja na ndani ya ule mkutano Ngeleja alipigwa picha amelala fofo ; hakumchukulia hatua zozote na mpaka leo anadunda, kwani wanamfichia siri zake nyingi za kifisadi na haikuwa bahati mbaya kumteua kuwadi wake Jairo kuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati!! Wote hawa ni wezi!!
   
 15. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nakushukuru kwa kuwakumbusha ndugu zangu, wadanganyika maana, ni wepesi sana kusahau. Wengine wanadhani kelele za Nape juu ya RA, EL na AC zinatoka kwa JK, kitu ambacho naamini hakiwezi kutokea daima na milele. JK hana ubavu wa kumwondoa waziri yeyote aliyeteuliwa kihalali na Rais RostiTamu ya Aziza.

  Baraza la Mawaziri litaendelea kuwa na wateule wa RA na EL hadi mwisho wa utawala wa CCM. Mark my words; hawa jamaa (RA na EL) wameishika CCM pabaya kuliko watanzania wengi wanavyodhani.

  Kelele za magamba zilipoanza niliwaandikia ktk thread moja kwamba hata iweje CCM haina jeuri ya kuwafukuza hao jamaa wala vibaraka wao kwa kuwa wao hasa ndiyo chama wengi wakaipuuza kwa kudhania Nape katumwa na JK.

  Kama tetesi juu ya mambo ya ndani ya chama cha magamba ni za kweli basi mkono wa Rosti umeshika mihimili miwili ya dola na pengine hata ule wa tatu. EXECUTIVE anaye JK na wengine kibao wanaomsaidia, pengine hata Mtoto wa Mkulima maana naye haeleweki. LEGISLATURE anaye Ma Anne MaK na washabiki wao. Huko kwingine (JUDICIARY) sijui lakini sitashangaa nikiambiwa ameushika mhimili huo pia.

  Kama utafuatilia kwa makini utagundua baada ya EPA ulaji mkuu wa Rosti upo wizara ya Nishati na Madini ambako si bahati mbaya kwamba kuna kibaraka wake, Ngeleja (Mwanasheria).
   
 16. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kikwete akifukuza mtu kazi ujue mwisho wa dunia umekaribia.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe Mkuu. Kikwete hawezi kufurukuta mbele ya Viongozi (Lowassa na Rostam) wa timu iliyoitwa MTANDAO maana anajua wanajua fika waliyoyafanya hadi yeye kuingia Ikulu. Sasa kama wakisema "liwalo na liwe" na kuanika siri zote hadharani za yale yaliyojiri katika kampeni za 2005 basi atakayeathirika zaidi na siri hizo ni Kikwete. Ni hasara kubwa kwa nchi kuwa na Rais aliyewekwa mifukoni na mafisadi.

  Hii kasheshe ya Richmond/Dowans inaingia mwaka wa sita sasa kutokana na Rostam kumuweka mfukoni Kikwete, vinginevyo tungeshasahau kuhusu Richmond/Dowans miaka mingi iliyopita
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  ngeleja hovyo sana,alidanganya bungeni kuwa kiwira imesharudishwa serikalini,kumbe ipo rehani kwa wadai
   
 19. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mafisadi na vibaraka wao ndiyo wanadumu katika nafasi na wizara wakati viongozi wengine na mawaziri wachapa kazi wanaondolewa kwa fitna na kuhamishwa hovyohovyo kama Sitta na Mzee Magufuli.

  Kwani hakuna uwezekano wa kuanzisha "The Base" yetu hapa TZ ambapo watu watajitoa kwa mali na kila hali dhidi ya mafisadi walioziba masikio? Ili fisadi akilalamikiwa sana na wananchi ama arejeshe mali aliyokwapua, aombe radhi na kujiuzulu au akumbane na septemba 11. Haya ni maoni tu maana naona dola haitaki kabisa kupambana na tatizo hili kwa kuwa yenyewe ni mhusika na ipo kutokana na kuwapo ufisadi. Kila unapotokea mgao wa umeme kiusanii ujue kuna jambo Rosti anataka kufanya. Safari hii mitambo yake inauzwa kwa wamarekani kama Richmond maana nayo ilitokea marekani kabla haijageuka feki. Kisha watapewa mkataba na ataendelea kukusanya ulaji.

  Serikali ya wanamtandao ni tunda la mti unaoitwa ufisadi. Maana, ulianza ufisadi kisha mtandao ukaingia madarakani kwa hiyo msitarajie matokeo yoyote ya maana dhidi ya ufisadi kwa kuwa ndiyo source ya chakula cha serikali hii.

  Naona kama tukiamua kujitoa kwelikweli tutaenda peponi pia maana katika nchi hii wanaonyanyasika kutokana na ufisadi karibu wote ni wana wa Mungu tunayemwamini. Mnaonaje wanajamvi?
   
 20. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Njia kuu za uchumi lazima zimilikiwe na serikali.
   
Loading...