Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

mi sina habari na kumuwaza JK najua atamwambia ngeleja apime,ajichunguze mwenyewe na akiona ana wajibika aachie ngazi mwenyewe...sina habari na serikali now..
 
Naona kama kuna conection kuzimwa kwa mitambo ya gesi-kutokezea kwa mgao na habari kwamba mitambo ya Dowans imeshauzwa kwa Symbian Power ambao wamesema kwa haraka kwamba wako tayari kuongea na Tanesco ili waiuzie umeme. Si hadithi ya kofia mpya lakini shehe yuleyule wa zamani?
 
Ni kwamba Kikwete akumteua Ngereja based on competence rather ilikuwa ni kwa uswaiba tu. Kwa hiyo don't expect kuwa ataondolewa kutokana na poor performance kama tunavyoona. Itawezekana tu siku mahusiano yao ya kibinafsi (si ya kikazi)yatakopoteteleka. Hiyo ndio administration ya JK.
 
Tusiwe na Haraka na Pupa na Jazba! Tusubiri maswali magumu kutoka kwenye kamati na majibu mepesi kutoka kwa Ngeleja!
 
kitu alichozungumza january ni kizuri kwa kutufahamisha juu ya hali halisi ilivyo,lakini cha ajabu wengine wanambeza na kumuita mnafiki,tuache ushabiki mtu akitoa mchango ambao unaweza ukawa na tija kwa taifa
 
ki ukweli makamba junior anajitofautisha sana na baba yake kwa mambo mengi . si shahbiki wa chama chake, lakn the man is potential. ngeleja hana na wala hatakuwa na jipya kwa sababu uwepo wake kwenye hiyo wizara una baraka za mafisadi

Makamba, if I read well what he said, he is siding the issue of Dowans kama alivyofanya kuanzia mwanzo. Hapo anasema watu wameleta quotations za 1000 wakati Tanesco inauza 300, na hapo nyuma kidogo Dowans walikuwa wanauza if not mistaken 165. Sasa utaona kabisa kwamba anaelekea wapi. Amini usiamini inawezekana kabisa Rostam na hata yeye mwenyewe Rais wanafanya kampeni kwa ajili ya Dowans lakini bila kujua pia kuwa wanataka kumsafisha Lowasa.
Kwa mtu wa kawaida hii siyo rahisi kuiona lakini ukifikiria kiupeo zaidi unaweza kuona kuna linkaga. Inawezekana kuwa hawajui kuwa pia pamoja na Dowans kupata biashara itakuwa pia imemsafisha Lowasa in a way or another. Hapa kuna personal interests.
Ukweli utajulikana tu!!!!
Serikali ya CCM imekuwa haitekelezi ahadi zake kwa wananchi kama walivyoahidi kwenye kampeni zao na hata ukiangalia wizara zote hakuna hata moja inayoweza kusema iko on target wote hao hawatekelezi ahadi na hata hiyo inayoitwa ilani ipasavyo. Ukata pia inaweza kuwa ni chanzo ijapokuwa Mkullo alikataa lakini haiwezekani nchi ikawa na fedha na hapo hapo bajeti za baadhi ya wizara zikawa zimekatwa kwa sana tu.
 
Naona kama kuna conection kuzimwa kwa mitambo ya gesi-kutokezea kwa mgao na habari kwamba mitambo ya Dowans imeshauzwa kwa Symbian Power ambao wamesema kwa haraka kwamba wako tayari kuongea na Tanesco ili waiuzie umeme. Si hadithi ya kofia mpya lakini shehe yuleyule wa zamani?
Muta... hapo niko nawewe. Hapa panatafutwa connection au sababu ya...... Hata siku moja Zebra hataacha mistari akizaliwa asiye na mistari basi huyo siyo zebra tena bali ni donkey!!!!
 
Since January is saying what I would have liked to hear and what I would have liked for our President to be saying then on this we are on the same page.... All I can say is maintain the consistency and you will go all the way JM.... and even if the party sacrifices you.... I am sure the Para-troopers of the "Truly Democratic Party" will welcome you with open hands where you can continue your crusade.....
 
TANESCO: Tunazungumza na Symbion Power



Na Edmund Mihale
Majira

HATIMAYE Shirika la Umeme (TANESCO) limekiri kuwa na mazungumzo ya kununua umeme wa megawati 112 kutoka kwa kampuni iliyonunua mitambo ya
kuzalisha ya umeme ya Dowans, Symbion Power kutoka Marekani

Taarifa ya TANESCO iliyosainiwa na Meneja Mwasiliano wa Shirika hilo, Bi. Badra Masoud Dar es Salaam jana, ilikiri kuwapo kwa mazungumzo hayo ambayo yanakwenda sambamba na mchakato wa kununua mitambo mipya ya umeme.

Katika taarifa hiyo Bi. Badra alieleza kuwa uamuzi huo wa TANESCO unatokana na ukarabati katika visima vya gesi katika kisiwa cha Songosongo, ambao umesababisha uzalishaji wa umeme katika mitambo ya Songas kusimama na hivyo kusababisha mgawo mkali wa umeme.

Gesi hiyo hutumika kuzalisha umeme kwenye mtambo wa Ubungo, Tegeta na Songas na ukarabati huo umesababisha upungufu wa megawati 350 kutoka kwenye gridi ya taifa.

Pia Tanesco imelazimika kutoa taarifa hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Bw. John Mnyika kutoa taarifa akimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha wote waliosababisha mgawo wa umeme, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja.

Bw. Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alisema hakuna haja tena ya kukodi mitambo ya dharura, badala yake serikali kupitia TANESCO ingenunua mitambo mipya ili kuepuka kuingia katika ufisadi kama wa Richmond.

Alieleza kuwa TANESCO imelazimika kufanya mgawo kwa mikoa iliyounganishwa katika Grid ya taifa
kwa siku nane mfululizo kuanzia tarehe 19 hadi 26 Mei, mwaka huu.

Ilieleza kuwa shirika limeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na upungufu wa umeme nchini ikiwemo kukodi mitambo ya kuzalisha umeme na kuanzisha miradi zaidi ili kuongeza vyanzo vya nishati hiyo.

Ilieleza kuwa kampuni 15 zilijitokeza kutaka kukodisha mitambo ya Megawati 260, lakini kati ya hayo tatu zilizorudisha fomu za kuonesha nia ya kukubali na baada ya mchanganuo na kampuni moja ndio iliyokidhi vigezo na ina uwezo wa kuzalisha megawati 70 na mitambo hiyo itafungwa Mkoa wa Tanga eneo la Majani Mapana.

Ilieleza kuwa mitambo ya zamani ya mafuta ambayo ipo TANESCO Ubungo ilisimamishwa kwa kipindi kirefu na haiwezi kutumika kwa sasa kwa kuwa ilishaharibika na vipuri vyake havipatikani kwenye soko na teknolojia yake imepitwa na wakati.

Ilieleza kuwa gharama za kuikarabati mitambo hiyo ni kubwa ukilinganisha na gharama za kununua mitambo mingine mikubwa na mipya.

Kumekuwapo na maoni mbalimbali ya wadau wakiitaka TANESCO kukataa maombi ya Symbion kuiuzia umeme, kwa madai kuwa kinachofanyika ni kiini macho kwa kuwa mradi huo ni sawa na ule wa Dowans na Richmond uliokataliwa na bunge, serikali pamoja na wananchi.

Kulingana na madai hayo ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakikanushwa na TANESCO, ni kuwa kila unapoibuka mgawo wa umeme, suala la Dowans hujitokeza, hivi sasa likiwa limejitokeza kwa jila la Symbion Power.

Gazeti hili liliwahi kuandika habari kuwa kwa muda mrefu kulikuwa na hujuma miongoni mwa wafanyakazi wa TANESCO zilizofadhiliwa na mmoja wa wafanyanyabiashara wakubwa nchini, ili kuhujumu baadhi ya miundombonu na kusababisha mgawo wa umeme, kwa lengo la kushinikiza shirika hilo ama kununua umeme au mitambo anayohusishwa nayo.
 
MAFISADI HAWANA JIPYA WAMEDODA NA WAMEFULIA KISIASA..........................., bado naendelea kuamini kwamba mafisadi hawana jipya na watazidi kuchemsha na kundi lao lote na vijana wao wote wao ndio wanaopanga njama na kumuingiza madarakani kijana wao kutoka visiwani JAMAL KASSIM kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mh Masauni(Mb) naamini hawatafanikiwa hata kidogo....nasema hata kidogo.

-wacha wamnunulia Kubenea hata JUMBO MASHINE PRINTER nini hicho kikoroboi cha milioni 20-30, ila njama wanazozipanga hazitafua dafu hata kidogo wanaplan nyingi kuliko uwezo wao wa kufikiri, wanahela nyingi hawajui wazifanyie nini, wanakundi kubwa lisilo kuwa na tija, hakuna watakalofanikiwa hao. plan wanazotumia kumuingiza JAMAL KASSIM kuwa mwenyekiti UVCCM hazitafua dafu ni bora litibuke tusubiri mwakani 2012 kuliko hizo njama zao, kikao kilichokaliwa na hao vijana wao wa mwmvulia chini ya HUSSEN BASHE BASHE wasidhani havijulikani vinajulikana na wanayoyafanya yanajulikana.

-WANAPINGO KAMA IFUATAVYO: kama LOWASA hawi rais 2015 basi kijana wao EMENUEL NCHIMBI awe rais na LOWASA kuwa WAZIRI MKUU TENA hiyo ndio hesabu yao hata hili wataula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, leo wamemgeuka mwanamama wao MARY CHATANDA kwa kuwa hakuweza kumsaidia demu wao BATILDA BURIAN kuwa mbunge ARUSHA MJINI sasa imekula kwao waendelee kuvurugana tu na kijana wao JAMES MILLYA mwalimu sijui shule ipi ya sekondari aendelee kutumika utadhani sio mmasai halisi.

-wanamthumu kijana wa watu bure MRISHO GAMBO bila sababu yeyote japo naye mwanzo alikuwa wao lakini hawakumpenda na baadae amejua ukweli sasa wanamuona mbaya, nchii kila aliyekataliwa na BABA W TAIFA MWALIM JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNA ATAKACHOFANYA KIKAKUBALIKA MILELE hata kama utamfanyia mtu madhali ni ww unafanya itakula kwako na hao unaowafanyia.

-LOWASA ALISHAKATALIWA NA BABA WA TAIFA watanzania wanajua hilo....................., Mzee kambarage alishawahi toa hundi ya DOLLA LAKI TANO AMBAYO LOWASA ALIHONGWA NA WAHINDI KUKIUZA KIPANDE CHA ARDHI LEO NDIO KUNA SHULE YA AGKHAN MZIZIMA PRIMARY SCHOOL, hii lilikuwa MKUTANO MKUU WA HALMASHAURI KUU 1995 watanzania hawajasahau na hawatasahau hilo. wakati huo alikuwa WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO.

-KUBENEA ATAKULA NAO SAHANI MOJA PAMOJA NA KUNUNULIWA HUO MTAMBO na hao aliotajiwa kuwashughulikiwa haita tokea mbona wanamiliki MAGAZETI YAO YA TAZAMA linatoka kila JUMANNE NA LIMESHINDWA KUFUA DAFU, WANAMILIKI MKAKATI linatoka kila IJUMAA nalo limeshindwa kufua DAFU? NINI WANATAPA TAPA HAWA WATU? WAMEFULA.

-WAMEKULA YA MBUZI WATAOTA MAPEMBE.............................!!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Ilielezwa wiki hii na Tanesco na Wizara kupitia kina Badru, Mhando na Ngeleja kuwa mgao wa umeme ungeisha leo baada ya kuanza kuzalisha gas ya songosongo. Hadi sasa kuna mgao wa umeme. Makamba na kamati yake wanasemaje kuhusu hili? Maana mara ya mwisho waliwabana sana and they promised to keep their word. What happens now that they did not keep their word?
 
Kuendelea kuamini kauli za serikali hii ni kupoteza muda wako wenye thamani
 
Endelea kusubiri mkuu, saa mbili usiku bado haijafika. Hata hivyo kesho kwa waTZ means mwezi kesho au zaidi.
Hata hivyo kwa baadhi ya maeneo mgawo umeshapungua makali, subiri subir na wewe neema itakufikia punde. lol.
 
Nimekuwa nafuatilia hii sinema ya umeme kwa takribani miaka 6 sasa. Mimi kama mdau mkubwa wa umeme nimeona, na nafikiri waziri husika, mh Ngeleja ajiuzulu kwa sababu utendaji wake hauna tija kwa taifa.

1. Hapo alipo hana fikra kabisa za kutatua suala la umeme kwa wananchi zaidi ya kukaribisha makampuni toka marekani kuja kuwekeza kwenye sekta hii nyeti. Hii ni kwa sababu makampuni haya hayaji kutupatia umeme bure, tunanunua, na inatakiwa angalau kila Mtanzania aweze kutumia nishati hii muhimu kwa maendeleo ya nchi, na mwananchi mmojammoja. HANA MKAKATI HUO
2. Suala la kuimarisha vyanzo vya uzalishaji nishati hapa Tanzania halipo kabisa katika mikakati yake. Anawaza MAJENERETA TOKA MAREKANI. Stigler's gorge, imelala muda wote. Kiwira ndo basi tena (kama mh zito hatakomaa, nayo itauzwa tena kwa wamarekani
3. Yeye kama waziri amefikia hatua ya kuwa msemaji wa TANESCO. Kama anaona hio kazi inafaa basi alipeleke wizarani kwake hilo shirika linaloelekea kuzimu

INAVYOONEKANA, NGELEJA amewekwa pale ili kuficha maovu yanayoendelea kuneemesha watu kupitia sekta ya umeme (NA MADINI). MRADI MKUBWA ULIOWATAJIRISHA MAFISADI TANZANIA KATIKA AWAMU YA JK NI UMEME JAMANI. Na yeye analifahamu hili.

Kama hatatoka mwenyewe asubiri kuwa kama Karamagi, tutakuzomea njiani ukipita, huyooo, huyooo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom