Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

Aibu kubwa! Chakufanya mgao ufanyike hadi nyumbani kwa mkuu wa mawaziri pia posho ya mafuta kwa genset no then tuone! Pia posho ya wabunge ikiondolewa njaa ikachukuwa mkondo hawatatetea wizi na upumbupumbavu wa wanaaokula pesa za watz bila huruma kwani huwezi mtetea mwenyekula wakati una njaa .
 
Nawashangaa wana magwanda kuwa mpaka sasa hivi bado hawajanasibisha kuingia kwa mitambo mipya ya umeme leo hii na kujiuzulu kwa Rostam jana.

Hamuoni kuwa RA kawazidi ujanja, jana changa la macho leo anaingiza mitambo mipya, haya anzeni majungu.
 
Hivi huyo jamaa alipewa hiyo nafasi ya nini?natamani nimface alafu niteme sumu iliyojaa kifuani kwangu.
Ngeleja nae kondoo wa kafara tu,hata aje nani!Peke yake hawezi,waliomuweka ndio wanajua kiini cha tatizo na jinsi ya kulimaliza. Ye nae anang'ang'ania nini? Zigo limemshinda awarudishie wenyewe.
 
Hawez kumfukuza Ngeleja, wote ni wanamtandao. Labda tutegemeea apate ajali ya kisiasa unless otherwise untill the final whistle
 
kesho I hope kwa mapenzi ya Mungu,ni ama za Ngeleja au za Wabunge makini wenye kulitakia mema taifa mama la Tanzania.wabunge wote pasipo kujali vyama au itikadi wala vyama wote kusimama kwa pamoja kuwa sasa zama za kifisadi kwenye umeme zimekwisha.Jamani wabunge wa Bunge letu tukufu kesho ndio kwa mala ya kwanza watende yale ambayo jamii haijawai kuyaona pale ambapo Wabunge wote kwa pamoja wanamuomba Ngeleja kuachia ngazi ili rais achague mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom