Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

Hivi wakuu !!!!jmani Rais wetu halioni hili tatizo!!!au kwa vile ss tunaabudu sna amani!!!!!ni jambo la kushangaza sna....
 
Hivi wakuu !!!!jmani Rais wetu halioni hili tatizo!!!au kwa vile ss tunaabudu sna amani!!!!!ni jambo la kushangaza sna....

Rais wako hakai nchini kila siku anakula misele kwenda kula bata kwenye nchi zenye umeme atajuje matatizo ya nchini kwake?
 
Sio nyie mlioipa ushindi ccm? Na bado miaka minne ya tabu inakuja. Hebu tunyamazieni hapa, wengne tuna hasira za karibu
 
Wakuu hii nchi kwakweli sielewi tunakoelekea kuna mgao wa umeme unaoendelea kwa saa 24 kila siku huku mikoani ambao hauko katika ratiba iliyotolewa magazetini wiki hii umeme unakatwa saa 12 jioni na haurudi hadi kesho yake saa 12 jioni na hapo kesho yake asubuhi unakatwa tena huku tunaelekea wapi jamani naona maisha sasa ni magumu ajabu.

Nilipita mtaani kazi zote zimesimama vijana wamekaa wanatazamana hali ikiendelea hivi vijana hawa ambao kazi zao zimechukuliwa na mgao wa umeme wataamua kufanya kazi usiku ya kutukaba na kuvunja vijumba vyetu amani itatoweka kabisa muda si mrefu hakuna tena usalama na ukizingatia usiku mzima giza mgao huu utaongeza pia mimba zisizotarajiwa na kuongeza idadi ya watu katika familia ambao ni mzigo na kuzidisha umasikini kwakuwa sasa usiku klwakuwa hakuna umeme itakuwa full mchezo wa baba na mama!! Serikali mpoo kuna janga kubwa mbele yetu!


mkuu, kuna majenerator...
serikali imewashinda sema bado wanang'ang'ania!
 
Hivi kweli jaman kwa mwendo huu tutaendelea lini jamani?! Tanesco wanalipwa bure bila ya kuzalisha chochote!
 
hivi wanachama wa Magamba nao wanataabika na umeme? mi nilijua wao hauwahusu kumbe upumbavu wao tunalia wote.
 
Mda sio mrefu watu tutaingia kitaa na kujinyakulia utawala wa mitaa kwa namna hii, kwa hali hii ipo siku mtu atatolewa utumbo mbele ya umati wa watu shauri yao, wasione tumekaa kimya tu twa tunga sheria za namna ya kupambana nao

Tatizo suala la accountability halipo hapa nchini. Kwa hili la umeme ilbidi Ngereja awe alikwisha jiuzuru muda mrefu. Tumeshuhudia watu wakiuawa hovyo na polisi, tumeshuhudia mabomu ya mbagala, gongo la mboto lakini wahusika wapo kimya as if hakuna kilichotokea. Lakini I hope siku itafika wananchi wachoka na kuingia mtaani na hilo ndio litakuwa suluhisho.
 
Mkuu hii nchi mbona isha uzwa kitambo sana,ww ulikua hujui.kalaga baho,bado tunasafari ndefu sana kufikia mahali jamaa wengine wapo,mm binafc nina wacwac na viongoz wetu,kwa sbb hatuwez kua tunazungumzia umeme na ikawa issue kubwa namna hii kwa watu zaid ya milion 40.sasa kwa shida kama hii wanashindwa wataweza kuwasaidia akina mama wajawazito huko vijijini.umefika wakat kwa kubadilisha hiyo safu ya uongoz.lakin ktk hili lazima tuwe wamoja ndio tutafanikiwa.kuna wkt inaniuma sana ninapo sikiliza siasa za Tanzania.watu na wakubwa huko juu wapo kimasilahi zaid na kusahau kabisa TANZANIA YAO
 
mie hata sielewi huu usanii wa serikali yetu, long since imeingia madarakani inatangaza tatizo la umeme ni janga la taifa...janga ktu gani bwana! huu usanii wao tu manbo ya =sha washinda kinachotakiwa sasa ni kutumia ubabe tu, kiongoz hakidhi haja za watu maneno kibao kuongea mambo ambayo hata yeye mwenyewe hayajui, kucheka cheka tu luningani mie nadhan anaambiwa sema hichi nas hichi usisema yeye bila kufuatilia anaropoka tu, kesi za umeme tangu na tangu, mitambo inaletwa na madege makubwa ila hatuono msaaada wowote kwa wananchi, aaaaah mie wananiboa hasira zikizid naingia naingia barabaran ikishindikana msituni tu, coz mie ntakufa sijawahi enjoy life kwenye nchi yangu sasa mambo gani haya wana jf
 
Kumbukeni alisema: "Mwinyi kakaa miaka 10, hakuyamaliza, Mkapa miaka 10 hakuyamaliza, mimi nimemaliza miaka 5 na hiyo mingine........... (sina hakika kama atafika 2015), nina hakika hata mimi sitayamaliza matatizo haya ya waTZ"
 
Hata mimi nashangaa......Sijui ni kwa nini kila kampuni mpya ya uzalishaji umeme inapotaka kuingia mkataba na TANESCO ni lazima kutokee mgao mkubwa wa umeme.....Angalia tangu ujio wa awali wa hawa Aggreko, Richmond/Dowans, Symbion na sasa hawa Aggreko tena mara kampuni hizi zinapotaka kusaini mkataba na TANESCO ni lazima nchi iingizwe kwenye mgao mkubwa sana wa umeme.........Au ndio mambo ya kuwaaminisha wananchi kwamba kuna upungufu mkubwa sana wa umeme kwa lengo la kuhalalisha ulaji?...

Inasikitisha sana aisee......

What a coincidence......

Tafakari.....................

na bado,tutaona vituko vingi juu ya Tanesco,wameamuwa sasa na wataingia mikataba feki mingi sana wakati huu,kama hatuamini tusubiri tutaona
 
Huu ni ufisadi wa hali ya juu! TANESCO inaweza kabisa kujitegemea na kuzalisha umeme wake wa kutosha kabisa bila kusaini mkataba na kampuni yoyote ile ya ufuaji wa umeme na hili liliwezekana miaka ya nyuma kabla ya matatizo ya umeme kuanza rasmi mwaka 1992. Sasa hivi kuna utitiri wa makampuni ukiongezeka kila kukicha IPTL, Symbion, Aggreko na wale wa Canada wanaovuna gas yetu kwa bei poa kabisa kisha kuwalangua TANESCO kwa bei ya juu tena in forex!
 
Aggreko, Glasgow-based temporary power firm said it had signed a deal with the Tanzania Electric Supply Company to provide 100MW of power for 12 months.

Aggreko will supply two 50MW diesel-powered plants at Ubungo and Tegeta, as well as manage fuel supply.

Aggreko said the exact value of the contract would depend on the monthly price of diesel and the amount of power generated. The firm will charge "a small fee" for managing the fuel supply.

The Scottish firm said the addition of 100MW of power would help stabilise the country's power supply and support continued economic growth while the Tanzania Electric Supply Company worked to implement long-term solutions to improve power generation and distribution.

Aggreko chief executive, Rupert Soames, said: "Having successfully delivered 40MW of emergency power between 2006 and 2008, we are delighted that - following a competitive tender process - we have once again been selected to be of service to Tanzania." This latest contract will take Aggreko's order intake in the first six months of 2011 to at least 630MW.



kama mnakumbuka,walizima umeme wakasaini mkataba na symbion power,sasa tena zima umeme wamesaini mkataba na hao jamaa,hiyo ndiyo tabia mpya ya kuingia mikataba

................ mie pia nilihisi kuna ka mtego, maana mgao kisha symbion, mama clinton now aggreko ! .............. daaah ! mmetuweka kwenye kilengeo !?
 
Posho wanayong'ang'ania wabunge inatosha kununulia mitambo mipya ya umeme lakini tanzania bahati mbaya hatuna wazalendo,
 
Hali ni hiyohiyo ,mfano morogoro kuna maeneo kila siku mgao kuanzia asubuhi hadi saa 6 hadi 8 usiku wala hakuna kubadilishana hii ni rushwa kwa tanesco, wanafunzi hawasomi usiku,hali ni mbaya natabiri maandamano wakati wowote kuanzia sasa yatafanyika kudai umeme ni haki yetu kuupata
 
Back
Top Bottom