Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

kuna ushahidi hapa?au unafuata mkumbo tu kwa kuwa unaemwamini wewe hapa JF anapinga nawe unapinga?tuangalie tusije kufanywa wafuasi ka wa kibwetele..!

Katika gazeti la THISDAY la leo 6/6/09, kuna lead article chini ya kichwa "Controversy over Peter Noni's new appointment" Anagalia hizi extracts:

Ezxtract 1 : "Previously, he (Noni) served as BOT's Director of Economic Policy, where he was among key central bank officials involved in the processing of payments from the EPA account"

Extract 2 : "The BOT officials on trial in the case are Ms Ester Mary Komu, Imani David Akim Mwakosya, and Bosco Ndimbo Kimela, with Noni testifying against them as their former boss."

Extract 3 : "An audit report by Ernst & Young named several senior BOT officials who held the following positions between June 2005 and July 2006 as beind "directly or indirectly" implicated in the EPA scandal:
The Governor (ballali), Director of Fianance, Secretary to the Board (two different officers served in this capacity during the period under review), Dirctor of Economic Policy (two different officers served in this capacity during the period under review), Deputy Director of the Debt Department (two different officers served as DDDD during the period under review), and Head of Bilateral and Commercial Debt."


Extract 4 : "The audit report reccommended disciplinary action to be taken against all BOT officials involved in the actions of "initiating, processing, authorizing and approving" the dubious EPA payments."
 
Kwani hakuna Mtz mwingine anaweza kuchukua nafasi ya TIB?

Ni Noni tu??

JF itumike ktk vetting as Bunge letu wamelala!
 
The ex TIB MD had suggested of advertising for his position but fell on deaf ears of MoFE.
Good governance calls for those kind of positions to be advertised (transparency) and the board should be the one to choose.
MD is supposed to be answerable to the board.
Noni is answerable to whom? The Minister or Ikulu? He (Noni) , may also now dictate who are to be his board members.
 
The ex TIB MD had suggested of advertising for his position but fell on deaf ears of MoFE.
Good governance calls for those kind of positions to be advertised (transparency) and the board should be the one to choose.
MD is supposed to be answerable to the board.
Noni is answerable to whom? The Minister or Ikulu? He (Noni) , may also now dictate who are to be his board members.

Nafikiri adui mkubwa wa nchi yetu ni mawazo mgando ya baadhi ya watawala. Wao fikra zao wao kila siku nafasi kama hizi ni za ulaji, na hivyo hawapo tayari kuona mtu ambaye si wao anakula. Mpaka tukiondoa watu wenye fikra hizi kutuamulia na kuacha standards zichukue nafasi hapo ndipo tutashuhudia uwajibikaji kamili.

Yaani kila kitu mtu kabla ya kutoa maamuzi anafikiria inaninufaisha vipi mimi na siyo itanufaisha vipi nchi.
 
kweli utetezi unaotolewa ni wa nguvu sana na inatia shaka,kama ni mtu mwadilifu sidhani kama inahitaji nguvu kubwa kiasi hicho kutetea uadilifu na uchapa kazi wa mtu.mkumbuke kuwa tuliomo humu JF tupo kwa maslahi ya nchi na sio babamdogo au jamaa.
 
Noni through his voda-shares-rostam-CCM-BOT-EPA(inside man wakina rostam BOT)-Promotion-TIB.. Noni is a billionaire about to get richer, lifestyle yake kwa tunayoijua ni top-class. Jamaa mkimya.humskii but Noni=NOMA!
 
Maajabu katika pita pita kwenye website ya Twiga cement kumbe Mlaki ni board mamber na ana shares Twiga Cement? sikujua!!! nimeelimika sasa.
Pia Noni ana shares Vodacom?
 
Kwenye Mwanahalisi Online kuna hadithi ya kuiva kwa Richmond nyingine. Miaka minne iliyopita, wakati EPA inafukuta sana, uhusika wa huyu Noni katika wizi huo ulionekana kuwa dhahiri sana na tulishangaa sana alipoteuliwa na Rais kIKWETE awe mkurugenzi wa TIB, ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kulinda fedha za EPA zitakazorudishwa na Wezi wa EPA. Watu wengi waiochangia hapa JF walionyesha kutokukubaliana kabisa na uteuzi huo ikionekana kuwa kweli ilikuwa ni namna ya kuficha ukweli.

Miaka miwili baadaye, ukazuka ugomvi mkubwa sana baina ya Mwakyembe na Rostam ambao tulitaarifiwa kuwa ulikuwa unatokana na kushindana kuhusu kupata enelo la kuzalisha umeme wa upepo huko Singida; kumbe kulikuwa na hii kampuni ya umemem ya Noni pia!.

Kwenye profile ya Noni hapa chini inaonekana kuwepo kwa uhusiano wa karibu baina yake na familia ya Kikwete, ambaye ni Rais wa Tanzania, na Rostam, ambaye ndiye aliyetuhumiwa kuwa nyuma ya wizi wa EPA kupitia Kagoda. Wakati wa uchaguzi wa mwaka jana kampuni ya Six Telecoms inajulikana sana kusambaza barua pepe za kutishia watu kuhusu Dr. Slaa, nadhnani kwa vile alikuwa amehadi kushughulikia wezi hao kwa nguvu sana iwapo angeingia Ikulu.

[h=1]Richmond nyingine yaiva
[/h]


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 24 August 2011

http://mwanahalisi.co.tz/print/richmond_nyingine_yaiva
noni.jpg




SERIKALI iko mbioni kufunga mkataba wa kufua umeme ambao tayari umeonekana utakuwa na utata. Mkataba huo ni kati yake na kampuni ya Karpowership Limited ambayo inamilikiwa na Peter Noni.


Noni ni mmoja wa watuhumiwa wakuu wa wizi wa fedha za umma kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).


Kwa sasa, Noni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB), ambako Rais Jakaya Kikwete alisema zitahifadhiwa fedha zilizoibwa kwenye akaunti ya EPA ambazo zinarejeshwa kwa mkataba maalum kati ya wezi na serikali.



Wakati fedha hizo zinakwapuliwa BoT, Noni alikuwa mkuu wa idara ya fedha za nje iliyohusika na fedha hizo.


Taarifa zinasema mradi huo kwa sasa uko katika hatua ya majadiliano kati ya serikali, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya Noni – Karpowership Ltd.


Kwa mujibu wa nyaraka ambazo gazeti hili limepata, serikali na kampuni ya Noni wamepanga kufunga mkataba wa kutumia jenereta zinazofungwa kwenye meli eneo la Bandari za Dar es Salaam na Tanga.



Utekelezaji wa mkataba huo umepangwa kuwa kati ya miezi 24 (miaka miwili) na miezi 36 (miaka mitatu) kutegemea makubaliano ya mwisho yatakavyoelekeza.



Kampuni ya Karpowership Limited imeahidi kuzalisha megawati 160 jijini Dar es Salaam na megawati 90 mkoani Tanga.



Msisitizo wa TANESCO katika muda huo unakuja kwa kuzingatia kuwa shirika hilo limelenga utekelezaji wa mkataba huo uendane na muda ambao serikali imeahidi kumaliza tatizo la uhaba mkubwa wa umeme nchini – Desemba mwaka huu.



Utekelezaji wa mkataba huo, hata hivyo, utahusisha pia idhini za matumizi ya miundombinu ya njia ya reli na bandari.



Hii ina maana ya kuwepo mawasiliano ya kina baina ya TANESCO na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya reli nchini (TRL).



Taarifa za kuwapo mradi huu zimekuja wiki moja baada ya serikali kufunga mkataba wa kununua jenereta za kuzalisha umeme zenye kutumia mafuta, huku ikishindwa kuendesha mitambo ya umeme ya IPTL iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.



Kila upande katika mkataba una wajibu wa kufanya mawasiliano hayo kwa ajili ya kufanikisha kupatikana kwa idhini ya kutumia miundombinu ya mashirika hayo mawili ya umma, kulingana na majadiliano yanavyoonesha.


Taarifa zaidi kuhusu majadiliano ya TANESCO na Karpowership Limited zinasema bei halisi ya mradi huo haijaamuliwa kwa kuwa mvutano uliopo katika utaratibu wa malipo ulikuwa haujasawazishwa.


Awali, TANESCO ilikuwa tayari kutoa garantii ya mkopo wa dola 57,290 (kiasi cha Sh. 70 milioni) kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya kuendeshea jenereta hizo za kwenye meli.



Msimamo wa Karpowership Limited ni kupata dola 75,000 (kiasi cha Sh. 90 milioni) kwa ajili ya kukidhi gharama za mafuta na uendeshaji mitambo yake.



Baadaye, pande hizo zilifikia pendekezo kwamba malipo yafanywe kwa kuzingatia kiwango cha kilowati moja senti 26.16 ya dola kwa kufuatia bei ya ununuzi wa mafuta ya dola 690 kwa tani moja.



TANESCO ilitaka kutumia bei hiyo lakini kwa kuzingatia asilimia 75 ya umeme utakaozalishwa Dar es Salaam kwa kutumia jenereta lenye uwezo wa kutoa megawati 100.



Karpowership ilisema itatangulia kuleta jenereta ya megawati 100. Vielelezo vinaonyesha mradi huo utagharamiwa kwa utaratibu wa malipo ya asilimia 75 ya gharama za utunzaji mitambo iwapo Karpowership watalipwa malipo ya awali ya dola 30,000 (kiasi cha Sh. 45 milioni) na kupata garantii ya kukopa dola 75,000 (kiasi cha Sh. 90 milioni).


Iwapo Karpowership watakubaliwa kubadilisha mtambo ndani ya mwaka mmoja, basi malipo yawe asilimia 75; bila TANESCO kuwapa dhamana ya kukopa benki.


TANESCO kwa upande mwingine imetaka ilipe asilimia 75 ya gharama za umeme utakaokuwa unazalishwa kutoka mwanzo wa mkataba hadi Desemba mwaka huu.



Gharama zitabaki hivyo pamoja na Karpowership kuongeza mtambo wa megawati 60 unaopangwa kuwekwa jijini Tanga.



Tatizo linalojitokeza ni kwamba serikali imejiingiza katika mradi ambao utaigharimu fedha nyingi kwa vile tayari ina mzigo wa kugharamia mitambo ya mafuta mazito (IDO) ya IPTL inayonyonya kiasi cha Sh. 40 bilioni kila mwezi.


Mradi huo unaenda sambamba na mradi mwingine wa uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta mazito uliosainiwa kati ya serikali na kampuni ya Aggreko. Huu utatekelezwa jijini Mwanza.


Miradi hiyo ni miongoni mwa miradi iliyotajwa na serikali bungeni katika kutafuta ufumbuzi wa haraka wa tatizo kubwa la uhaba wa umeme nchini lililosababishwa na mambo kadhaa ikiwemo upungufu wa maji katika mabwawa ya TANESCO ya Mtera, Kihansi na Pangani.



Katika hatua nyingine, nyaraka zinaonyesha kuwa Karpowership itagharamia ufungaji wa njia kubwa inayosafirisha kilovoti 132 za umeme kutoka kituo cha TANESCO Ilala mpaka bandarini Dar es Salaam.



Noni ambaye aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Bodi ya Benki Kuu kabla ya kuteuliwa kuongoza Benki ya Raslimali, anatajwa kumiliki au kuwa na hisa katika kampuni mbalimbali nchini.



Kampuni hizo ni pamoja na HotSpot, Planetel, PEM Ltd na Six Telecom (Tanzania) yenye ubia na kampuni za kimataifa zinazotekeleza mradi wa kuzalisha megawati 100 za umeme kutokana na upepo mkoani Singida.



Mradi wa umeme wa upepo unatekelezwa na kampuni ya Wind East Africa Ltd (WIND EA), chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia iliyotoa mkopo kwao.



Hata hivyo, historia ya utendaji wa shaka kuhusu Noni inadaiwa kuwastua wakuu wa Benki ya Dunia walipokuta jina lake limo miongoni mwa wamiliki hisa katika mradi wa kuzalisha umeme wa upepo – WIND EA ambao walikuwa wakijadili jinsi ya kuupa fedha.



Nyaraka zinaonyesha kuwa washirika wa WIND EA walilazimika kukubali kufanya marekebisho ya mgawanyo wa hisa ili kuiridhisha benki ya dunia na mmoja wa washirika hao aliahidi kusalimisha taarifa zote zinazohusu mamlaka ya Noni katika kampuni.



Kampuni nyingine yenye hisa katika WIND EA inatajwa kuwa ni Kentec ya Denmark yenye hisa asilimia 10.


Kulingana na makubaliano ya maandalizi ya kubuni mradi huo yaliyofikiwa Agosti 2009, Six Telecoms watahodhi asilimia 45 ya hisa, Kentec asilimia 5 na Aldwych International ya Uingereza hisa 50 katika WIND EA.

Washirika wa Noni katika umiliki wa Six Telecom wanatajwa kuwa ni pamoja na Rashid Shamte. Nyaraka zinaonyesha kuwa Noni anamiliki pia mashamba yaliyoko Kabuku, Korogwe na Handeni, mkoani Tanga kupitia PEM Ltd.

Kampuni ya Aldwych inafungamana na matajiri wenye biashara Afrika Kusini, Uholanzi na Mauritius
 
katika gazeti la thisday la leo 6/6/09, kuna lead article chini ya kichwa "controversy over peter noni's new appointment" anagalia hizi extracts:

Ezxtract 1 : "previously, he (noni) served as bot's director of economic policy, where he was among key central bank officials involved in the processing of payments from the epa account"

extract 2 : "the bot officials on trial in the case are ms ester mary komu, imani david akim mwakosya, and bosco ndimbo kimela, with noni testifying against them as their former boss."

extract 3 : "an audit report by ernst & young named several senior bot officials who held the following positions between june 2005 and july 2006 as beind "directly or indirectly" implicated in the epa scandal:
The governor (ballali), director of fianance, secretary to the board (two different officers served in this capacity during the period under review), dirctor of economic policy (two different officers served in this capacity during the period under review), deputy director of the debt department (two different officers served as dddd during the period under review), and head of bilateral and commercial debt."


extract 4 : "the audit report reccommended disciplinary action to be taken against all bot officials involved in the actions of "initiating, processing, authorizing and approving" the dubious epa payments."

huyu na deo kweka na lyumba ndie waliemuweka kikwete madarakani hata huyo rostam kama sio watu wanne akiwemo huyu wasingeiba huko epa hii ni ka info tu huyu hana hela mbaya ...nyie si mlisema kikwete katoka kwa mungu sasa mungu lazima atumie waja wake kama hawa kufanikisha mawazo yenu mkitaka kumuondoa mnatakiwa mkasafishe maombi yenu kwanza mliodai kikwete kachaguliwa na mungu sjuui wa bagamoyo ama yupi
 
huyu na deo kweka na lyumba ndie waliemuweka kikwete madarakani hata huyo rostam kama sio watu wanne akiwemo huyu wasingeiba huko epa hii ni ka info tu huyu hana hela mbaya ...nyie si mlisema kikwete katoka kwa mungu sasa mungu lazima atumie waja wake kama hawa kufanikisha mawazo yenu mkitaka kumuondoa mnatakiwa mkasafishe maombi yenu kwanza mliodai kikwete kachaguliwa na mungu sjuui wa bagamoyo ama yupi

Sawa tumekusikia mkuu, ila nayeye 40 zake zipo njiani...
 
Nimerudi na kusoma maoni yangu kwenye hii mada the first day Noni alipoteuliwa... Nimejikuta nimegubikwa na huzuni.
Mzee Mwanakijiji, pole kwa kugubikwa na huzuni, hii ndiyo Tanzania yetu, hawa ndio viongozi wetu tuliowachagua wenyewe kwa ridhaa yetu, hapa ndipo walipotufikisha, na tunasubiri kwa hamu wapokezane vijiti 2015 tuwape miaka mitano mingine waendelee kutupeleka kule wanapotakiwa kutufikisha.

Mungu ibariki Tanzania.

Pasco.
 
Hivi kweli Rais Kikwete alipomteua Noni alikuwa hajui uhusika wake na EPA? au alipuuzia?
 
Back
Top Bottom