Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

Mie nashangaa kabisa hamjui ni nini kinaendelea.

2010 ni mwaka wa Uchaguzi,zinatafutwa pesa za kampeni zitatoka wapi?hivi mmesahau zile pesa za EPA zilizorudishwa zilipelekwa wapi??I mean Benki Gani?TIB.

Endeleeni kusumbuka na kujiuliza ila tunaojua nchi vizuri tunajua nini kinafanyika hivi sasa na kuna wakurugenzi wengi watabadilishwa ili kufanikisha abadhi ya mambo!
 
Kwani lile changa la macho tulilopigwa kuwa fedha zilizorudishwa za EPA zimewekwa TIB mlitegemea nini????? Ngoja muone miujiza sasa!!!!!
Mkuu,ile mihela iliyorudishwa ya EPA iko TIB? na mzee nanihii ambaye alikuwa nanhii benki nene wakati wa skandali la nanhii ndo katumwa ailinde hiyo mihela,du,ndo ya chui akamlinde mwanambuzi? I am speechless!
 
My Take:
Kama huyu jamaa kweli ana chembe yoyote ya kile kinachoitwa Uadilifu, atakataa nafasi hii aliyoteuliwa hadi kesi ya EPA itakapokwisha na Rais ataacha huu mchezo wa kuinfluence the course of justice kwa kumteua mmoja wa washtakiwa katika nafasi kubwa ya kusimamia benki ambayo imepokea fedha zinazohusika katika mashtaka ambayo yeye (noni) ni shahidi.

This is a classic example of travesty of justice.[/QUOTE
]

MMKJ,nadhani unataka kulazimisha jambo ambalo hata mtoto wa primary analo jibu lake,vipi akatae uteuzi wakati yeye ni shahidi tu?hiyo kesi ya EPA hata ikiisha vipi NONI haitamgusa kwa kuwa akishatoa ushahidi wake ataondoka kisha atakuja shahidi wa pili na watatu....etc wa serikali,....SHAHIDI ATAENDELEA KUWA SHAHIDI NA MSHITAKIWA ATAENDELEA KUWA MSHITAKIWA
Hapo HAPANA Mkulu,unapotosha wasomaji.
Kisheria SHAHIDI ANAWEZA KUGEUKA KUWA MSHITAKIWA.
Tuwe makini tunapobonyeza vitufe vya keyboard zetu na tuheshimu tasnia za watu.
Kama jambo hulielewi ,usilisemee.
 
Mchezo ni uleule wa EPA, sasa hivi wanahamishia kambi TIB na wanampeleka huyu jamaa huko kwa utekelezaji. Utasikia PESA nyingi zimepelkwa huko kwa ajili ya kusaidia kilimo na kisha kingmaker kama kawaida yake atachota na kuweka mfukoni mwake na kuwagawia CCM kidogo kwa ajiili ya kampeni.

Hiyo kampeni tayari imezinduliwa juzi hapa Dar. inakwenda kwa jina, "kilimo kwanza".Kuna matrilioni ya pesa yatahusika kwenye hiyo kampeni. Dots bado ziko scattered sana lakini tunaweza kuanza kuziconnect! Usishangae kusikia 'Kagoda', inarudi kwa jina la 'Kaguda' chini ya mmiliki 'Rustam" badala ya 'Rostam'.
 
sikatai na unachosema,mimi noni ni mtu wangu wa karibu sana,na juzi tu tulikuwa pamoja kwenye msiba wa mdogo wake,tukaenda bhupandagila kuzika...ila nataka kukwambia kitu,mimi sinufaiki na pesa ya noni,mi nna familia yangu,naishi vizuri tu hapa uk.kama noni akifanya madudu au nikijua madudu yake sintoacha kumchana,na pia kujua profile nzuri ya mtu kama ulivyoandika hapo juu jinsi jamaa alivyohangaika na kampuni yake mpaka leo kufika hapo haikufanyi wewe kumwita fisadi,je unajua planetel ina shareholder wangapi?
Mkulu this now is too much.Let it go.
Unakuwa mbishi mpaka unaudhi.
 
ADVOCATES OF THE DEVILS keep it up Wakuu,Sioni kitu cha kushangaza kwa sababu JK hana hulka ya kuchagua wasafi wala kuchukulia hatua wachafu na wezi wakuu.

Nakumbuka wakati fulani mwaka jana ilizungumzwa hapa JF kuhusu uozo wa mtendaji mkuu wa Benki ya Posta, hakukuwa na hatua zozote zimechukuliwa na kwa taarifa ni kwamba si tu kwamba hachukuliwi hatua bali anaongezewa mkataba wa miaka mitatu,Ni ukweli unaojulikana hapa BOT kwamba TPB management haina uwezo na inaipeleka benki pabaya,ushauri wa wakaguzi haufuatwi.

Rejea hotuba ya waziri wa Fedha kuhusu kuziongezea uwezo Benki za umma,Serikali itaanza kuipatia TIB mabilioni, then TPB ikifuatiwa na TWIGA Bancorp, hivyo basi ili kujihakikishia maisha bora 2010 ni budi wawe na watu wachafu wanaoweza kuwatumia...

BRAVO JK and RA
 
Ndugu zangu msisahau kwamba huu ndiyo utamaduni wetu.

Wakati watu wanalalamika kuhusu Zombe kwa mauaji na unyang'anyi; Mahita anampandisha cheo kuwa RPC Rukwa,

Wakati wana Shinyanga wanalalamika kuhusu mwenyekiti wao wa jumuiya ya wazazi kwa ubadhilifu, Mkapa anamteua kusafiri naye kwenye ziara za raisi,

Wakati watu wanalalamika kuhusu mzee wa vijisenti; CCM wanamteua kwenye kamati ya kuchunguza mkataba wa kifisadi wa UVCCM na jengo linaendelea kujengwa.

Wakati Hussein mwinyi alikacha JKT; anapewa kuingoza wizara ya Ulinzi na JKT!

Wakati mkuu wa wilaya ya Nyamagana anatetea uwanja usibinafsishwe na kubalishwa matumizi yake, mkulu anamstaafisha,

Wakati Mwakyembe anatetea NBC isiuzwe, wakubwa wanamuondoa kwenye bodi ya NBC,

Wakati Ibrahimu Katuma anatetea NMB isiuzwe; anaondolewa uenyekiti wa bodi,

Wakati TANESCO wanapinga kuletewa uongozi wa Net Group solution; Net group solution wanaingizwa kwa mtutu wa bunduki na virungu vya FFU

Wakati Mengi anataja majina ya mafisadi papa serikali inamjia juu na kutaka kubadilisha sera ya vyombo vya habari;

Wakati fisadi RA anataka kumtaja Mengi kama fisadi nyangumi na mkwepa kodi serikali unamruhusu kutumia TBC1.

La Jakaya kumpa ulaji Noni sio la ajabu jamani, ndiyo utamaduni wetu!
 
Mkuu Mwanakijiji, kwa kuongezea tu,

a. Kama Peter Noni ni mtu mwadilifu na alishuhudia nyaraka za uongo za makampuni ya EPA zikipitishwa mikononi mwake kutoka kwa kina Mwakosya kwenda kwa Ballali au kutoka kwa Ballali kwenda kwa Mwakosya na yeye akakaa kimya na kuacha wachote fedha kama kisimani basi ni mwoga na hana uadilifu.

Mkuu, kusema kuwa ni mwoga na hana uadilifu ni kumsifia sana. Mimi naamini kuwa kwa yote uliyoyasema hapo na kama ndivyo alivyokuwa akiyatekeleza, basi nae ni mkosefu kama wengine wanaoshitakiwa (conspiracy to crime).

Noni hawezi kujitoa kwenye chain ya utekelezaji wa malipo ya madeni ya EPA wakati nae alikuwa katikati ya chain yenyewe. Anaweza kuthibitisha ni kwa kiasi gani aligundua mapungufu (u-fake) wa kampuni zilizoomba malipo hayo? Anaweza kuthibitisha alitekeleza vipi majukumu yake kupinga/kushauri/ kuokoa wizi wa EPA kupitia kampuni hizo fake ambazo zilipita mezani kwake? Anaweza kujitoa vipi katika chain nzima ya kuhusika moja kwa moja ama vinginevyo katika sakata la EPA akiwa kama Afisa wa ngazi ya juu ambae pia alishugulikia malipo hayo?


b. Kama aliziona nyaraka hizo na mawasiliano hayo na hakujua kuwa ni za uongo na yeye akaziacha zipite na kuzikubalia badala ya kupiga kelele wakati huo kiasi kwamba mwenyewe amekiri ati alitoa mapendekezo kwa mdomo (akijua Marehemu hawezi kukanusha) kuwa mambo yasifanyike hivyo ni mtoto mdogo tu anaweza kuamini. Kama hakujua nyaraka (nyingine zipo hapa ni za uongo) kitu ambacho ni rahisi hata kwa mtu ambaye si msomi ina maana hana uwezo wa kusimamia idara nyeti na zaidi kabisa hana uwezo wa kuchambua mambo ya kiuchumi huko TIB.
Kauli ya mdomo haiwezi kuchukuliwa kama kauli endapo haiwezi kuthibitika. Hivyo, siamini kuwa aliwahi kumshauri Gavana Ballali kuhusu chochote anachodai kumshauri endapo hataweza kuthibitisha ukweli wa ushauri huo. Ni aibu kwa mtu msomi, kiongozi wa taasisi kubwa ya nchi kutumia mdomo kuwasilisha ushauri muhimu kama huo.

Kama hayo hapo juu ni ya kweli, basi ni dhahiri kuwa Rais anahamishia ugonjwa kwenye Bank ya Rasilimali Tanzania (TIB). Inaonyesha dhahiri kuwa Noni si tu kwamba si mtu makini, bali pia hana uwezo wa kuchambua mambo muhimu na kuleta tija.


c. Nakataa kabisa kuona Rais anamteua shahidi wa kesi muhimu wizi mkubwa wa mabilioni kuwa afisa wa juu wa benki nyingine wakati akiwa katika Benki Kuu aliachilia madudu yafanyike. Aidha Kikwete mwenyewe ameshiriki katika wizi huu (and I'm serious!) au yeye mwenyewe hajui kuwa Peter Noni amewahi kufanya kazi Benki Kuu wakati wa wizi wa EPA. Vinginevyo alichofanya ni kuwachezea akili watanzania kama alivyofanya kwa kumteua tena Chenge kuwa Waziri!!

Mimi ningependa kujua vigezo vilivyotumika kutomjumuisha Noni katika kesi ya EPA. Maana kwa akili ya kawaida tu, haiwezekani kuwa katika mlolongo mzima ni yeye tu asiestahili kustakiwa. Tunajua kuwa kama Gavana Ballali angekuwa hai, angeshtakiwa, Wakuu wa Idara wote waliohusika wameshitakiwa (labda kama kuna wengine ambao hawajatajwa). Ila ni Noni tu ndie alie huru na mashtaka hayo. Kivipi?

Tunaambiwa kuwa alishiriki kufanikisha wizi wa Kagoda. Je hiyo si uthibitisho wa kutosha kuona kuwa alishiriki zaidi katika wizi mwingine uliohusu EPA? Maana ni kweli kuwa pesa nyingi za EPA zilitumika kwenye uchaguzi 2005. Iweje Noni ashiriki za Kagoda tu na si nyinginezo?

Kama ni kulindana, nadhani walindwe wote na sheria ziwekwe pembeni. Tujue kuwa sheria zetu zimetuchosha. Kama ni kufuata sheria, wote waliohusika washitakiwe kwa usawa na haki.
 
this is when RA anawapeperushia "kidege" mbele ya nyuso zenu! Shahidi wa serikali ni lazima atunzwe bwana..!
Mkkj...

kwa mazingira ya utawala wetu maana ya mfumo (KATIBA) Raisi anaweza kuteua mtu nje ya mazingira yao (ukada, mwenzetu,)???????
 
Watu wanaposema RA ndio Rais wa nchi hii mnabisha!! Sasa mnaona huyu Noni ndiye aliwezesha fedha za EPA kuibiwa BOT na yeye alikuwepo kama Sanje alivyosema wakati mikataba ya Kagoda inatiwa saini pale Mirambo 50 ofisini kwa RA; halafu wapiganaji wanajidanganya kuwa Jakaya anawaunga mkono kupinga UFISADI!! Kikwete ni mdau halisi wa ufisadi nchini. Wadanganyika mkale baho.
 
Jamani wana jamii wenzangu samahanini kwa kutokuwepo mtandaone kwa muda kidogo.

Hivi ina maana Muungwana haoni kelele zote hizi wanazopigiwa hawa mafisadi.Yule aliyekuwa mkurugenzi BOT na aliyefacilitate wizi pale BOT kapewa ulaji bada ya kuiba BOT .Soma chini -

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. Peter Efraim Mayunga Noni, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kuanzia tarehe 27 Mei, 2009.

2. Hadi uteuzi wake Bwana Noni alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Utendaji (Director of Strategic Planning and Performance Review) katika Benki Kuu ya Tanzania.

3. Uteuzi huu ni kufuatia Bw. William A. Mlaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI


Source website ya wizara ya fedha-

http://www.mof.go.tz/mofdocs/anouncement/UTEUZI%20TR.pdf

Waheshimiwa Wabunge mliopo hapa hamwezi kumuuliza Waziri kwenye kikao cha Bajeti kinachokuja kuhusu kigezo kilichotumia kumteua mtu huyu ambaye alijua na kufumbia macho wizi wa EPA pale BoT ili amshauri Rais atengue uteuzi huo?

Isijekuwa wanataka kutengeneza EPA nyingine kwa ajili ya 2010 si mnakumbuka zile pesa kiduchu zilizorejeshwa na kina Jeetu Patel zimepelekwa TIB kwa ajili ya mikopo ya Kilimo? Yaani wanamteua akatumie marejesho yale aliyoya-facilitate yatoke BoT ili akayachoree ramani mpya pale TiB?
 
Nafasi kama hizi zisingekuwa za KUTEUANA. Zingetangazwa kwenye magazeti, watu wakaomba, wakafanyiwa UDAHILI, anayestahili akapewa. Pengine wanaJF walio na sifa hizi na UCHUNGU na NCHI yetu wangezipata nafasi hizi. Tukiendelea na mtindo huu wa kuteuana na kuzawadiana vyeo Tanzania itabaki kama ilivyo miaka nenda miaka rudi.
 
as long as auditor wa serikali hafanyi auditing ya fedha za vyama vya siasa....tusitegemee ccm kuacha kula mapesa ya umma.
 
Huyu Noni ni fisadi muda sasa, na si fisadi wa mapesa ni fisadi wa ngono pia yeye na yule rafiki yake fisadi mwingine ambaye ni mwanasheria, Tenga. Wamemtoa Mkono BOT hili rafiki yake Tenga hapate tenda. Scandal zake ni nyingi sana kuhusu maisha yake binafsi pia
 
Kwa kuangalia kijuu juu tu unaona rais wetu anavyotubeza waTz kiaina kwani hamna wasomi mpaka awape nafasi wale wenye vijiharufu vya ufisadi .
kigezo cha usomi mbona wako wengi wakati tunapata uhuru ndo walikuwa wachache
 
Huyu Noni ni fisadi muda sasa, na si fisadi wa mapesa ni fisadi wa ngono pia yeye na yule rafiki yake fisadi mwingine ambaye ni mwanasheria, Tenga. Wamemtoa Mkono BOT hili rafiki yake Tenga hapate tenda. Scandal zake ni nyingi sana kuhusu maisha yake binafsi pia

acha unafiki wewe
 
jk kumpoint noni ni uchafu?acha kushikiwa akili...usifikiri hiyo ni nafasi ya kisiasa,noni ameenda shule,angalia record yake na nafasi alizoshika toka ameingia BOT


Acha hizo wewe mkuu wangu, kuwa na elimu ya A kwenye vyeti si maana kuwa wewe ndiye mtendaji sana!!! Kwanza vipanga wengi huwa si watendaji wazuri. Kama kweli Peter Noni ni mtendaji au kiongozi mzuri mbona hakuweza kutumia elimu yake kuzuia wizi wa EPA. Yeye kuna watu aliwabariki pale wakapata fedha zile chafu. RA RA RA RA, oh oh oh, Noni anafahamu vema dili zake. Na kwa kuwa RA ni Rais kivuli wa Tz ni lazima atamteua Noni kupitia msemaji ceremonial!!!

Halafu wakuu, fahamu kuwa the so called TIB ndiko zile pesa za EPA zinapelekwa, zitatumika kwa uchaguzi!!! Wewe subiri!!! Kama kweli ni za kununulia au kusaidia kilimo, kwa nini zisitumike kununua na kusambaza ile Mbolea kule kiwanda cha Minjingu??? Oh Oh Oh. Kingine ni kuwa TIB itakuwa (natumaini kazi imeshamalizika year 2007/2008) a morgage bank, sasa niambie who will benefit with that??? Oh Oh mafisadi papa bwana.

Majuzi naye huyo Peter Noni, aliteuliwa tena kuwa bodi member wa taasisi fulani hivi????? Of course anayeteua bodi member kwa taasisi za serikali ni Waziri mwenye dhamana!!! Waziri alisema wazi kuwa bodi member wale waliteuliwa kwa baraka zake mwenye Nchi!!! I laughed!!!
 
Jamani wana jamii wenzangu samahanini kwa kutokuwepo mtandaone kwa muda kidogo.

Hivi ina maana Muungwana haoni kelele zote hizi wanazopigiwa hawa mafisadi.Yule aliyekuwa mkurugenzi BOT na aliyefacilitate wizi pale BOT kapewa ulaji bada ya kuiba BOT .Soma chini -

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. Peter Efraim Mayunga Noni, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kuanzia tarehe 27 Mei, 2009.

2. Hadi uteuzi wake Bwana Noni alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Utendaji (Director of Strategic Planning and Performance Review) katika Benki Kuu ya Tanzania.

3. Uteuzi huu ni kufuatia Bw. William A. Mlaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI


Source website ya wizara ya fedha-

http://www.mof.go.tz/mofdocs/anouncement/UTEUZI TR.pdf
Sina la kusema
 
c. Nakataa kabisa kuona RAis anamteua shahidi .......QUOTE]

Agenda 2010

I hate Mwanakjj by now b'coz anawaongezea Wadanganyika uvivu wa kufikiri. Hivyo itakuwa ndoto daima kutenda.

Yaani angalia; anawatafunia, anawawekea mdomoni, anawazungushia ndimi zao, wengine mpaka anawaazima na saliva!, anasukuma matonge kwenye makolomeo na sasa anataka ayasindikize matonge mpaka matumboni. Hii ni HATARI.

I hate you Mwanakijiji by NOW
 
Back
Top Bottom