nimegundua kuwa wengi hapa mnaandika ama mnashabikia tu kitu ambacho hamkijui,katika mabandiko yote sijaona hata moja lenye kumhusisha noni na ufisadi zaidi ya ushabiki tu ufisadi,ufisadi,ufisadi.
wengi humu ama hamjui au hamna history ya noni hivyo mnajaribu kuunganisha unganisha sentensi za uongo na ushabiki ili kumweka kwenye kundi la mafisadi,mmoja kasema kuhusu jaq noni kuwa swahiba na mama salma,hiyo ni kweli lakini haimfanyi kikwete kuchagua watu wabovu kwenye serikali yake.
kuna watu wamenichana sana kwenye mabandiko yao kuwa nanufaika na pesa za noni ama mimi ndio noni mwenyewe lakini nasema kwamba,kumjua na kumfahamu noni hakutonifanya nimfichie madhambi yake,namfahamu noni kuwa ni mtu mwadilifu,mwenye busara na heshima na mwenye kufuata maadili ya kazi,hivyo sintoacha kumtetea kwa nguvu zote pindi nnapoona watu ambao hawamjui wala hawajui lolote kuhusu noni wakileta ushabiki wao tu hapa wa kufuata mkumbo
nawasilisha