Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
Kwanza hii INATISHA sana. Lakini kuna mambo ya kuweka kumbukumbu sawa. Kwanza kubwa ni kuhusu kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na familia ya Rostam, Noni hakuficha share zake Mirambo, bali ameuza kwa RA aliyeamua kuhamishia zile za Caspian katika Mirambo. Wanaweza kuwa wanajua wanachokifanya kwa kuwa kuna watu wengine wako nyuma yao (viongozi wa sasa na wa zamani). Inawezekana waliamua kufanya hivyo ili waweze kutekeleza ule mpango wao wa kuuza hisa zao South Africa na tayari walikwishakutumia hisa hizo kuchukua fedha kutoka benki ya NedBank ya Afrika Kusini. Tukumbuke madudu yote ya Meremeta na Tangold, NedBank inahusishwa na wakurugenzi wa benki hiyo ni wanahisa wa Deep Green (dudu jingine).
kwa hiyo, kwa Noni kufanywa shahidi, kwa Noni kuteuliwa kwends TIB, kwa Rostam (Kagoda) kutoshitakiwa, kwa Maregesi na wengine kutoshitakiwa (japo kwa sasa) na kwa RA kutetewa kwa nguvu zote na kwa TICTS kuendelea kupeta (Karamagi&RA) tunapata picha moja kubwa ya kutisha ambayo kwa maoni yangu (wengine watafikiri kivyao) ni kwamba:
Kuna SIRI NZITO itakayokuja KUTIKISA NCHI ikiwa WATANZANIA (kokote duniani katika nafasi zote) WATAAMUA kusema SASA INATOSHA.(Nitaeleza kwa kina kwa wakati mwafaka).
Hoja ya pili ni kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB,William Mlaki: Mlaki ni mmoja w awatuhumiwa wa kesi ya wizi wa fedha za CIS akiwa na Yussuf Manji na mwanamke mmoja anayetajwa kwa jina la Rehema. Hao watatu walikuwa tayari wameandaliwa mashitaka kwa DPP, tayari kupelekwa Kisutu, tokea mwaka 2007. Jambo la kusikitisha na kutisha zaidi ni pale kesi hiyo ilipoyeyuka, na huenda sasa inaweza kufikishwa mahakamani baada ya Mlaki kustaafu (kama alivyofanywa Mgonja). Kwa muhtsari nchi hii imekuwa ya KUSADIKIKA, maana hatuna uhakika wa kitakachotokea.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI, BABA UTULINDE TUJIKOMBOE