Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

lakini mbona hii ya leo imekuwa kimya kimya sana?

Bado vyama vyote viko msibani! Naona sasa Tanzania tuenda pazuri. JK bwana kiboko. Alisema kinachomsumbua ni mgogoro wa Zanzibar: ameumaliza kwa CUF kuingia kwenye muafaka baada ya miafaka ya akina Anyaouk kushindikana. Chini ya JK ikawezekana. Sasa hapa bara na kwenyewe kukaanza kitu inaitwa maandamano.JK akauliza ni nani hao wanaandamana na kusababisha machafuko hasa Arusha akaambiwa ni CDM. Basi amewaita Ikulu ili wapate muafaka!
 
Invisible, asante kwa taarifa hii.Wanajf wenzangu, ile much anticipated photo ya wakisalimiana, nilioitafuta kwa udi na uvumba, hatimaye nimeiona!. Roho yangu imetulia, tuliyoyasema kule nyuma hatimaye yametimia! Thread ya kutimia iko mbioni kupanda. wale wote mlionitukana sana pale mwanzo nilipoeleza Chadema Yakubali Yaishe!, Yamtambua Rasmi JK!. Mlio hai niombeni msamaha, waliotamgulia nimeshawasamehe!
Naitafuta ile thread yangu ya chadema wakubali yaishe
Ili nii update!.
 
Rais wa Tanzania JK, alivyokuwa toto la mjini anawapa kwanza Kahawa na Tende then anawamaliza na Juice za Machenza...Haaa!! Hapo Chadema wanacheka cheka tu..mkutano gani wa usiku imekuwa Party..
Dogo acha kiherehere.
Angalia picha ya tatu uniambie hii ni kitchen party.
 
Jamani sisi wananchi tuwe macho tusije tukahujumiwa tukakosa chama cha upinzani cha kututetea kama walivyokosa wenzetu wa Zanzibar sasahivi wanahaha Seif na Karume walianza hivihivi chinichini.
Muafaka wa kitaifa! Maumivu ya kichwa huanza taratibu!
 
Rais Jk kakutana na Chadema Ikulu na Slaa ndani?
"Mimi ndio Rais wenu"-JK

Ritz, kwa heshima na taadhima nakuomba sana utambue kitu kimoja tu nacho ni kwamba uwe CCM, Chadema, CUF, NCCR... sote ni Watanzania kwanza. Nakuhakikishia hakuna Mtanzania hata moja anayeweza kuitakia mabaya nchi yetu hata kama tofauti za kimtazamo zinatawala mioyo ya wengi. Utani ni jambo zuri lakini kuna wakati utani katika mambo ya msingi yanayohusu uhai wa taifa letu, unaweza kuleta hali isiyoeleweka miongoni mwa jamii.

Nimekuwa nikifuatilia post zako humu ukumbini na mara nyingi nimezipuuza hasa pale zinapoonekana kutawaliwa na hali ya kutokuwa makini. Lakini, ukubali usikubali, ukweli wa mambo ni kuwa hali ya taifa katika kipindi hiki ni ngumu na tunaelekea kubaya na tunahitaji kushtukia hatma ya hii safari yetu ya hatari. Jakaya Kikwete ni Raisi, hili halina ubishi, lakini kama wananchi lazima tukubali kuwa dereva wetu huyu anaelekea kushindwa kulimudu gari.

Iwe ndani ya serikali anayoiongoza au ndani ya chama anachokiongoza, Raisi wetu kwa sababu moja ama nyingine anapwaya na hakuna dalili kuwa hali hii itabadilika kwa kumtegemea yeye tu. Ni wazi ushauri ambao amekuwa akiupata ndani ya chama na serikali umeshindwa kuinusuru nchi na sasa lazima, ataka asitake, atafute ushauri nje ya hapo. Nani mwingine wa kumpa huo ushauri kama si uongozi wa Chadema, chama pekee kisichofumbia macho udhaifu wake?
 
wakuu naona wote tumehama na tunaongelea kushikana mikono wa rais wa ukweli an rais feki. naomba mwenye dondoo atujuze kuwa Chadema waliongea nini na rais?

Nadhani wanandaa mpango wa kuunda GNU ifikapo 2015 kama walivyofanya Wazanzibari. Si unajua Wazanzibari ndio Mabwana wa Siasa ndani ya nchi hii.
 
lakini mbona hii ya leo imekuwa kimya kimya sana?

Mkuu Zumbemkuu,

Nadhani Mbowe walikutana na JK kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kumleta the Peoples president "Dr Wilbrod Peter Slaa " ikulu.


Mkuu Mwanakijiji;

Nadhani uko sahihi,haya ni maongezi ya katiba mpya.Ukifuatilia siasa za Tanzania kwa sasa CHADEMA ina watu,namaanisha watu wanaisikiliza CHADEMA.CCM imebaki na dola.Ili kuweza kuwa na "People owned Constitution" ni lazima kuwa involve CDM.Kwa hili nampongeza JK,ametambua hilo mapema kitu ambacho wana CCM wenzake wasingeweza kukubali.Kwa hili pia JK ameonesha kuendelea kutambua CDM kama a serious Party.Ukiangalia picha ya pili hapo kuna mengi ya kujifunza,Watu wote wanne wako makini kusikilizana.I think katika swala la katiba kuna haja KUBWA ya kuwa pamoja. Good CHADEMA,Good JK
 
Bado vyama vyote viko msibani! Naona sasa Tanzania tuenda pazuri. JK bwana kiboko. Alisema kinachomsumbua ni mgogoro wa Zanzibar: ameumaliza kwa CUF kuingia kwenye muafaka baada ya miafaka ya akina Anyaouk kushindikana. Chini ya JK ikawezekana. Sasa hapa bara na kwenyewe kukaanza kitu inaitwa maandamano.JK akauliza ni nani hao wanaandamana na kusababisha machafuko hasa Arusha akaambiwa ni CDM. Basi amewaita Ikulu ili wapate muafaka!


Kimbunga,
Wakati mwingine nikikusoma sikuelewi kama uko baridi au moto!
 
siasa si uadui na katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu

hongera sana viongozi wetu hapa munaonyesha kwa vitendo kuwa mnaijali ya Tanzania Tutapishana kwa hoja hatimae tutafikia muafaka kwa ajili ya Tanzania na Watanzania wote
 
Invisible na Wana JF,

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake,

Kikubwa tunataka kujua kutoka Chadema ni kitu gani kimeongelewa (Ndio ni kuhusu Mchakato wa Katiba), kimejadiliwa na ni nini Rais amekubali mapendekezo yao.

Nawapongeza pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa letu, kwa vizazi vyetu na vijavyo. Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.

Nawasilisha
 
Jamani sisi wananchi tuwe macho tusije tukahujumiwa tukakosa chama cha upinzani cha kututetea kama walivyokosa wenzetu wa Zanzibar sasahivi wanahaha Seif na Karume walianza hivihivi chinichini.
 
Ukisikia wanamme wambea na Pasco yumo mtu unaenda hadi Ifakara kuvizia picha juu ya kaburi i can't believe.
Ukisikia wanaume kama mabinti basi ndio hao kina Pasco, wanaishi mjini kwa ukanjanja tu na ubabaishaji na kuvizia semina ambazo hata hawajaalikwa, ukitaka kuwajuwa vizuri hawa makanjanja kina Pasco nenda pale Habari maelezo asubuhi ni lazima wafike pale ili kujuwa leo mnuso uko wapi, na walivyokubuhu kwa ukanjanja hadi Press card wanazo.
 
Jamani sisi wananchi tuwe macho tusije tukahujumiwa tukakosa chama cha upinzani cha kututetea kama walivyokosa wenzetu wa Zanzibar sasahivi wanahaha Seif na Karume walianza hivihivi chinichini.
Do not become a doubting Thomas. Nyerere alipokwenda UN hakuenda kusaliti maslahi ya Watanzania.
 
siasa siiiii uadui wana JF.binafsi nafarijika sana na hatua hii.hatuna sababu ya kumwaga damu,kujeruhiana kisa siasa.

Nchi maskini kama Tanzania hatuna sababu ya kuhasimiana hadi tunashindwa kusalimiana eti madaraka.nawaponeza wote kwa kuwa wana siasa wastaarabu.

Leo Dr Slaa naye amepata fursa ya kunywa juice ya ikulu lau glass moja.
 
Back
Top Bottom