Kikwete akubali kukutana na CHADEMA

Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.

Unaweza kuwa Rais wa wote kwa kutumia mabavu,udikteta na ubabe kama anavyofanya Rais Kiwete!

Ni lazima Kiwete akubali kukutana na CHADEMA maana wana mambo ya msingi wanayoyasimamia na yanakubalika kwa Watanzania walio wengi. Lazima ajue kuwa HATUKO KUUNDA KATIBA YA CCM BAALI YA WATANZANIA WOTE. Nafikiri Kiwete sasa ameanza kuona kuwa MAJI YANAANZA KUZIDI UNGA na lazima akae meza moja na upinzani ili asikie NGUVU ZA HOJA ZA CHADEMA na si HOJA ZA NGUVU za wabunge wa CCM wanaotaka kuwaburuza Watz.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana unaonyesha kuwa Kiwete alipata kura 5.2m kati ya Watanzania takribani milioni 45. Sasa wasemaje ni Rais wa wote?Ndani ya CCM yenyewe Kiwete kwa sasa hatakiwi halafu wewe unadanganya watu kuwa ni Rais wa wote,acha hizo mama.

Kiwete wako anatakiwa akubaliane na CHADEMA vile wanavyoona inafaa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Si CHADEMA tu baali hata makundi mengi ya wanaharakati na Watanzania wasio na vyama hawajakubaliana na namna Bunge la CCM linavyotaka KUWABURUZA Watanzania kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

Kiwete na CCM yake lazima wasome alama za nyakati. Wasifikiri Tanzania ya sasa ni ile ya enzi za Mwalimu Nyerere ya CHAMA KIMOJA kwenye miaka ya 1960s. Huo jinga na upuuzi hauna nafasi kwa Tanzania na Dunia ya sasa.
Kila mtu anafahamu kwamba CCM na Kiwete wao wanataka kulazimisha mchakato uendelee kama wanavyotaka wao ILI WAENDELEE KUBAKIA MADARAKANI NA KUITAWALA TANZANIA MILELE KWA KUTUMIA KATIBA MBOVU ILIYOPO AMBAYO INAYOWALINDA.

Kiwete lazima akubali ili yaishe. Vinginevyo yeye na CCM yake watapambana na NGUVU YA UMMA WA WATANZANIA na siyo CDM.
 
kwa akili zenu mnadhani jk angekataa kukutana na cdm? Hana ubavu wa kukataa. Naona pia watu wanavumisha sana eti jk kafanya jambo la maana sana. Ukweli ni kuwa HANA JEURI YA KUKATAA KUKUTANA NA CDM! Cha msingi hapa tujaribu kufanya uchambuzi wa yale yatakayojadiliwa humo. Najua kabisa kwa jk kukubali kajiweka katika mtego mgumu sana ambao hakuwa na namna ya kuuepuka, na pengine alijua cdm watamtokea tu
 
They culd mek a deal via this special dialogie!Watazame watz wanataka nin,wakat gan na kwa namna gan wataka wafke wapi!Uzma we2 ni wa kitambo hivo wema na uungwana ni vitendo,KIFO CHAJA hakuna atakaeish milele dunian!
 
Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) wamedhamiria kumwona Rais Kikwete kwa ajili ya mjadala wa mswada wa marekebisho ya katiba hasa mchakato wake. Hii ikiwa na maana kwamba CHADEMA wanahitaji kuongea na Rais wa nchi kama kiongozi wa nchi. Cha kushangaza sana huyu Nape Nnauye jana akaongea na waandishi wa habari akasema hilo ombi na nia ya CHADEMA litajadiliwa na NEC ya CCM. Kwa nini hadi NEC ya CCM?? Kwani CHADEMA wanataka kumwona Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM au Rais wa nchi?
Kwa dhan hii ya Nape na CCM yake ndiyo maana tuna wasiwasi kuwa mchakato mzima wa mswada wa marekebisho ya katiba unasimamiwa na CCM kwa masirahi yao binafsi. Hakuna mantiki kwa NEK kujadili nia ya CHADEMA kukutana na Rais. Kwa maana nyingine inaonekana tayari CCM wameshaandaa majibu kwa Kikwete namna ya kuwajibu CHADEMA.
Ninawaomba CCM wasiingilie sana juhudi zinazofanywa na wananchi walio na uchungu na nchi hii katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.
 
Hakika usemi huu umetimia "mtoto akikunyea mkono hautakiwi kuukata na badala yake unausafisha na maji". Si kitu cha ajabu kuona mtoto wako uliyemzaa anajaribu kujitutumua huku akijua fika kuwa wewe ndiye Baba yake, CHADEMA ni kama mtoto aliyepotoka na Sasa ametambua ya kwamba alifanya makosa na sasa anarudi nyumbani ili kuanza maisha mapya. Kwa maana hii Baba hana sababu ya kukataa kumkaribisha nyumbani kwa kuwa si yule tena aliyepotoka bali ni mtoto mwingine.

Umuhimu wa Baba kukubali kumpokea mtoto wake aliyeshindikana unatokana na mambo mengi, Mtoto huweza kubadilika tabia kutokana na makundi yanayomzunguka na hivyo kujikuta akifanya vitu visivyotarajiwa na hususani kile kipindi cha "Barehe" au anapopevuka na hivyo kuanza kujiona yeye ndiye yeye au inawezekana alikwisha pevuka lakini kwa bahati mbaya mawazo ya maisha yake ni ya utegemezi toka kwa wengine na hivyo siku zote ataendelea kuwa na mawazo tegemezi, hii ni sawa na kusema "TUMEAMBIWA NA MBOWE TOTOKE NJE YA BUNGE " lakini mtoto hapati nafasi ya kujiuliza na hata kama akipata nafasi hana uwezo wa kujua la kutenda au kutafakari kwa kina, Kwa hatua hii mtoto anahitaji maombi pekee toka ndugu zetu wakristu au dua kwa ndugu zetu wa kiislamu.

Nimatumani yangu maombi kwa njia ya sala au dua limeanza kufanya kazi au kipindi cha "Barehe" cha kujifanya mjuaji kimepita na sasa mtoto ametambua makosa aliyoyafanya na sasa anasema "BABA NARUDI NYUMBANI".

HONGERA MWENYEKITI WA CCM TAIFA.
 
Mtu akishakuwa mwanachama wa CCM na akili inakosa mwelekeo! Nape akitoka ndani ya ccm ndiyo atajua kama CHADEMA walitaka kuongea na rais ama mwenyekiti wa ccm.
 
Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) wamedhamiria kumwona Rais Kikwete kwa ajili ya mjadala wa mswada wa marekebisho ya katiba hasa mchakato wake. Hii ikiwa na maana kwamba CHADEMA wanahitaji kuongea na Rais wa nchi kama kiongozi wa nchi. Cha kushangaza sana huyu Nape Nnauye jana akaongea na waandishi wa habari akasema hilo ombi na nia ya CHADEMA litajadiliwa na NEC ya CCM. Kwa nini hadi NEC ya CCM?? Kwani CHADEMA wanataka kumwona Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM au Rais wa nchi?
Kwa dhan hii ya Nape na CCM yake ndiyo maana tuna wasiwasi kuwa mchakato mzima wa mswada wa marekebisho ya katiba unasimamiwa na CCM kwa masirahi yao binafsi. Hakuna mantiki kwa NEK kujadili nia ya CHADEMA kukutana na Rais. Kwa maana nyingine inaonekana tayari CCM wameshaandaa majibu kwa Kikwete namna ya kuwajibu CHADEMA.
Ninawaomba CCM wasiingilie sana juhudi zinazofanywa na wananchi walio na uchungu na nchi hii katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Hivi kinakushinda nini kujuwa kama magwanda ni chama cha siasa kama ilivyo magamba? Hivi kinakushinda nini kuelewa kuwa magwanda wanakwenda kama magwanda na si kwa wadhifa wwote wa kiserikali? hivi kinakshinda nini kuelewa kuwa Kikwete ni Mwenyekiti wa magamba? Ikiwa kuomba kwa magwanda kwenda kumuona na Rais na Rais kukuali kunaongelewa hadi mitaani ni kwanini wenye Mwenyekiti wao wasiongee? Unanshangaza!
 
Ndio maana mimi naunga mkono dhana ya kutenganisha kofia mbili za uenyekiti wa chama na urais, ili iwe inajulikana wazi fulani yuko pale kama nani
 
Tunaomba na mapendekezo ya Bunge dhidi ya Jairo & Co yafanyiwe response ya haraka
kama hili.
 
Wewe hufahamu yafuatayo:-
1. CCM hawajali ustawi wa taifa hili kwa hiyo hata watanzania wasio na hatia wakifariki wakti wa kudai haki zao kwao ccm ni sawa tu! [tumeshayaona hayo Pemba, Mbeya, Arusha, Mwanza, Igunga, Geita, Nyamongo, e.t.c]
2. CHADEMA ni chama makini kinachoangalia madhara yatakayotona na uamuzi wao [hasa kwa wananchi na sio kwenye chama] kabla ya kufanya huo uamuzi tofauti na ccm wanaofanya uamuzi kisha kuangalia matokea kama yanamadhara kwao [ccm].
3. CCM wanaongozwa na hisia si uhalisia tofauti na wenzeo CDM wanaoangalia zaidi uhalisia [tumeshayaona haya wakti wa matokeo ya urais ambapo wangeweza kuitisha vyombo vya habari nakusema hatutambui matokeo ya urais ambapo watu wangeingia abarabarani, tumeyaona hayo kwenye kupinga muswada wa katiba, tumeyaona hayo Arusha, e.t.c].
TAMBUA KWAMBA KWA SASA AMANI YA NCHI HII INALINDWA NA CHADEMA SIO CCM KAMA UNAVYODHANI!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hakika usemi huu umetimia "mtoto akikunyea mkono hautakiwi kuukata na badala yake unausafisha na maji". Si kitu cha ajabu kuona mtoto wako uliyemzaa anajaribu kujitutumua huku akijua fika kuwa wewe ndiye Baba yake, CHADEMA ni kama mtoto aliyepotoka na Sasa ametambua ya kwamba alifanya makosa na sasa anarudi nyumbani ili kuanza maisha mapya. Kwa maana hii Baba hana sababu ya kukataa kumkaribisha nyumbani kwa kuwa si yule tena aliyepotoka bali ni mtoto mwingine.

Umuhimu wa Baba kukubali kumpokea mtoto wake aliyeshindikana unatokana na mambo mengi, Mtoto huweza kubadilika tabia kutokana na makundi yanayomzunguka na hivyo kujikuta akifanya vitu visivyotarajiwa na hususani kile kipindi cha "Barehe" au anapopevuka na hivyo kuanza kujiona yeye ndiye yeye au inawezekana alikwisha pevuka lakini kwa bahati mbaya mawazo ya maisha yake ni ya utegemezi toka kwa wengine na hivyo siku zote ataendelea kuwa na mawazo tegemezi, hii ni sawa na kusema "TUMEAMBIWA NA MBOWE TOTOKE NJE YA BUNGE " lakini mtoto hapati nafasi ya kujiuliza na hata kama akipata nafasi hana uwezo wa kujua la kutenda au kutafakari kwa kina, Kwa hatua hii mtoto anahitaji maombi pekee toka ndugu zetu wakristu au dua kwa ndugu zetu wa kiislamu.

Nimatumani yangu maombi kwa njia ya sala au dua limeanza kufanya kazi au kipindi cha "Barehe" cha kujifanya mjuaji kimepita na sasa mtoto ametambua makosa aliyoyafanya na sasa anasema "BABA NARUDI NYUMBANI".

HONGERA MWENYEKITI WA CCM TAIFA.
 
Uelewe wa Watanzania ni mdogo sana kwa sababu ya NDIO MZEE mentality. Akisema mkubwa hata ameongea pumba, alichoongea kinaonekana cha maana na anapewa credit.

Nimeshangaa watu wakimsifu JK eti kwa sababu amekubali kuongea na CHADEMA. Je, ni wazo lake ili apewe credit? Kwanza kitendo cha yeye kukaa kimya mpaka pale viongozi wa CHADEMA kuhitaji kuongea naye ni kuonyesha uwezo wake mdogo wa kuongoza.
 
wana njaa tu, wanajipeleka kwa kikwete namna hiyo, kweli viongozi wa siasa cdm hamna, MH kikwete wape chai, na bahasha hao, ni njaa ndio inayowasumbua.
 
kwanini waliamua kutoka bungeni, mapendekezo yao wangewasilisha bungeni.

CHADEMA walifanya vema kutoka bungeni ili kukataa propaganda za kichama zilizokuwepo ndani ya bunge. Fuatilia walichosema wabunge wote wa CCM bungeni kuhusiana na mswada huo - hakuna hata mmoja aliyeonesha busara ya kuujadili mswada na mapendekezo ya CHADEMA, wanaharakati na majaji wastaafu badala yake waligeuza bunge kuwa kijiwe cha kuwakejeli CHADEMA, wanaharakati na majaji wastaafu. CHADEMA waliona kuwa ndani ya bunge hakuna hata mbunge mmoja wa CCM aliyetaka kuonesha busara, kujadiliana nao ilikuwa ni kupoteza muda. Na sasa wanaenda kumwona Rais wakiamini kuwa Rais atakuwa na busara kuliko wabunge wa chama chake. Alionesha busara hiyo katika uamuzi wa ama kuwa na katiba mpya au la. Wapambe wa CCM walisema hakuna sababu ya kuwa na katiba mpya, JK akasema itaandikwa katiba mpya, mara wanaCCM unafiki na fuata upepo wakaitikia kibwagizo kwa nguvu, tutaandika katiba mpya. Inategemewa JK ataridhia ushauri wa CHADEMA, majaji wastaafu na wanaharakati, na baada ya hapo wanaCCM unafiki na fuata upepo lazima wataitikia kibwagizo kwa nguvu ya ajabu.
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.
From politeness
 
Ulianza pointi yako vizuri sana (kwamba JK ni raisi wa wote), sema unachanganya topic kutokana na ukereketwa.
Kimsingi nampongeza JK kutokana na kukubali kukutana na Chadema, kwa sababu katiba itakayorekebishwa inatuhusu wote, kama vile ambavyo JK ni raisi wa wote, hata ambao hawakumpigia kura. Kafanya suala la msingi sana kukaa meza moja na Chadema kusikiliza hoja zao. Cha muhimu tu, katika kikao hicho raisi awe kama mkuu wa sirikali, na si kama mwenyekiti wa chama, otherwise hakuna kitakachotokea cha kutusaidia kusonga mbele
 
Back
Top Bottom