Kwanini CHADEMA hawafanyi Mikutano ya hadhara kama ilivyokuwa awamu ya Mzee Kikwete?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,992
142,008
Wakati wa Awamu ya 4 Rais akiwa Kikwete CHADEMA walikuwa Wanafanya sana mikutano ya hadhara tena bila chopa na walipata nyomi.

Lakini awamu pamoja na kuruhusiwa na Rais Samia bado hawafanyi Mikutano kabisa!

Tatizo nini?
 
Posho kutoka kwa mabwana zao wa ulaya imekata, mabeberu wameona wafadhili BongoFlavourHonour ya Sugu pale Alaaaa Flanseee, chini ya ubalozi wa ufaransa.

Kutumika kuna mwisho
 
watu awaji kwenye mikutano wanapambania maisha.
hali ya maisha ya utawala huu kwa raia ni mbaya ukilinganisha na wakati wa Jakaya.

wakati wa Jakaya ukiwaita watu wanakuja kama wote kwenye mikutano tofauti na sasa.
 
Wakati wa Awamu ya 4 Rais akiwa Kikwete CHADEMA walikuwa Wanafanya sana mikutano ya hadhara tena bila chopa na walipata nyomi.

Lakini awamu pamoja na kuruhusiwa na Rais Samia bado hawafanyi Mikutano kabisa!

Tatizo nini?
CCM na wabunge wenu wa mchongo wanaifanya hiyo mikutano? Mkikosa cha kuongea kazi yenu ni kuokoteleza vihoja. Tanzania ina chama kimoja tu cha upinzani? Kwanini musiviseme vyama vingine vya kina Zitto, Lipumba nk au Chadema pekee ndiyo inayowanyima usingizi?

Mbowe na Lissu kama mnasikia kazieni hapohapo mmewakamata pabaya.

Tozo, mikataba ya hovyo ya Bandari, kuuzwa kwa mbuga za wanyama, uonevu kwa Wamasai, kupanda kwa gharama za maisha, mfumuko wa bei, hali mbaya ya uchumi, rushwa, wizi nk vyote hivi mnasubiri Chadema iwasemee. Wabunge wenu kazi yao ni hipi?

Tulidanganywa nchi ikipata madiwani na wabunge wa chama kimoja maendeleo yatakuja kwa siku mmoja sababu wapinzani wanawachelewesha, haya sasa ogeleeni kwenye hayo maandeleo. Msiwe wepesi wa kurubuniwa na watawala, wanatumia ujinga wenu kwa manufaa yao.
 
Back
Top Bottom