Kikwete akubali kukutana na CHADEMA

theophilius

Senior Member
Nov 19, 2010
150
54

kulingana na taarifa ya ITV JK amekubali kukutana na chadema. Je atafanya busara kusikiliza na kuelewa watakayomweleza?

=============
UPDATE
=============

Ikulu imetoa taarifa kwa Umma kuthibitisha nia ya Rais kukutana na ujumbe wa CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuomba viongozi wa chama hicho kukutana na Mheshimiwa Rais kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mheshimiwa Rais Kikwete amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu ni jambo jema.

Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Mheshimiwa Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutanana viongozi hao wa CHADEMA na kuzungumzia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 22, 2011
DODOMA
Fungua attachment usome zaidi
 
Attachments

  • ombiChadema.doc
    64.5 KB · Views: 342
Last edited by a moderator:
Haya ndio mambo yanayoniudhi..... Akutane nao kwa nini?
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.
 
Ameonyesha kuwa yeye ni baba mzuri..ngoja awasikilize wanawe na kuwapa ushauri na kuwafunza siasa za TZ!
 
CDM, pangilieni point vyema, na aeleweshwe just from a horse's Mouth!...Aachane na kuzungumza kwa kuwekewa maneno mdomoni!
 
Jk inaonekana kila akilala anaiota chadema maana siku hizi ktk hotuba zake lazma awataje chadema.
Anyway, asije akaleta ulaghai kama walivyowaletea CUF.
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.

cha msingi ni kuyapa uzito, watakayozungumza ikiwa ni pamoja na kuridhia kutousain mswada, kwani kuna shida gani ikiwa yeye na wenzake walioupitisha wanadhani unaakisi mawazo ya watanzania, si waupeleke kwa wananchi wasikie maoni yao ni yepi!
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.

vp budget ya Posho yenu, kuna posho review imepita, kama bado komaeni na Nape kaz mnayofanya ni nzuri... Bt kuweni 2ta iyundia 2me mkifanya mchezo... Nyinyi jisauni 2...
 
Nina subiri niione MIBUNGE ya CUF na vidume vyao CCM itakavyokuwa na AIBU mara mambo yakibadilika. Uzuri wa Rage yeye hana aibu.

Ahh, nasikia kuwa Egypt wale Wanajeshi na wao wameufyata na sasa watapisha katiba mpya na serikali ya Uraia.

Taratibu tu somo litaeleweka. Hata Lady FF atakuja kumsifu Nyerere siku moja.
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.
You talk too much, many issues at one time the bad thing is most of them are speculations.
 
This is a good news! I real like it. Sasa nasubiri akububali pia na mapendekezo watakayompelekea.

God forbid, akikataa tu, kaisha!?
 
Back
Top Bottom