makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.
Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.
Unaweza kuwa Rais wa wote kwa kutumia mabavu,udikteta na ubabe kama anavyofanya Rais Kiwete!
Ni lazima Kiwete akubali kukutana na CHADEMA maana wana mambo ya msingi wanayoyasimamia na yanakubalika kwa Watanzania walio wengi. Lazima ajue kuwa HATUKO KUUNDA KATIBA YA CCM BAALI YA WATANZANIA WOTE. Nafikiri Kiwete sasa ameanza kuona kuwa MAJI YANAANZA KUZIDI UNGA na lazima akae meza moja na upinzani ili asikie NGUVU ZA HOJA ZA CHADEMA na si HOJA ZA NGUVU za wabunge wa CCM wanaotaka kuwaburuza Watz.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana unaonyesha kuwa Kiwete alipata kura 5.2m kati ya Watanzania takribani milioni 45. Sasa wasemaje ni Rais wa wote?Ndani ya CCM yenyewe Kiwete kwa sasa hatakiwi halafu wewe unadanganya watu kuwa ni Rais wa wote,acha hizo mama.
Kiwete wako anatakiwa akubaliane na CHADEMA vile wanavyoona inafaa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Si CHADEMA tu baali hata makundi mengi ya wanaharakati na Watanzania wasio na vyama hawajakubaliana na namna Bunge la CCM linavyotaka KUWABURUZA Watanzania kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
Kiwete na CCM yake lazima wasome alama za nyakati. Wasifikiri Tanzania ya sasa ni ile ya enzi za Mwalimu Nyerere ya CHAMA KIMOJA kwenye miaka ya 1960s. Huo jinga na upuuzi hauna nafasi kwa Tanzania na Dunia ya sasa.
Kila mtu anafahamu kwamba CCM na Kiwete wao wanataka kulazimisha mchakato uendelee kama wanavyotaka wao ILI WAENDELEE KUBAKIA MADARAKANI NA KUITAWALA TANZANIA MILELE KWA KUTUMIA KATIBA MBOVU ILIYOPO AMBAYO INAYOWALINDA.
Kiwete lazima akubali ili yaishe. Vinginevyo yeye na CCM yake watapambana na NGUVU YA UMMA WA WATANZANIA na siyo CDM.