Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

JK atataka, atawaza, atajaamua .............mpaka 2015 ataondoka kama rais aliyewaacha wanainchi njia panda zaidi

toka lin JK amefanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa??Kaanza kumsifia Warema

Raisi Kilwete ni Mtu Makini sana, hakurupuki wala haendeshwi kwa majungu na umbeya, ktk kipindi chake tumedhuhudia amewawajibisha mawaziri wengi. Na wengine wameshitakiwa wapo mahakamni, mambo haya hatujawahi kuyashuhudia kipindi chochote.
 
JK analimaliza hili suala la Escrow kwa staili ya aina yake. Kila mtanzania ataridhika kwa maamuzi yake ya busara atakayoyatoa STAY TUNED!!

Maamuzi magumu ni yale ya kuamua kuchia ngazi ya URAIS basi.Mengineyo ameyafanya mwenyewe yawe magumu sababu amekubali kuwa Mwizi na kuungana na wezi kuliibia Taifa analoliongoza,na ndiyo maana ameona uamuzi ni MGUMU maana wenzake wameshika MPINI yeye kashika MAKALI.:msela::msela::cheer2::cheer2:
 
JK:Akatiza ziara ya Mizengo Pinda



Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.

chanzo:JK:Akatiza ziara ya Mizengo Pinda - BBC Swahili
Nani analipa hizi gharama jamani? yaani ameitwa! Halafu atarudi kuendelea na ziara yake!:confused2:
 
I will always support Professor Muhongo to get hold on the current post.He has done a lot!
 
Kinachokera kila mtu mwenye akili timamu; (wewe jipime; sikuhukumu!) kuhusu swala hilo sio uteuzi; bali hatua ya Jk; tena Dr/Profesa mzima kabisa!! kumsifia mtu anayejiuzulu kutokana na tuhuma za wizi wa mali ya umma?!!; mtu anatuhumiwa kwa wizi kisha Rais anasema "mwaminifu na mwadilifu??!!"; na Rais amekubali ajiuzulu meaning kuna jambo lenye mashiko hapo! kweli Rais anajua maana ya maneno hayo au ni akili za mbayuwayu??!
Naona haya sana kujitambulisha kokote kama natokea nchi yenye ubadhirifu kiasi hiki unaolindwa na kutetewa na mkuu wa nchi!!, Eheee Mungu tuokoee na majanga haya ya CCM!; Eheee Mungu sikiliza kilio cha wanao hawa watanzania!!!

Athali za prostate cancer ni pamoja na ubongo kujua maji.
 
Raisi Kilwete ni Mtu Makini sana, hakurupuki wala haendeshwi kwa majungu na umbeya, ktk kipindi chake tumedhuhudia amewawajibisha mawaziri wengi. Na wengine wameshitakiwa wapo mahakamni, mambo haya hatujawahi kuyashuhudia kipindi chochote.

Ni kweli ni mtu makini kwa upeo wako wa kufikiria mkuu
 
Kama kura za katiba pendekezwa zilipigwa kwa E-mails, skype, fax kwa nini arudi alaf Jmosi aendelee na ziara! huu ni ufisadi wa kodi ya watanzania

Kwani hadi aitwe ina maana aliondoka bila kumuaga mkuu wake?au wakati huo mkuu alikuwa hana jambo lolote?maake hizi ni gharama za walipa kodi halafu akisikiliza arudi tena wakati huu angeweza kuongea kwa simu na yakaisha,kwanza gharama za ndege inabidi walipe faini kwa kuwa hawakuwemo katika utaratibu wa kurudi kabla ya muda waliotarajia warudi.Au ndio matokeo ambayo hayakutarajiwa ya serikali za mitaa yameongeza presha.
 
hivi pinda ana impact gani katika maamuzi ya hii nchi ?
 
Hadi sasa matokeo yaliyokusanywa ni kutoka katika vijiji 9,047 na mitaa 3,078.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kimeongoza uchaguzi huo kwa kujinyakulia vijiji 7,290 sawa na 80.58% na mitaa 2,116 sawa na asilimia 68.7% huku chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikijinyakulia vijiji 1,248 sawa na 13.8% na mitaa 753 sawa na 24.5%.
Ikumbukwe ushindi wa 80.58% wa CCM ni pamoja na wagombea waliopita bila ya kupingwa kutokana na mapingamizi au Upinzani kushindwa kusimamisha wagombea ambao ni 33%. Hivyo kwa maeneo ambayo uchaguzi umefanyika utaona jinsi ushindani ulivyokuwa mkubwa. CCM wameshinda kwa 47% tu.
Chama cha Wananchi CUF kimeibuka nafasi ya Tatu kwa kujinyakulia vijiji 382 na mitaa 235 wakati NCCR Mageuzi kikipata mitaa 8, ACT mitaa 9, TLP mtaa 1 na vijiji 2, UDP Vijiji 4 na NLD vijiji 2.
Kata 120 zinatarajiwa kufanya Uchaguzi wiki hii.

Hiki ndio wapinzani wanatakiwa wawaonyeshe wananchi ili wajue ushindani ulikuwaje na ccm wanaposema asilimia 80 wanamaanisha nini. Uzuri wa data yakinifu ndio huu unataja idadi ya mitaa ccm waliyoshinda kwa kura, na waliyoshinda kwa magumashi. Ukijaribu kuangalia ccm hawataki kabisa ufafanuzi wa aina hii maana wanapata homa ya matumbo ndio maana unaona wanakimbilia kwenye asilimia bila kunyumbulisha ukweli huu. Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja ...
 
I will always support Professor Muhongo to get hold on the current post.He has done a lot!

Hapana ndugu yangu, taarifa za ukweli toka ameingia wizarani mwaka wa kwanza ameiingiza tanesco hasara mara 3 ya aliyoikuta, mpaka mwaka huu ameshaingizia tanesco hasara mara 4 zaidi ya mwaka jana. Pitia taarifa ya CAG
 
JK anataka kufanya maamuzi magumu sana kwa maslahi ya Taifa.

Uamuzi mgumu ambao nitaupongeza na kuukubali ni wa yeye KIKWETE kuamua kuachia ngazi kwa kutamka hadharani kuwa nchi imemshinda kuongoza tofauti na hivyo hana uwezo wa kutoa maamuzi yeyote magumu
 
JK analimaliza hili suala la Escrow kwa staili ya aina yake. Kila mtanzania ataridhika kwa maamuzi yake ya busara atakayoyatoa STAY TUNED!!
Bila kumtosa Pinda atakuwa hajafanya lolote hata kabla ya kumaliza mda wake atateua baraza jingine la mawaziri, kiranja wao ni ovyo kabisa.
 
Hiki ndio wapinzani wanatakiwa wawaonyeshe wananchi ili wajue ushindani ulikuwaje na ccm wanaposema asilimia 80 wanamaanisha nini. Uzuri wa data yakinifu ndio huu unataja idadi ya mitaa ccm waliyoshinda kwa kura, na waliyoshinda kwa magumashi. Ukijaribu kuangalia ccm hawataki kabisa ufafanuzi wa aina hii maana wanapata homa ya matumbo ndio maana unaona wanakimbilia kwenye asilimia bila kunyumbulisha ukweli huu. Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja ...

Sasa hivi CCM iko ICU haina uwezo wa kuchanganua wao kila kitu ni propoganda.
 
Isije kuwa wanakuja kutengua uwaziri mkuu??? Maana c kawaida kurudishwa hm anaweza kuagana na uwaziri mkuu bila kutarajia
 
Back
Top Bottom