Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Hivi JK hakujua kuwa Pinda ana ziara hadi anaisitisha au siku hizi kila mtu anamficha mwenzake anachowaza.
 
kiwanda chetu cha kupika uongo kinaendelea vizuri sana na kazi yake
 
KWA UFUPI
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Dubai. U.A.E. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.

Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.

Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.

Chadema yakerwa JK kumsifia Werema

Jana, Chadema kilielezea kusikitishwa kwake na sifa alizotoa Rais Kikwete kwa Jaji Werema kuwa ni mwaminifu na mwadilifu wakati amejiuzulu kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema kitendo cha Rais kumsifu Jaji Werema kinawakatisha tamaa Watanzania.

"Hakupaswa kupongezwa badala yake Rais angemwambia kwamba alikuwa kwenye taratibu za kumfukuza kazi," alisema Mnyika na kuongeza kuwa hata watuhumiwa wengine katika kashfa hiyo wanaposikia Rais akimpongeza mwenzao wanaona makosa yao ni jambo la kawaida linaloweza kupongezwa.

"Hata vyombo vya dola vitaogopa kumshtaki Werema kwa sababu amepongezwa na Rais kwamba ni mtumishi ambaye alikuwa mwaminifu na mwadilifu," alisema Mnyika.

Alisema Watanzania wanasubiri Rais kuwafukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katibu mkuu wake, Eliakimu Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na bodi nzima ya Tanesco.

"Baada ya kufukuzwa wanatakiwa kushtakiwa," alisema Mnyika.

Chanzo:Mwananchi


hii habari ni kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya wajinga
 
Hapa ndo jk atajijengea jina au kujiua kabisa katika mioyo ya watanzania
 
CHADEMA wanakwerwa na JK kumsifia Werema kwani walimteua wao?


Kinachokera kila mtu mwenye akili timamu; (wewe jipime; sikuhukumu!) kuhusu swala hilo sio uteuzi; bali hatua ya Jk; tena Dr/Profesa mzima kabisa!! kumsifia mtu anayejiuzulu kutokana na tuhuma za wizi wa mali ya umma?!!; mtu anatuhumiwa kwa wizi kisha Rais anasema "mwaminifu na mwadilifu??!!"; na Rais amekubali ajiuzulu meaning kuna jambo lenye mashiko hapo! kweli Rais anajua maana ya maneno hayo au ni akili za mbayuwayu??!
Naona haya sana kujitambulisha kokote kama natokea nchi yenye ubadhirifu kiasi hiki unaolindwa na kutetewa na mkuu wa nchi!!, Eheee Mungu tuokoee na majanga haya ya CCM!; Eheee Mungu sikiliza kilio cha wanao hawa watanzania!!!
 
CHADEMA wanakwerwa na JK kumsifia Werema kwani walimteua wao?

Ivi umeshapiga mswaki? unafkiria JK alitoka na suruali zake tu pamoja na mashati yake ya mitumba kuja kuiongoza Tanzania? Kwa nini Chadema wasiseme na watanzania wengine, JK hakuekwa pale ni ukoo wake ni Watanzania ndio waliompa mamlaka sasa kwanini asihojiwe? Tunacholalamika Warema ni mwizi sasa ni uaminifu upi huo ambao rais amempongeza.
 
Back
Top Bottom