Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Kama kulikuwa na jambo kama hilo, Waziri Mkuu alisafarije nje ya nchi? Rais anafanya kazi kwa ad hocs hakuna ratiba ya kazi?

Hatujui undani wake,lolote laweza kutokea.Labda ni kupanga safu mpya ya mawaziri.Bado Raisi atahutubia Taifa siku ya ijumaa na hatujui nini anataka kulieleza taifa.
 
KWA UFUPI
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Dubai. U.A.E. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.

Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.

Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.

Chadema yakerwa JK kumsifia Werema

Jana, Chadema kilielezea kusikitishwa kwake na sifa alizotoa Rais Kikwete kwa Jaji Werema kuwa ni mwaminifu na mwadilifu wakati amejiuzulu kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema kitendo cha Rais kumsifu Jaji Werema kinawakatisha tamaa Watanzania.

“Hakupaswa kupongezwa badala yake Rais angemwambia kwamba alikuwa kwenye taratibu za kumfukuza kazi,” alisema Mnyika na kuongeza kuwa hata watuhumiwa wengine katika kashfa hiyo wanaposikia Rais akimpongeza mwenzao wanaona makosa yao ni jambo la kawaida linaloweza kupongezwa.

“Hata vyombo vya dola vitaogopa kumshtaki Werema kwa sababu amepongezwa na Rais kwamba ni mtumishi ambaye alikuwa mwaminifu na mwadilifu,” alisema Mnyika.

Alisema Watanzania wanasubiri Rais kuwafukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katibu mkuu wake, Eliakimu Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na bodi nzima ya Tanesco.

“Baada ya kufukuzwa wanatakiwa kushtakiwa,” alisema Mnyika.

Chanzo: Mwananchi

siku zote kijwete huwa anauma na kuouliza kwani hamumjui?
 
Mojawapo ya maamuzi magumu aliyofanya JK ni pamoja na kumsifia Mh aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya kulitia hasara taifa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
CHADEMA wanakwerwa na JK kumsifia Werema kwani walimteua wao?

We Mhudumu wa baa uwe hata na akili za kurudisha change kwa wateja eboo,
Ukumbuke kuwa Rais yuko pale kwa niaba ya watanzania.

Rais alimteua Werema kwa niaba ya watanzania si kwa niaba ya familia yake.

Mnyika ni mmoja wa watanzania wanaowakiliswa na JK hivyo ana haki ya kusema kama hakuridhishwa na jambo hilo kwa sababu JK yuko kwa niaba ya watanzania.

Ndio maana leo anatakiwa kuwaadhibu wezi kwa sababu wamewaibia watanzania!
 
Last edited by a moderator:
Hatujui undani wake,lolote laweza kutokea.Labda ni kupanga safu mpya ya mawaziri.Bado Raisi atahutubia Taifa siku ya ijumaa na hatujui nini anataka kulieleza taifa.

Suala la Escrow inajulikana kwa kipindi sasa haitakuwa 'impromptu' kiasi hicho.
 
Hatujui undani wake,lolote laweza kutokea.Labda ni kupanga safu mpya ya mawaziri.Bado Raisi atahutubia Taifa siku ya ijumaa na hatujui nini anataka kulieleza taifa.

Wewe unategemea kusikia lolote la maana??
 
Tatizo ni kwamba huyu ndugu yetu hadi apewe kashikashi ndio hufanya maamuzi magumu...

Mkuu maamuzi ya kuwawajibisha wezi wa Mali ya umma ni magumu kwa Rais wa Nchi?
Labda kama na huyo Rais ni mshirika wao kwenye huo wizi.
Haya mambo ni ya kipuuzi sana.
 
Hadi sasa matokeo yaliyokusanywa ni kutoka katika vijiji 9,047 na mitaa 3,078.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kimeongoza uchaguzi huo kwa kujinyakulia vijiji 7,290 sawa na 80.58% na mitaa 2,116 sawa na asilimia 68.7% huku chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikijinyakulia vijiji 1,248 sawa na 13.8% na mitaa 753 sawa na 24.5%.
Ikumbukwe ushindi wa 80.58% wa CCM ni pamoja na wagombea waliopita bila ya kupingwa kutokana na mapingamizi au Upinzani kushindwa kusimamisha wagombea ambao ni 33%. Hivyo kwa maeneo ambayo uchaguzi umefanyika utaona jinsi ushindani ulivyokuwa mkubwa. CCM wameshinda kwa 47% tu.
Chama cha Wananchi CUF kimeibuka nafasi ya Tatu kwa kujinyakulia vijiji 382 na mitaa 235 wakati NCCR Mageuzi kikipata mitaa 8, ACT mitaa 9, TLP mtaa 1 na vijiji 2, UDP Vijiji 4 na NLD vijiji 2.
Kata 120 zinatarajiwa kufanya Uchaguzi wiki hii.
 
CHADEMA wanakwerwa na JK kumsifia Werema kwani walimteua wao?

Siyo Chadema tu bali Mtanzania ye yote mwenye mapenzi mema na hii nchi lazima akerwe na hili la Jk kumsifia Werema. Tangu lini mkosaji akasifiwa??!!
 
IKULU haina encrypted lines ? Upuuuuuziiiiiiiiiiiiiii.....
Hichi nacho kichekesho kingine.. kwamba anarudi halafu jumamosi aende kuendelea na ziara! Matumizi mabaya ya kodi za watanzania haya.. Ni nini hicho anachoitiwa ambacho kimeshindikana kujadiliana kwa skype, email, au simu?
 
Vyanzo vya ndani ya ofisi ya pm vya siri vimeelezea wasiwasi wa ziara ya pm uarabuni ambayo siyo kawaida. Vyanzo hivyo vimedai ziara hiyo ni harakati za kutafuta pesa za kuwezesha kampeni na harakati zake za kugombea uraisi. Ikumbukwe kwamba Raila Odinga wakati agombea urais nchini kenya aliripotiwa kuzuru mataifa ya uarabuni na habari zilienea nchinie humo kuwa amesaini mikataba kadhaa na kupewa fedha za kampeni ambayo Kenyatta alidai ni kuuza nchi. Pia tukumbuke kuwa eneo la loliondol liliuzwa kwa kampuni ya OBC ya familia ya kifalme ya falme za kiarabu chini ya utawala wa mwinyi. Ndani ya eneo hilo ambalo linamgogoro na wafugaji baada ya serikali kusaini mkataba wa kuwaongezea makazi ya wafugaji kumekuwa na hali ya sintafahamu huku Nyalandu akisuluisha kisanii ili kupata kura za serikali za mitaa. Mwaka 2005 nilibahatika binafsi kuzuri eneo hilo na nilishutushwa na maandishi yaliyokuwa mbele kabisa yakisomeka "Karibu falme za Kiarabu".

Pia eneo hilo linauwanja wa ndege na jeshi linalovaa nguo za rangi za majeshi ya uarabuni na mamia ya wafanyakazi wa kiarabu wakiwemo asikari viongozi. Pia kumekuwepo malalamiko ya ukiukwaji wa haki za kbinadamu kwa wananchi wa eneo hillo.
 
[h=1]JK:Akatiza ziara ya Mizengo Pinda
[/h]
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.

chanzo:JK:Akatiza ziara ya Mizengo Pinda - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom