Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Kikwete akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,782
Reaction score
5,172
KWA UFUPI
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Dubai. U.A.E. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.

Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.

Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.

Chadema yakerwa JK kumsifia Werema

Jana, Chadema kilielezea kusikitishwa kwake na sifa alizotoa Rais Kikwete kwa Jaji Werema kuwa ni mwaminifu na mwadilifu wakati amejiuzulu kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema kitendo cha Rais kumsifu Jaji Werema kinawakatisha tamaa Watanzania.

"Hakupaswa kupongezwa badala yake Rais angemwambia kwamba alikuwa kwenye taratibu za kumfukuza kazi," alisema Mnyika na kuongeza kuwa hata watuhumiwa wengine katika kashfa hiyo wanaposikia Rais akimpongeza mwenzao wanaona makosa yao ni jambo la kawaida linaloweza kupongezwa.

"Hata vyombo vya dola vitaogopa kumshtaki Werema kwa sababu amepongezwa na Rais kwamba ni mtumishi ambaye alikuwa mwaminifu na mwadilifu," alisema Mnyika.

Alisema Watanzania wanasubiri Rais kuwafukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katibu mkuu wake, Eliakimu Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na bodi nzima ya Tanesco.

"Baada ya kufukuzwa wanatakiwa kushtakiwa," alisema Mnyika.

Chanzo: Mwananchi

 
JK anataka kufanya maamuzi magumu sana kwa maslahi ya Taifa.
 
Hichi nacho kichekesho kingine.. kwamba anarudi halafu jumamosi aende kuendelea na ziara! Matumizi mabaya ya kodi za watanzania haya.. Ni nini hicho anachoitiwa ambacho kimeshindikana kujadiliana kwa skype, email, au simu?
 
CHADEMA wanakwerwa na JK kumsifia Werema kwani walimteua wao?
 
Chanzo cha taarifa kuwa PM ameitwa arudi home? au ndo yale yale, full uzishi?
 
JK analimaliza hili suala la Escrow kwa staili ya aina yake. Kila mtanzania ataridhika kwa maamuzi yake ya busara atakayoyatoa STAY TUNED!!
 
JK anataka kufanya maamuzi magumu sana kwa maslahi ya Taifa.

inampasa kufanya maamuzi sahihi sana wakati huu kwasababu NDIO FURSA YAKE YA MWISHO kuandika historia yake kama Raisi katika Taifa hili.

Hata ikibidi kumrudisha Lowasa kama waziri mkuu afanye hivyo
 
Something terrible is coming........Leo najua mawasiri mizigo kama wale wakina Membe lazima wapige dili za mwisho mwisho, na zile fedha za Gadhafi lazima akazifufue manake anajua arudi katika hiyo nasafi
 
Back
Top Bottom