Kikwete akabidhiwa magari 50 ya wagonjwa

Kikwete akabidhiwa magari 50 ya wagonjwa

Ni kweli kwa kushusha uchumi kutokea budget ya dola bilion 10 mwaka 2005 mpaka dola bilioni 9 mwaka 2015.
Hongereni sana wana CCM, tuambieni reserve BOT iko kiasi gani???

Wanapenda namba ila hawajui hesabu. Prof. Jay alisema hiki "unapiga hatua tisa mbele na kurudi nyuma hatua hatua kumi kisha unajipongeza" wacha yatakwisha na ujinga wa watanzania.
 
Umecheka nini sasa eleza wewe umeelewaje hapo?

kama utaona kicheko changu ni kama sijui....nafikiri kicheko changu kimeambatana na mtazamo wa maswali yangu....kukumbuka kwa makubwa yapi?? ndio maana nimesema fafanua..unaweza kumsaidia
 
Hivi kupewa msaada wa dola laki 3 na mtu ambaye hakusanyi kodi bali analipa tunaona ni fahari. Sisi kodi zetu tunazokusanya tuna peleka wapi kama hata dola laki 3 tusaidiwe?
 
Gharama ya kununua magari hayo yote haifiki hata billion moja a.k.a vijisent vya chenge au hela ya mboga ya Tibaijuka. Badala ya kudhibiti ufisadi wa mamia ya mabillion anakwenda kuombaomba. Hii ni aibu kwa taifa uwezo tunao, pesa zipo,rasilimali zipo kwann tunaaibika hivi? Cha kushangaza zaidi anaona sifa kuombaomba. "There is no free lunch in london."
 
Wanapenda namba ila hawajui hesabu. Prof. Jay alisema hiki "unapiga hatua tisa mbele na kurudi nyuma hatua hatua kumi kisha unajipongeza" wacha yatakwisha na ujinga wa watanzania.

maneno ya ngebe kama haya ndo hunifanyia nitamani ukawa wachukue madaraka ili nije nione jamaa kama wewe mtakuwa na lipi la kusema itakopopita miaka mitatu ama minne halafu hakuna jipya watakua wamefanya zaidi zaidi ya kutunisha vitambi vyao.
 
Nafikiri kuna uzi humu ndani unaosema kuwa magamba yanapenda hesabu lakini hayajui.

Safari ya wiki moja ulaya ina cost zaidi ya hiyo hela lakini magamba walivyo hamnazo mnapiga makofi tu. Hivi mtaacha lini uzuzu wenu?
 
Hela za kununua L/Cruiser GX V8 171 zipo ila za kununua GARI za wagonjwa hakuna!!!
 
maneno ya ngebe kama haya ndo hunifanyia nitamani ukawa wachukue madaraka ili nije nione jamaa kama wewe mtakuwa na lipi la kusema itakopopita miaka mitatu ama minne halafu hakuna jipya watakua wamefanya zaidi zaidi ya kutunisha vitambi vyao.

Lazima tusafishe uchafu wenu mliocha kwanza. Kama unajua hesabu, lazima tutoke kwenye negative, tufike zero halafu tuanze safari ya positive. I hope umeelewa.
 
Ivi kuna cha bure dunia hii nayoishi mimi au kuna dunia nyingine ??

Nimejikuta nawaza hvyo tu.
 
Labda ni ambulance 5 na siyo 50? Umefikiria hilo pia.

Ambulance hamsini itakuwa wamekosea figure ni million 3.

Hata uki google bei za ambulance used ni zaidi ya hiyo.

Wewe tazama tu wajuu lakini kumbuka, hata pua na macho yako yanakusuta, yanaanganilia juu? Fikiri.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kwani atazipaki nyumbani kwake jk? Au zitatumika hospitalini?

shida sio kupaki kwake au vinginevo, najalibukujiuliza sisi kama nch tunashindwa kununua kwa fedha yetu??

mbona mawashawasha ya polisi yananunuliwa bila mabakuli??
 
Decent Dia Jewel (DMCC, hivi kuna mtu hata kwa ku'google' tu amekutana na kampuni yenye jina hilo? Hata vichochoroni Mumbai kampuni hiyo haijulikani. Je ikulu ya Tanzania imeijuaje hii kampuni? Mpaka inatoa msaada kimataifa lazima tu ingejulikana huko India katika biashara ya vito (jewelry) lakini ndio hivyo tena haijulikani. Yale yale ya Richmond Development Company...sijui safari hii sisi tumewakabidhi nini!

Pamoja na hayo ambulensi 50 kwa dola 300,000 ni sawa na kila moja kwa dola 6,000! Ni magari au pikipiki? Nakumbuka tuliwahi kuletewa za mwanzo.
 
Back
Top Bottom