Waziri wa Fedha: Magari yaliyotumika yanayoingizwa Nchini kutozwa Ushuru wa 50%

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,879
Reaction score
16,311
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni Juni 11, 2026, ametangaza kupandishwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, huku kigezo cha umri wa gari kikichukua nafasi kubwa.

Katika mabadiliko hayo, magari yenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 10 yamepandishwa ushuru kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 20. Kwa upande wa magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 lakini hayazidi miaka 20, ushuru wake umepandishwa kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40.

Kasi hiyo ya ongezeko imegusa pia magari chakavu zaidi, ambapo Mhe. Balozi Khamis amebainisha kuwa magari yenye umri unaozidi miaka 20 na kuendelea sasa yatatozwa ushuru mkubwa wa bidhaa wa kiwango cha asilimia 50.

Akitolea ufafanuzi lengo la hatua hiyo, Waziri wa Fedha ameeleza kuwa mbali na kuongeza mapato ya serikali, mkakati huo unalenga kupunguza uingizaji wa magari hayo mabavu ambayo yamekuwa yakisababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kupitia uzalishaji wa taka ngumu, ambazo zimekuwa zikitumia gharama kubwa kuziteketeza.

Balozi Khamis amelihakikishia Bunge kuwa hatua hizo mpya za ushuru wa bidhaa kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 355.09.

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni Juni 11, 2026, ametangaza kupandishwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, huku kigezo cha umri wa gari kikichukua nafasi kubwa.

Katika mabadiliko hayo, magari yenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 10 yamepandishwa ushuru kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 20. Kwa upande wa magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 lakini hayazidi miaka 20, ushuru wake umepandishwa kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40.

Kasi hiyo ya ongezeko imegusa pia magari chakavu zaidi, ambapo Mhe. Balozi Khamis amebainisha kuwa magari yenye umri unaozidi miaka 20 na kuendelea sasa yatatozwa ushuru mkubwa wa bidhaa wa kiwango cha asilimia 50.

Akitolea ufafanuzi lengo la hatua hiyo, Waziri wa Fedha ameeleza kuwa mbali na kuongeza mapato ya serikali, mkakati huo unalenga kupunguza uingizaji wa magari hayo mabavu ambayo yamekuwa yakisababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kupitia uzalishaji wa taka ngumu, ambazo zimekuwa zikitumia gharama kubwa kuziteketeza.

Mhe. Balozi Khamis amelihakikishia Bunge kuwa hatua hizo mpya za ushuru wa bidhaa kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 355.09.
Duh! Utafikiri Tanzania wanatengeneza magari. …Shida ya kuongozwa na zero brain ndio hii. Watanzania mtapigika sana hadi mtaita maji mma msipochukua hatua
 
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni Juni 11, 2026, ametangaza kupandishwa kwa viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, huku kigezo cha umri wa gari kikichukua nafasi kubwa.

Katika mabadiliko hayo, magari yenye umri wa kuanzia miaka 8 hadi 10 yamepandishwa ushuru kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 20. Kwa upande wa magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 lakini hayazidi miaka 20, ushuru wake umepandishwa kutoka asilimia 30 hadi asilimia 40.

Kasi hiyo ya ongezeko imegusa pia magari chakavu zaidi, ambapo Mhe. Balozi Khamis amebainisha kuwa magari yenye umri unaozidi miaka 20 na kuendelea sasa yatatozwa ushuru mkubwa wa bidhaa wa kiwango cha asilimia 50.

Akitolea ufafanuzi lengo la hatua hiyo, Waziri wa Fedha ameeleza kuwa mbali na kuongeza mapato ya serikali, mkakati huo unalenga kupunguza uingizaji wa magari hayo mabavu ambayo yamekuwa yakisababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kupitia uzalishaji wa taka ngumu, ambazo zimekuwa zikitumia gharama kubwa kuziteketeza.

Mhe. Balozi Khamis amelihakikishia Bunge kuwa hatua hizo mpya za ushuru wa bidhaa kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 355.09.
Duu kazi ipo.
 
Back
Top Bottom