Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,713
Rais Jakaya Kikwete
Akizungumza baada ya kukabidhi funguo za magari hayo, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Chetan Shah alisema magari hayo yatasafirishwa na kuwasili rasmi nchini kuanzia mwezi Julai mwishoni hadi Agosti.
"Tunakukabidhi magari haya ya kubeba wagonjwa kwa ajili ya kusambazwa maeneo mbalimbali, ikiwemo vijijini. Wazo la kutoa msaada huu nililipata nilipotembelea Tanzania na kushuhudia namna wananchi hasa wa vijijini walivyokuwa wakitaabika kwa kukosa huduma za afya kutokana na ukosefu wa usafiri," alisema Shah.
Alisema amekuwa akitembelea Tanzania mara kwa mara hasa kutokana na biashara ya kampuni yake ya madini na ndipo alipopata uamuzi wa kutoa magari hayo kusaidia wale wote wasio na uwezo wa usafiri katika sekta ya afya.
Kwa upande wake, Rais Kikwete aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kukiri kuwa bado kuna maeneo nchini yenye uhitaji mkubwa wa magari ya wagonjwa. "Hili ni eneo ambalo ki ukweli bado lina uhitaji mkubwa.
Tunashukuru sana kwa kufikiria kutusaidia na kwa kweli msaada huu utatufaa sana," alisema.
CHANZO: Habari Leo(19 JUNE 2015)