Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Kikwete afanye nini Kuuokoa Urais wake?

Viongozi wengi wanapokuja kuomba kura (kwa walewanaochaguliwa kwa kura) wanakuja kwa unyenyekevu na kutoa ahadi mbalimbali kwa wananchi, lakini wakisha pata, basi inakuwa tofauti kabisa na waliyo sema. MIMI NAWAFANANISHA NA PAKA ANAYETAKA MFUPA,ATAKUBEMBELEZA NA KUKUFUTA KWA MKIA WAKE ILI UMPE, UKISHA MPA, ANASAHAU KUWA WEWENDIYE ULIYEMPA NA UKITAKA KUMNYANG'ANYA, YUKO RADHI AKUPARUE KWA MAKUCHA YAKE.Hii ndo tabia ya viongozi wa kitanzania.
 
Ukweli unabaki kuwa, serikali ya CCM inaendelea kutojali kwa kujua kuwa hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kufanya lolote kurekebisha hali iliyopo. Vyama vyote vya upinzani havionyeshi kukomaa vya kutosha kuwa tishio kwa CCM. Kwahiyo wakulaumiwa ni hao hao wapinzani. Bahati mbaya wanatumia nguvu nyingi kuilaumu CCM badala ya kunadi sera zao na kujenga imani ya waTanzania kwao ili wapate support inayohitajika kujenga chama imara. Vilio haviwezi kuleta mabadiliko Tanzania.

Kwa upande mwingine, Wakenya nao wanaanza kujiuliza kwanini wana Mahakama za Kadhi kwenye Katiba yao. Kumbuka, wamekuwa nazo kwa muda mrefu sana. Mjadala unaoendelea hapa ni mabadiliko ya Katiba (Constitutional Reforms) na moja ya ajenda ni kuondoa Mahakama za Kadhi kwenye Katiba mpya ya Kenya.
 
Kwa kadiri mambo yanavyokwenda na kwa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo mzigo wa Matumaini ambao Rais Kikwete alichutuma kuubeba ndivyo unavyozidi kuwa mzito na unaozidi kumuelemea.

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi bila ya shata atatambua kuwa Rais Kikwete hawezi kuwa mwenye furaha. Bila ya shaka manung'uniko yanamkera na zaidi ya yote yale yanayoendelea kwenye Chama "chake". Mgongano wa mawazo unaoendelea kwenye vyombo vya habari, masuala ya mikataba ambayo watu walifikiria yameisha na Mkapa, siyo tu vimetia doa bali vimepaka rangi mbaya kabisa kwenye utawala wake.

Kikwete sasa hivi hana jinsi bali kucheza "pata potea". Anao uamuzi wa kuendelea na timu ile ile ya watu 60, na kutarajia mabadiliko kwa kutumia makaripio na barua za maonyo na uelekezaji, au anaweza kubadili mwelekeo wa utawala wake. Vyovyote vile atakavyofanya, Rais Kikwete anakabiliwa na mtihani mkubwa kabisa wa utawala wake hadi sasa.

Je, atakuwa ni Rais ambaye atashuhudia kumeguka kwa CCM? Je atakuwa ni Rais ambaye ameshindwa kuwadhibiti watu aliowateua na kusababisha kambi siyo kwenye chama tu bali pia kwenye utendaji?

Ana uchaguzi wa kuona ni jinsi gani anaweza kuokoa Urais wake, CCM na hatimaye yeye mwenyewe kutoka katika historia ambayo imeanza kuandikwa?

Afanye nini Rais Kikwete ili auokoe Urais wake, aiimarishe CCM, na zaidi ya yote aweze kutimiza ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania?

How sure are we that he cares anyway!

Watu wanasema kikubwa alichokuwa anakitaka JK ni kuwa Rais. Na jinsi mambo yanavyoendelea kujitokeza ni kwamba aidha hajali ama amekata tamaa hataki kujishughulisha sana kurekebisha status quo, anaona 'bora liende'. Lakini, kinachoonekana ni kwamba anataka urais wake uwe wa vipindi vyote viwili ndio maana anakwenda kwenye sehemu ambazo zinakasoro 'kwake' na kujaribu kuweka mambo sawa kwa mfano Mkoa wa Mbeya.

Kwa mazoea ya nchi yetu na kwa doctrine ya 'amani na utulivu' iliyopandwa na kushamiri akilini mwetu na uvumilivu wa wananchi, ambavyo vinatumiwa kama silaha ya kujihami kwa viongozi, JK anaweza asihitaji kufanya lolote zaidi ya kuacha mambo na matatizo yanayolikabili taifa letu yajitatue yenyewe kama ambavyo amekuwa akifanya. Hatujamsikia akitoa sauti ya kukemea yanayoendelea. Kama angelikuwa anajali angelishayashughulikia yote kwa kukemea kwa sauti kali na baadhi ya matatizo yangerekebika.

Nasema hivyo kwa sababu kwa upande mwingine wanaomfahamu JK kwa karibu zaidi wanasema anaweza kabisa kuamua kuandika historia ya aina yake kwa kugeuka mbogo na kulirudisha taifa katika mstari. Pamoja na 'tabasamu' lake, anayo hulka ya kiburi na ukali. Uwezo wakugeuka mbogo kwa manufaa ya Taifa anao na lolote linaweza kutokea iwapo tu atataka kufanya hivyo.

Tupo tunaoamini kwamba anaweza kuandika historia na ataiandika, whether for better or for worse ni uamuzi ambao uko ndani ya uwezo wake.
 
mi naona hana cha kufanya zaidi ya kukaa kimya kama anavyofanya sasa na kuamka 2010 kupiga porojo za kuomba kula tena
 
gademu!.. I wrote this in 2007!

Je, atakuwa ni Rais ambaye atashuhudia kumeguka kwa CCM? Je atakuwa ni Rais ambaye ameshindwa kuwadhibiti watu aliowateua na kusababisha kambi siyo kwenye chama tu bali pia kwenye utendaji?

Ana uchaguzi wa kuona ni jinsi gani anaweza kuokoa Urais wake, CCM na hatimaye yeye mwenyewe kutoka katika historia ambayo imeanza kuandikwa?
 
Mimi namshauri kama kweli ameingia kweny urais kwa peas za mafisadi, basi akiri ilo na aombe msamahaa kwa watanzania, and then awe kinyume na mafisadi wote na atoe amri ya kuwachukulia atua za kisheria. Nadhani akifanya hivyo ataiokoa nchi na kuponya nafasi yake ya urais
 
Nadhani ajiuzulu ampishe Salim A. Salim au Dr. Mohamed Shein au pengine Magufuli Pombe John
 
Wee bwana wee, kelele za vyura kisimani havimzuii tembo kunywa maji. Kikwete atapeta kwa asilimia 85 mwaka 2010 pamoja na madudu yote haya. Unakumbuka bunge la rubber stap la enzi ile ya 47? Watu wanapiga kelele weee, watasema mate yakiwatoka kaa chizi vile, ati wana hasira sana na uozo wa wizara na serikali, halafu sentensi ya mwisho niiiiii? "NAUNGA HOJA MIA KWA MIA"

Lyatonga alibebwa kwa shangwe na vifijo, akajua kalamba dume, lakini mwisho ulikuwaje? Hata kura aliyoipiga yeye mwenyewe haikuhesabika, achilia mbali aliyopiga mke wake, wanae na bintize na wapwa! Akalalama kweli sababu kahujumiwa, lakini tukaambiwa "haioni Ikulu ng'o! aendelee kubebwa.

Kwa hiyo hizo kelele za ufisadi sio roadblock kwa Kikwete kwenda Ikulu. Anaingojea roadblock ya 2015 ambayo kwa kweli hana ujanja ila kama atageuka dikteta. Swali la Kikwete afanye nini kunusuru uraisi wake linafaa kuliuliza 2014.

Leka
 
Nadhani ajiuzulu ampishe Salim A. Salim au Dr. Mohamed Shein au pengine Magufuli Pombe John

smdh1.gif
 
Kwa maoni yangu hakuna chochote atakachoweza kufanya ili kurudisha imani ya uongozi wake mbovu ambayo imepotea miongoni mwa Watanzania walio wengi. Kuinusuru nchi katika janga kubwa siku za usoni ni bora tu atangaze kwamba 2010 hatagombea tena.
 
Breaking News!

Amerudi kutoka Misri na ameitisha "Emergency Cabinet Meeting" leo jioni.

We shall wait and see how atatokajetokaje kwenye kitanzi hiki. Lakini nahisi mambo yatakuwa yale yale ya inaction, which it seems to me is a valid option in Tanzanian politics - Do Nothing!
 
Breaking News!

Amerudi kutoka Misri na ameitisha "Emergency Cabinet Meeting" leo jioni.

We shall wait and see how atatokajetokaje kwenye kitanzi hiki. Lakini nahisi mambo yatakuwa yale yale ya inaction, which it seems to me is a valid option in Tanzanian politics - Do Nothing!

Emeregency meeting for what? yaani siku zote hizi hajawahi kuitisha emergency meeting hadi hii leo? In my opinion this too little too late. It is time for him to announce that he won't participate in next year's election.
 
.........Huyu mwakani CCM watamchagua tena kugombea urais, maana hadi afikishe miaka 10 ya utawala.
Kwa akili ya wapiga kura wa Tanzania wataichagua tu CCM hata kama Kikwete hakufanya vizuri katika kipindi hichi alichotawala.Tatizo asilimia kubwa ya wapiga kura wapo vijijini, na huko vijijini hao wanachojua ni CCM tu chama cha Nyerere.
Unaleta ma-dharau kwa sisi tulioko kijijini sisi tuna akili nyingi kuliko nyie mlioko mjini na tunajua rais wetu anatupenda sisi watu wa kijiji barabara nyingi zimeanza kujengwa kwa kiwango cha lami..na tunajua vyama vingi..lol usitudharau
 
Migomo ni dalili ya demokrasia na uhuru ambao ndio azma yake..ulifikiri watu hawakogoma zamani kwasababu gani kumbuke enzi zile makaburi walisindikizwa kwa polisi..uhuru ni haki yako migomo na maandamo yanaendelea duniani kote kila siku..labda ugeni wako katika demokrasia ndio tatizo.

Kwi kwi kwi
Mpeni maji ya kunywa.... ya kogoma.
 
bwa ha ha ha...

Halafu inachekesha sana kumsoma anayejiita kuwa mpinzani na "mwanachama mwandamizi wa CUF" akitokwa mipovu kumtetea Kikwete.
jinyonge nipo huru ..unafikiri upinzani ni kupinga kila kitu? after all unataka nimsupport mbowe?? na slaa??? ha ha unachekesha?
 
Back
Top Bottom