Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,633
- 6,229
Mtu B,
Je hawa watu wako huwa wanawaonea huruma hawa watu?
Hizo picha mbili ni athari za mgodi wa dhahabu Mara ambazo aliyeweka sahihi anafahamika. Watu wanaumia na wao wanapeta tu na mashingi yao ya bei mbaya. Halafu huyu kama ni mama au mdogo wako/mwanao, unategemea kuwa utajisikia huruma?
Angelikuwa anachakalika kuokoa watu kama hao juu, amini amini nakuambia, hata Dr.Slaa asingelikuwa maarufu na sanasana wangelikuwa wote serikali na huku akimfanya Dr. Slaa kuwa PM wake na siyo huyo Mamvi aliyekuja kukomba hela bila hata kunawa. Hapo hatujamzungumzia Mkono na Rostam Azziz ambao hao ndiyo kabisaaaa.........

Kweli nimetazama anavyoanguka kwenye hii video imeniuma sana na imenisikitisha. Katika hali ya ubinadamu, inasikitisha sana kuona binadamu mwenzio akizimika vile. Halafu alipoanza kusema 'aise' kabla hajaanguka, nadhani alikuwa anajisikia vibaya sana au maumivu lakini akajikaza aendelee na hotuba. Nimeumia pia jinsi sauti ilivyoanza kufifia kama anayetaka kutafuna ulimi, yaani kama ni ndugu yako yuko katika hali hiyo utatishika sana.
Kama kuna wanaofurahia kitendo cha binadamu mwenzao kuteseka vile mbele ya watu, hao ni makatili tu. Hakuna siasa hapa. Siasa ni kupingana kwa hoja na si kutakiana mabaya. Mimi napinga CCM kwa dhati, lakini nimesononeshwa sana na madhila yaliyompata JK pale jukwaani. Kama binadamu mwenye umri sawa na babangu, nimemtazama anavyoanguka kwa masikitiko makubwa, ikanijia picha kama babangu mzazi akianguka vile mbele ya umati, itakuwaje. Nimeumia sana.
Pole sana mheshimiwa, Mungu akujalie afya njema uwe salama, urudi kwenye mpambano. Tunahitaji mpambano baina ya watu walio wazima wa afya ndio maana napenda upone, tupate nafasi ya kukusikia katika kampeni, ujibu hoja zetu ukiwa mzima tufanye uchaguzi tukiwa tumesikia hoja za wagombea wote.