GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Kweli nimetazama anavyoanguka kwenye hii video imeniuma sana na imenisikitisha. Katika hali ya ubinadamu, inasikitisha sana kuona binadamu mwenzio akizimika vile. Halafu alipoanza kusema 'aise' kabla hajaanguka, nadhani alikuwa anajisikia vibaya sana au maumivu lakini akajikaza aendelee na hotuba. Nimeumia pia jinsi sauti ilivyoanza kufifia kama anayetaka kutafuna ulimi, yaani kama ni ndugu yako yuko katika hali hiyo utatishika sana.

Kama kuna wanaofurahia kitendo cha binadamu mwenzao kuteseka vile mbele ya watu, hao ni makatili tu. Hakuna siasa hapa. Siasa ni kupingana kwa hoja na si kutakiana mabaya. Mimi napinga CCM kwa dhati, lakini nimesononeshwa sana na madhila yaliyompata JK pale jukwaani. Kama binadamu mwenye umri sawa na babangu, nimemtazama anavyoanguka kwa masikitiko makubwa, ikanijia picha kama babangu mzazi akianguka vile mbele ya umati, itakuwaje. Nimeumia sana.

Pole sana mheshimiwa, Mungu akujalie afya njema uwe salama, urudi kwenye mpambano. Tunahitaji mpambano baina ya watu walio wazima wa afya ndio maana napenda upone, tupate nafasi ya kukusikia katika kampeni, ujibu hoja zetu ukiwa mzima tufanye uchaguzi tukiwa tumesikia hoja za wagombea wote.
 
Fidel Castro alipoanguka jukwaani alikaa akatafakari. Sasa hivi sio Rais wa CUBA alioiunda yeye na kuwakabili Wamarekani vilivyo. Amemwachia mdogo wake potelea mbali hata kama sio demakrasia kwa vigezo vya Magharibi. JK akae atafakari upya. Ikibidi Ridhiwani aliyesaka wadhamini awe Rais wetu!( Nimewakwaza wengi?)
Vinginevyo EL ambaye inaaminika walikubaliana kuwa atakuwa mrithi wake achukue nafasi hiyo kuliko kuongozwa na mgonjwa tena ugonjwa unaogusa akili. CCM mnataka kuipeleka wapi TANZANIA yetu?
 
Kweli nimetazama anavyoanguka kwenye hii video imeniuma sana na imenisikitisha. Katika hali ya ubinadamu, inasikitisha sana kuona binadamu mwenzio akizimika vile. Halafu alipoanza kusema 'aise' kabla hajaanguka, nadhani alikuwa anajisikia vibaya sana au maumivu lakini akajikaza aendelee na hotuba. Nimeumia pia jinsi sauti ilivyoanza kufifia kama anayetaka kutafuna ulimi, yaani kama ni ndugu yako yuko katika hali hiyo utatishika sana.

Kama kuna wanaofurahia kitendo cha binadamu mwenzao kuteseka vile mbele ya watu, hao ni makatili tu. Hakuna siasa hapa. Siasa ni kupingana kwa hoja na si kutakiana mabaya. Mimi napinga CCM kwa dhati, lakini nimesononeshwa sana na madhila yaliyompata JK pale jukwaani. Kama binadamu mwenye umri sawa na babangu, nimemtazama anavyoanguka kwa masikitiko makubwa, ikanijia picha kama babangu mzazi akianguka vile mbele ya umati, itakuwaje. Nimeumia sana.

Pole sana mheshimiwa, Mungu akujalie afya njema uwe salama, urudi kwenye mpambano. Tunahitaji mpambano baina ya watu walio wazima wa afya ndio maana napenda upone, tupate nafasi ya kukusikia katika kampeni, ujibu hoja zetu ukiwa mzima tufanye uchaguzi tukiwa tumesikia hoja za wagombea wote.

Sawa kabisa mkuu, wengi sana humu ndani tumemhurumia. Pia Dr Slaa na Prof Lipumba nao waliweka siasa pembeni wakaonesha huruma zao kwa binadamu mwenzao aliyepata tatizo kubwa kiasi hicho.

Ila mbona yeye mwenyewe hajihurumii? Nadhani mwisho wa siku hata sisi tukishindwa kumwonea huruma hatutastahili lawama!
 
Kuanguka Ni dalili kuwa afya yake si nzuri hivyo Watanzania tumpumzishe, tumpe mwingine jukumu hili kubwa la kuongoza nchi kuliko kumpa mgonjwa majukumu wakatati tukijua kuwa afya yake si nzuri. Tutakuja kumuua bure!!
CHADEMA Oyeeeeeeeeeeee
 
Mods, mbona ile picha ambayo mkulu kabebwa mmeiondoa? Can you give us details? Kumetolewa shinikizo nini?
 
Rais wetu keshaamka. Nawasifu JF. Hakuna chombo kingine cha habari kilichothubutu kuweka picha ya aina ile hapa Tanzania.
 
Ushauri wangu kwa wanajukwaa wote, ukiweka mbali siasa za vyama sisi sote tu watanzania. Linapotokea jambo lisilo la furaha na tulipokee hivyo kama Watanzania, la Furaha nalo tulipokee kama Watanzania. Jambo la kuanguka Raisi wa Nchi si jambo dogo, linaweza hata kuathiri bei za Hisa za Makampuni yalijaindikisha DSE. Tucheke pale panapostahili kucheka, panapohitaji pole na tuseme pole, ushabiki mwingine haujengi!!!

Acha kukariri: Tanzania ina soko la hisa la kiasi hicho? Hisa za TBL haziwezi athiriwa na kuanguka kwa raisi anyeumwa: kwa sababu akianguka, watu hunywa zaidi ama kwa kufurahi, au kusikitika. Raisi ni mgonjwa; hii ni mara ya tatu kuanguka hadharani, hatujui ameanguka mara ngapi nyumbani. Sertiously, hakuna cha huruma hapa, hapa ni facts. Aamue kupumzika, ampishe Dk Bilali au who ever fits ili yeye awe raisi aliyestaafu, aweze kupumzika. Kama umati wa watu unamfanya aanguke vile, vipi siku tukivamiwa na nchi jirani, si atazimia kabisa?
Kwanini hataki kupumzika? Kwani aliahidiwa kuwa he is the best president Tanzania can't have? Ametumikia miaka mitano, kama kweli hana madhambi apumzike. Kinachomfanya ang'ang'nie hiyo post ni kwa vile ameharibu mahali, na hivyo anahitaji muda kurekebisha. Watu wasafi hawang'ang'anii madaraka hivi. Igga mfano wa Thabo Mbeki.
Hatuwezi kumhurumia mtu asiyejihurumia.
Tutampa pole, lakini kwanza ajipe YEYE pole na ajihurumie .......
 
Rais wetu keshaamka. Nawasifu JF. Hakuna chombo kingine cha habari kilichothubutu kuweka picha ya aina ile hapa Tanzania.
Wildcard acha kuongopea watu mchana mchana

01.jpg

006.jpg

003.jpg
 
Kuna unachokiona kwenye picha hizo za magazeti zaidi ya hao jamaa wa UwT? Hebu angalia tena ile picha iliyokuwa JF. Kuna kitu cha JK utakiona tu.
 
Hiv hapa jamvini hakuna wataalamu wa afya watueleze ukweli? Sio siri tena, afya ya JK sio nzuri na haijaanza leo, ni tatizo alilonalo muda mrefu na analifahamu.

Muuguzi mmoja alinifahamisha kuwa hizo huwa ni dalili za kifafa, kwamba humtokea mtu anapokuwa excited. Kwa mazingira ya sasa ya JK niwazi yuko excited. Zaidi ya hapo amejiongezea strees, kutoka zile za kuwemo safarini kila siku hadi zinazotokana na msimamo hasi wa wafanyakazi dhidi yake baada ya kutoa matamshi yenye kashfa na sasa ndio anatambua madhara yake kwa safari yake kurudi Magogoni. Ujio wa Dr Slaa kwenye kinyang'anyiro cha Urais ni jambo ambalo hakulitegemea, alitegemea mteremko ule ule kutoka kwa kina Lipumba, ghafla anaingia mpambanaji wa kweli, imemuongezea stress.

Jambo la msingi hapa ni Watanzania, hususani CCM kuachana na unafiki, kuingalia afya ya mgombea wao katika uhalisia wake badala ya kulionea aibu
 
mods natoa shukurani zangu kwa kuondoa video ile..................inaweza kupelekea mtu akapata nightmere!
 
Kuna unachokiona kwenye picha hizo za magazeti zaidi ya hao jamaa wa UwT? Hebu angalia tena ile picha iliyokuwa JF. Kuna kitu cha JK utakiona tu.
Picha gani mkuu labda unasema hii

watanzania na unafiki ndiyo maana hatuna maendeleo sasa hii video ina kitu gani cha ajabu mpaka watu wengine wanaitoa kulinda heshima sijui nini upumbavu nothing graphic at all
Video mbona bado zipo na watu tumezicopy kwa kumbukumbu kuwa kuna siku rais wetu alidondoka jukwaani, angalia post no.1.
 
ai jamani nyie ...........angekuwa baba yenu nyie mngefurahi anadishwe kila kona alivyoanguka na alivyobebwa kama maiti?
 
Hiv hapa jamvini hakuna wataalamu wa afya watueleze ukweli? Sio siri tena, afya ya JK sio nzuri na haijaanza leo, ni tatizo alilonalo muda mrefu na analifahamu.

Muuguzi mmoja alinifahamisha kuwa hizo huwa ni dalili za kifafa, kwamba humtokea mtu anapokuwa excited. Kwa mazingira ya sasa ya JK niwazi yuko excited. Zaidi ya hapo amejiongezea strees, kutoka zile za kuwemo safarini kila siku hadi zinazotokana na msimamo hasi wa wafanyakazi dhidi yake baada ya kutoa matamshi yenye kashfa na sasa ndio anatambua madhara yake kwa safari yake kurudi Magogoni. Ujio wa Dr Slaa kwenye kinyang'anyiro cha Urais ni jambo ambalo hakulitegemea, alitegemea mteremko ule ule kutoka kwa kina Lipumba, ghafla anaingia mpambanaji wa kweli, imemuongezea stress.

Jambo la msingi hapa ni Watanzania, hususani CCM kuachana na unafiki, kuingalia afya ya mgombea wao katika uhalisia wake badala ya kulionea aibu

Ukiangalia hiyo picha utagundua kwamba mke wa JK halii bali anasononeka wakati majirani zake wanalia. Hivi hiyo inaashiria nini????
 
Back
Top Bottom