Kikuu vs AliExpress

kamati yamaamuzi magumuu

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
227
262
Samahani Wana JF, nimekuwa na uzoefu kidogo na kuagiza bidhaa China kupitia Kikuu App.

Wana kasoro kadha wa kadha, mfano kuchelewa kufikisha kwa baadhi ya bidhaa, ufinyu huduma kwa wateja kulingana na wingi wa wateja wenyewe, pia ubora wa bidhaa baadhi huwa sio bora.

Nimejaribu kuuliza kwa baadhi ya watu wengi wao wananishauri nitumie AliExpress japo sijawahi kuwatumia, wana unafuu.

Sasa mchango wenu kati ya Kikuu na AliExpress yupi bora.

Nakaribisha maoni si kejeri wana JF.
 
sijawahi kutumia kikuu, huwa natumia aliepress na vitu vinanifigiaga wilayani kabisa.

Vitu unavifuata posta na mzigo unaweza kutrack kwa kutumia website ya posta tz pia.

ila kwa kuitazama website ya kikuu wanafanya dropshing kwa aliexpress.

Nunua vitu pia kwa aliexpress, then utapata experience ya kipi bora.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kikuu na Aliexpress.

Huduma kwa wateja

Aliexpress wana huduma bora sana kwa wateja, kuanzia kuhakikisha ubora wa bidhaa, usalama wa pesa zako na hata kurudishiwa pesa zako, kitu ambacho ni tofauti sana na Kikuu.

Ufikishwaji wa mizigo

Aliexpress mzigo unafika hadi posta ya mwisho wa wilaya yako, na unaweza kuj track mzigo wako baada ya siku 5 hadi 10

Usalama wa pesa zako

Ukinunua kitu aliexpress, pesa zote huwa zinakuwa chini ya aliexpress mwenyewe, na muuzaji atapewa pesa pale tu utakapothibitisha kupokea mzigo wako na kiridhika nao, vinginevyo aliexpress atakurudishia pesa zako

Refunding process

Aliexpress refunding yao ni ya uhakika na ya haraka zaidi, pesa zinarudishwa kwenye account hako ndani ya muda mchache sana.

Karibu sana mkuu
 
sijawahi kutumia kikuu, huwa natumia aliepress na vitu vinanifigiaga wilayani kabisa.

Vitu unavifuata posta na mzigo unaweza kutrack kwa kutumia website ya posta tz pia.

ila kwa kuitazama website ya kikuu wanafanya dropshing kwa aliexpress.

Nunua vitu pia kwa aliexpress, then utapata experience ya kipi bora.
Aliexpress unalipa kwa mpesa?
 
Mkuu nataka kuagiza Nokia 2 aliexpress hatua gani nipitie?
 
Aliexpress...ndo nmeagiza mzigo natarajia..kupokea soon..nikiupata bila ttzo lolote ntakupa mrejesho..sema shida iliyopo mzigo unachukua siku nyingi kufika.
 
Aliexpress unalipa kwa mpesa?
Master card au visa card.

Kwa m-pesa inabidi utumie m-pesa master card.

Hatua za kutengeneza m-pesa master card.
1. Bofya *150*00#
2. Chagua lipa kwa mpesa.
3. M-pesa master card.
4. Tengeneza card
5. Utapata details za card yako.

Ukija kwa benki, tumia equity bank au banc abc.

Ila nimeeona m-pesa master card ni nzuri maana kama mzigo haykufika au nimeletewa ndivyo sivyo na nikifungua dispute basi refund yangu inakuja moja moja kwenye simu hata kama card imeexpire.
 
Back
Top Bottom