Uwe na master card, visa card au m-pesa master card kwa ajili ya malipo.
Ingia aliexpress na ujisajili kutumia e-mail yako.
Anza kutafuta bidhaa unayoitaka yaani nokia 2.
Bonyeza button ya buy.
Itakuja page yenye sehemu ya kuweka information za card pamoja na shipping address.
Kwenye shiping address utaweka sanduku la posta au kama hauna unaweka jina la wilaya mkoa, cha msingi ni namba na majina yawe yale yaliyo kwenye vitambulisho vyako.
Kwa sababu posta watahitaji kitambulisho.
Baada ya hapo place order, baadae seller atakupa tracking namba kufuatilia mzigo umefikia wapi.
Unaweza tumia web ya 17track kufuatikia mzigo, zipo nyingi tovuti za namna hiyo.
Then vumilia kwa wastani itachukua wiki tatu ila kama utakuwa na haraka tumia dhl ila gharama zake si za kitoto.
Usisahau kucheki reviews kabla ya kununua