3D Printers, Design, 3D Scanning, and other related technology special thread.

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,532
3,316
Salaam wana tech.

Kama heading inavyosomeka hapo juu, huu uzi utajikita kwenye 3D printing, designing & etc.

Lengo la kuanzisha huu uzi ni kutokana na umuhimu wa ukuaji wa teknolojia ya 3D printing na wingi wa faida zake na kwenye hii forum ya JF hamna popote imezungumziwa kwa undani, zaidi ya kuwa mentioned kwenye baadhi ya posts.

Ila wapo watu kwenye hii field kwa Tanzania yetu japo si wengi sana, hivyo basi nategemea thread hii itawaunganisha wote waliopo kusambaza awareness na uzoefu kwa wengine watakaopenda kujifunza zaidi kuhusu 3D printing technology.



Baada ya maelezo hapo juu, nitazungumzia 3d printing & 3d printers kwa kifupi kwasababu kuna maarifa mengi sana ukitumia google, youtube kwa beginers, hivyo basi hii itakua kama kufungua macho tu kwa mafunzo zaidi zipo articles, videos na tons of info kwa mtandao.
Mtanisamehe nitachanganya lugha maana baadhi ya misamiati ya kiswahili ni migumu.

3D printing ni aina moja wapo ya industrial production process, na inafahamika kama additive manufacturing kwa maana kitu kinatengenezwa au kuundwa kwa kuongeza material, ukiacha additive manufacturing pia kuna Subtractive manufacturing hii utendaji wake ni kinyume cha additive manufacturing kwamba kitu kinaundwa ama kutengenezwa kwa kupunguzwa materials,

Mfano hai unaotaka kufanana na hizi concept ni wale wanao tengeneza vinyago, ukichonga gogo ili kupata sanamu labda la mnyama zoezi zima litakua ni kupunguza material kwenye gogo lako mpaka unakuja kupata picha ya mnyama unayemchonga, huu ni mfano kinachoongelewa kwenye substractive manufacturing, kwenye additive inakua unaongeza sasa ni kama unavyojenga nyumba ili nyumba ikamilike unaanzia chini unaenda ukongeza material mpaka nyumba inakamilika.

Hiyo ni mifano tu ili uelewe ufanyaji kazi wa hizi tec, ila katika ulimwengu wa computer hizo process za kuongeza au kupunguza material zinaendeshwa kwa mahesabu ya hali ya juu kuzingatia tolerances na vipimo halisia.
3D inaama ya three dimension, wengi mmesoma algebra mmekutana na x & y graph zile ni 2 dimension (2D) kwa maana kuna axis mbili tu x & y, kwa walioenda mbali kimasomo mmekutana na x, y & z kwa maana ya 3 dimension axes.

Hivyo basi kwenye 3D printing zinatumika 3 axes kuunda kitu, kwa maana kama unataka kuunda kitu, uundwaji utakamilishwa kwa axis zote tatu kutumiwa, na hizi axes ndio muundo wa chombo husika ni kama imaginary skeleton.

Ili uweze kufanya 3D printing unahitaji vitu vifuatavyo
1. 3D printer
2. CAD software
3. Slicer software
3. Filament

Hivyo ni vitu vinne muhimu

Unapokua na vitu hivyo basi kinachobakia ni wewe binafsi uwezo wako wa kubuni vitu, na hata kama huwezi kubuni basi vipo vingi mitandaoni unaweza download uka print kwenye printer yako.

3d printer, kama ilivyo simu au computers 3d printers zipo aina mbalimbali na zenye sifa mbali mbali, zipo za bei kubwa zaidi zipo za bei ya kati na zipo za bei ya chini, zinatofautiana kwa features na uwezo, pia zipo brand nyingi tu zinazo zalisha hizi printer, mfano Ender, Prusa, Ultimaker, Voron, Bambulab na nyinginezo nyingi.

CAD software zipo aina nyingi sana, hii ndio hutumika kuandaa michoro au 3D models ambazo utahitaji kuzi print hapo mwishoni. baadhi ya hizi ni Solidworks, TinkerCAD, FreeCAD, Designspark, Fusion360, Blender na nyinginezo nyingi.

Slicer software, pia zipo kadhaa, hii kazi yake ni kutafsiri 3d models ulizofanya kwenye CAD software na kuzibadilisha kuwa katika mfumo wa gcode, lugha ambayo 3d printer inaelewa maana inacheza na coordinates positioning kwenye zile 3 axes. mfano wa hizi kuna Cura slicer, Ocra, Bamb slicer na nyinginezo.

Filament, hizi ni material ambazo hutumika kwenye 3d printer kuunda kitu unachotaka, zinakua katika spools ufanyaji kazi wake ni zinayeyushwa na kukaushwa wakati wa uundaji, zipo aina nyingi plastics, metals, wood, n etc.

3D printers maarufu zaidi na zinazotumiwa na watu wengi sana ni hizi

3328.jpg


ender 3v2.jpg


Filament
Kama nilivyoelezea hapo juu filament ndio material zinatumika hivyo basi zipo aina kadhaa za filament, ila kwa hapa tutaangalia za plastic zaidi, hizi aina zinatofautiana vitu vingi kwenye chemical composition level hivyo basi matumizi yake yatategemea mlolongo ufuatao

1. Kitu cha kwanza sio material zote zipo supported kwa printer zote, katika zoezi la uchaguzi wa material inabidi kuangalia uwezo wa printer yako, kisha ujue unachotengeneza kinaenda kufanya kazi gani, hivyo ni muhimu kujua kwa undani aina za material, itakusaidia kukamilisha project zako kwa ufasaha

Aina za filament (material) ni kama zifatazo;
  • PLA Filament
  • ABS Filament.
  • ASA Filament
  • Carbon Fiber Filament
  • Nylon Filament
  • FLEX Filament.
  • HIPS Filament
  • PVA Filament
  • PETG Filament
  • TPE Filament
  • PC Filament
Hizo ni baadhi ya material zinazotumika kwa wingi zaidi ila pia zipo aina nyingine na bado kilakukicha zinakuja mpya, katika hizo PLA ndio maarufu zaidi kwasababu ya urahisi wa bei pia utengenezwaji sio wa gharama kama aina nyinginezo imatengenezwa kwa corn.

Hizi filament znakuja kwa uzito tofauti tofauti, kuna za 1/2 KG, 1KG & 2KG na zaidi kulingana na mahitaji ya wateja
pia zinakuja za rangi tofauti tofauti.
816BNH8c2PL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg




*******************^^^^^^^^*********^^^^^^^^*************^^^^^^^^**********



Updates 20/08/2023

Uzi nitakua naendeleza kidogo kidogo kama nilivyosema yapo mengi ya kuandika na kufafanua vyote haviwezi kuisha kwa siku moja au mbili.

Mara ya mwisho tuliangalia aina za material kwa maana ya filament zinatotumika kwenye 3D printers, kwa kuzingatia utofauti wa sifa ya kila filament, pia zinatoa fursa ya kuchagua filament kuendana na matumizi ya unachotaka ku print na uwezo wa printer yako.

Faida za 3D printing
Kwa dunia ya sasa 3D printing imekuja kuwa na umuhimu mkubwa sana hasa kwa industrial designers, Engineers, tuseme katika field zote tu hata kwenye medical field ipo kwa sana.

Kwanini imekua na umuhimu sana?
Imekua na umuhimu kwasababu imerahisisha kupunguza gharama na muda katika bunifu mbalimbali, mfano mdogo ni huu, unapobuni biadhaa yako kwa matarajio ya kuja kuuza kama product kamili kuna mchakato hapo katikati, kwa maana ya kuhamisha wazo mpaka kuja kwenye uhalisia, kwa kipindi cha nyuma ilikua inakupasa kupeleka wazo lako kwenye viwanda/kiwanda walihamishe wazo lako na designs zako katika uhalisia lengo likiwa ni kupata bidhaa iliyo bora na kukidhi matakwa ya wazo kuu, hivyo basi ilikua ni gharama kubwa kwasababu inabidi ulipie gharama za kuaandaa prototypes mbalimbali mpaka kuja kufikia hatua ya mwisho kazi kubwa inakua imefanyika,
Kwasasa ni tofauti kabisa mtu ana wazo atapambana kutengeneza prototype na kuhakikisha anafanyia kazi changamoto zote kwenye prototype husika mpaka anakuja kupata a clean version, hii sasa hata akiipeleka kiwandani kazi inakua ndogo na gharama pia zitapungua, na muda pia utapungua.

Mfano hai mwingine, niliwahi kupata client alihitaji kutengenezewa roller ya aluminium yenye maandishi nadhani kuna bidhaa alikua anazalisha hivyo alikua anaitumia kuweka mark kwenye bidhaa yake, alinipa vipimo vyote, kwasababu hiyo roller kuna sehemu ilikua inafungwa kwenye mashine yake, nilichokifanya nilitengeneza prototype kulingana na vipimo na sifa zote alizotaka nilitumia 3D printer, protoype ilikua na material ya plastic haijakidhi mahitaji ya mteja lakini lengo lilikua ni kuhakiki ile CAD model niliyo design kama ipo sawa, na kweli ilikuwa sawa baada ya kufanya vipimo vyote muhimu.

Hatua iliyofata ilikua kumtafutia mteja hitaji lake la aluminium roller kwa bahati mbaya kwa Tanzania yetu sijaona kampuni zilizowekeza kwenye CNC milling kwa aina ya ile roller ilihitaji kuwa machined na CNC, hivyo basi nikawavutia waya wachina tukajadili nnachotaka, nikawatumia design files, wakanitumia quotation nadhani ilikua kama 75$ per roller, na client alihitaji roller mbili, kama mnavyowajua wabongo tena ile kazi ilikwama mteja hakuonyesha nia tena ya kazi kuendelea.

Nimesema haya nikaweka na story ya client wangu, ili kufikisha ujumbe kwamba hamna kinachoshindikana unaweza uka design product yako na kuizalishia china kama hapa kwetu hamna watu wenye uwezo wa kufanya hivyo, iwe ni kipuri cha mashine au chochote kile na kwa material yoyote unayotaka hata kama ni titanium ni pesa yako tu.


Nitashare project ndogo nimeifanya jana kutatua changamoto ndogo

Kuna mashine ya co2 laser cutter naitumia kwenye workshop yangu, ina changamoto ya kuzalisha moshi sana na muda mwingine toxic fumes kulingana na aina ya material una deal nazo,

Katika kutafuta suluhu ya tatizo hilo nimekutana na mashine ambazo kazi yake ni kuchuja hizo fumes kutoka kwenye exhaust pipe ya laser cutter ila tatizo bei zake ni ghali sana.

Ukiangalia utendaji wa kazi wa hizo mashine za kuchuja fumes hamna cha ajabu sana sana ni fan na baadhi ya air filters pamoja na activated charcoal ambayo unaweza kuitengeneza kwa mkaa wa kawaida ukiongezewa baadhi ya vitu.

Hivyo basi nimeamua kutengeneza filter ndogo ambayo ntakua nabadilisha hizo charcoal maana ndie key player kwenye ufyonzaji wa fumes.

NItaweka picha na maelezo kidogo

IMG_20230820_104406.jpg

Natumia hii 4 inch elbow kwenye outlet exhaust ya mashine na nyuma ya hii elbow kuna inline fan mbili ambazo zinavuta moshi na fumes kutoka ndani ya mashine kwenda nje, hii elbow ipo nje lakini nataka kupunguza makali ya moshi unaopita hapo.



IMG_20230820_104533.jpg

Kabla sijaenda kwenye computer huwa napendelea kuwa na pen na notepad kwa ajili ya rough sketches na vipimo, na kulichora wazo lako inanisaidia kwa upande wangu, kwa hiyo hapa nilichukua vipimo vya hiyo elbow, nilitaka nitengenze filter insert ambayo nitakua naipachika mbele ya elbow na ndani ya hiyo insert kutakua na kama kikombe ambacho ndani yake ile activated charcoal itakua inakaa.


3.jpg

2.jpg

1.jpg

Baada ya kama ya saa moja na nusu hivi nikamalizana na modelling ya hizo parts ntakazotumia kwenye filter yangu, hizi CAD models nimefanya kwenye CAD software kama nilivyoandika kule juu vitu vinavyohitajika ili uweze kufanya printing, kwa hiyo hatua inayofata baada ya hapa ni ku export files kisha nitumie slicer software kwa ajili ya kufanya translation to machine language na mwishoe nitume files kwenye printer kwa ajili ya printing kuanza.



IMG_20230820_110419.jpg

IMG_20230820_110432.jpg

IMG_20230820_110502.jpg

Hizi ni hatua za printing zikiwa zimekamilika.




IMG_20230820_104607.jpg

IMG_20230820_104614.jpg

IMG_20230820_104637.jpg

IMG_20230820_104647.jpg

IMG_20230820_104709.jpg

IMG_20230820_104859.jpg

IMG_20230820_104925.jpg

IMG_20230820_104948.jpg

Na hizi ndio printed parts katika picha tofauti tofauti.





IMG_20230820_105015.jpg

IMG_20230820_105017.jpg

IMG_20230820_105201.jpg

Hatua ya mwisho majaribio coupling, mpaka hapa wazo limeenda kwenye uhalisia kwa asilimia 90, hivyo ntamalizia kuandaa hizo activated charcoal na kuja kuziweka zinapopaswa kukaa na kuangalia ufanisi wa filter hii.


Nimeweka mlolongo wote ili tujifunze wazo linapoanzia, au namna ya kubadili wazo kuja katika uhalisia.

Ahsanteni


Uzi utaendelea yapo mengi ya kuandika.
karibuni.
 
Unaweza kufua engine kw 3D printer?
Sijaelewa kufua unamaanisha nini, ila kama una maanisha kuunda engine, jibu ni ndio zipo taasisi na makampuni wameweza kufanya hivyo ikiwa ni part ya R & D, kama ujuavyo hii teknolojia ya 3D printing bado ni changa, hivyo unaweza pitia mitandao ukajionea baadhi ya engines zilizoundwa kwa process hii.

Unaweza pitia hii link NASA walitengeneza rocket engine
3D Printed Rocket Launched Using Innovative NASA Alloy
 
Sijaelewa kufua unamaanisha nini, ila kama una maanisha kuunda engine, jibu ni ndio zipo taasisi na makampuni wameweza kufanya hivyo ikiwa ni part ya R & D, kama ujuavyo hii teknolojia ya 3D printing bado ni changa, hivyo unaweza pitia mitandao ukajionea baadhi ya engines zilizoundwa kwa process hii.

Unaweza pitia hii link NASA walitengeneza rocket engine
3D Printed Rocket Launched Using Innovative NASA Alloy
3D technology na AI how are they related chief?
 
Stay blessed brother, Huu uzi ni elimu na business idea kiujumla. By the way unaweza kuweka gharama za mashine ya 3D printer?
Kuhusu gharama kuanzia 300,000 unaweza kupata 3D printer ila shida ni reliabilty kwa hizi cheapo printers.

Ila wengi waliongia kwenye 3D printing wameanza na brand maarufu inaitwa Creality wana series za printer tofauti tofauti na bei hutofautiana pia kulingana na features, ila the most popular ones ni ender 3, ender 3v2 kwa yeyote anayeanza 3D printing ningemshauri aanze na hizi kwasababu kuna vingi vya kujifunza na community support ni kubwa aina hizi mbili za printer, bei zake nadhani kwasasa ni kwenye 175USD.
 
3D technology na AI how are they related chief?
Naweza kusema AI is simply a component of technology, hivyo basi kama inavyokua deployed kwenye nyanja zote basi hivyo hivyo na kwenye 3D printing technology pia imekuwa deployed kwenye baadhi ya high end 3D printers kama features kutatua aina kadhaa za changamoto.
 
Naweza kusema AI is simply a component of technology, hivyo basi kama inavyokua deployed kwenye nyanja zote basi hivyo hivyo na kwenye 3D printing technology pia imekuwa deployed kwenye baadhi ya high end 3D printers kama features kutatua aina kadhaa za changamoto.
Tafsir ya neno 'printing" nikirelate na 3D Tech at the same time nikirelate na ile printing ya stationary (hardcopy) napata mkanganyiko kidg
 
Tafsir ya neno 'printing" nikirelate na 3D Tech at the same time nikirelate na ile printing ya stationary (hardcopy) napata mkanganyiko kidg
Hii ni definition ya printing kutoka kwenye english dictionary.
"the art, process, or business of producing books, newspapers, etc., by impression from movable types, plates, etc. the act of a person or thing that prints."

hapo kwenye etc ndio kuna mengineyo zaidi ya paper.
 
Updates 20/08/2023
Kwa wafuatiliaji wa uzi huu nimeweka updates kwenye main thread.
karibuni kwa michango,maswali, maoni n.k
 
Updates 20/08/2023
Kwa wafuatiliaji wa uzi huu nimeweka updates kwenye main thread.
karibuni kwa michango,maswali, maoni n.k
Mkuu Umeme ukikata inakuwaje, kama haijamaliza kuprint, na material yanapatikanaje hizo plastic.
 
Mkuu Umeme ukikata inakuwaje, kama haijamaliza kuprint, na material yanapatikanaje hizo plastic.
Umeme ukirejea kuna option ya ku resume ilipoishia.

Kuhusu material zipo, kuna watu wanauza japo sio wengi sana, njia nyingine ni kuziagiza china.
 
Umeme ukirejea kuna option ya ku resume ilipoishia.

Kuhusu material zipo, kuna watu wanauza japo sio wengi sana, njia nyingine ni kuziagiza china.
Software gani ambayo wewe hutumia, kufanya 3d designing.
 
Hizi
FreeCAD
Sketchup
ANSYS spaceclaim

Ya mwisho ndio naitumia sana.
Sawa mkuu, mi nimezoea tumia sketchup naweza tumia hio kweli ku export model nilizodesignia hapo....!?
Na upatikanaji wa hizo filament hapa kibongo bongo vipi.
 
Sawa mkuu, mi nimezoea tumia sketchup naweza tumia hio kweli ku export model nilizodesignia hapo....!?
Na upatikanaji wa hizo filament hapa kibongo bongo vipi.
Ndio unaweza export, ila tumia STL format unapo export models zako, hizo ndio utatumia kwenye slicer.

Kuhusu Filament kama utakosa unaweza nicheki nnazo pia nauza kwa atakae hitaji.
 
Hizi filament material ulizosema za wood zinapatikana bongo ? Na je naweza kutumia 3d printing katika furniture designing kwa jinsi inavyofanya kazi? Specification za computer kwa ajili ya kukaa izo CAD software zipoje. Kwa mtu ambaye hana chochote kabisaa roughly cost ya kuwa na iyo machine na pc na kila kitu kinacho hitajika inaweza kuwa kiasi gan?
 
Hizi filament material ulizosema za wood zinapatikana bongo ? Na je naweza kutumia 3d printing katika furniture designing kwa jinsi inavyofanya kazi? Specification za computer kwa ajili ya kukaa izo CAD software zipoje. Kwa mtu ambaye hana chochote kabisaa roughly cost ya kuwa na iyo machine na pc na kila kitu kinacho hitajika inaweza kuwa kiasi gan?

Kuhusu kupatikana bongo kiukweli sidhani kwasababu ya demand bando ni ndogo sana au tuseme hamna kabisa

Pili unatakiwa kufahamu, filament za wood zinatengenezwa kwa wood dust zikichanganywa na PLA base, ratio inategemea brand na brand.

Kuhusu specs za computer, bahati nzuri hizi soft hazihitaji computer za uwezo mkubwa sana computer yoyote kuanzia core i3 na minimum RAM ya 4GB unaweza run hizo software.

Kuhusu gharama, kwenye upande wa pc siwezi fanya estimation kwasababu ya variables nyingi zina affect bei.

kwa upande wa printer inategemea budget yako, upo tayari kutumia kiasi gani kwasababu kwa bei kama bei zinaanzia as low as 300k na kuendelea, mind you bei inaakisi uwezo na features za printer husika.

Kama ni kwa ajili ya kuanza nashauri uanze na ender 3 printers, utaweza kujifunza vingi kuanzia troubleshooting na vitu vinginecyo vingi, kadri utakavyooenda mbele unaweza acquire mid to high range models kulingana na uhitaji wa shughuli zako. Gharama zina range 400k-500k kwa hizi model.

Binafsi nilianza na creality ender 3v2, saivi natumia bambu lab P1P, najikusanya nguvu nije kuchukua na bambu lab X1 carbon , hizi moja printer bora sana kwasasa kwenye soko la 3D printing.
 
Back
Top Bottom