Exile
JF-Expert Member
- Feb 21, 2021
- 1,406
- 3,363
Marekani imefanya duru ya nne ya mashambulizi dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen, maafisa wa Pentagon walithibitisha Jumatano usiku.
Baadhi ya makombora 14 ya Houthi, ambayo Marekani inasema huenda yalilengwa kwa ajili ya mashambulizi ya meli katika Bahari ya Shamu, yalilengwa na majeshi ya Marekani.
Centcom - kamandi ya Amerika Mashariki ya Kati - ilisema maeneo hayo yalipigwa na makombora ya Tomahawk yaliyorushwa kutoka kwa meli za Jeshi la Wanamaji la Marekani
Mashambulizi hayo yanakuja huku Marekani ikiwataja Wahouthi kama "magaidi wa kimataifa".
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan alisema hatua hiyo, ambayo ilibatilisha uamuzi wa kuondoa jina hilo katika siku za mwanzo za utawala wa Biden, ni kujibu mashambulizi yanayoendelea ya wanamgambo hao dhidi ya meli za kibiashara katika eneo hilo.
Waasi wa Houthi walianza kushambulia meli za wafanyabiashara mwezi Novemba, wakisema walikuwa wakijibu operesheni ya kijeshi ya Israel huko Gaza. Tangu wakati huo, kundi hilo limeanzisha mashambulizi kadhaa dhidi ya meli za kibiashara zinazopitia Bahari ya Shamu , mojawapo ya njia za meli zenye shughuli nyingi zaidi duniani
Waasi wa Houthi wa Yemen wameilenga meli inayomilikiwa na Marekani katika Ghuba ya Aden baada ya Washington kusema italitaja tena kundi hilo kuwa "magaidi wa kimataifa".
Kundi hilo lilisema liliipiga "Genco Picardy" kwa makombora ambayo yalisababisha "pigo lamoja kwa moja".
Jeshi la Marekani linasema kuwa meli hiyo ilipigwa na ndege isiyo na rubani Jumatano jioni
Chanzo: BBC swahili