Kikosi kazi hiki kimefitinika!

Kikosi kazi hiki kimefitinika!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,694
Reaction score
870,414
Twende kwa namba zao
1. Mwathirika mtupa ganda (hasahau)
2. Mfadhili mwezeshaji (mla ndizi)
3. Mlinzi mkuu (baba)
4. Mtoto mtukutu (mfaidikaji limbukeni)

Kwa wale wazazi nadhani wanaelewa nguvu aliyonayo baba.. Watoto huwa wanaringishiana nguvu za baba zao... Wakichikozana utasikia wakiambizana.... Ntakusemea kwa babaangu! Baba ni kichwa kweli kweli...

Kwa wale wana uswazi. Kule uswahilini kwetu wanajua nguvu walizo nazo baadhi ya wazee mtaani na kwa kukosa weledi watoto wao wasio na makuzi sahihi hutumia nguvu za baba zao vibaya. Hufanya matendo mabaya wakijua fika hawagusiki na hawawezi kulala sero wala kufanywa lolote. Wanaogopeka!

Kuna story inafanana na hii. Ndugu mmoja wa mshirika kibiashara alifanyiwa kitu kibaya kwenye ujasiriamali wao. Aliyemfanyia hivyo akiwa ni mtu mwenye ushawishi na rafiki mkubwa wa mtoto mtukutu, hakujali kabisa maumivu ya mwathirika..

Na mwathirika kila alikopita alikuta tayari Mfadhili keshapita na kufanya yake... Jamaa akawa hana jinsi bali kuishi kama ndezi. Siku zote akitishiwa kuingizwa shimo la Tewa. Kuna wakati alinaswa na kuponea tundu la sindano.

Kila uvumilivu huwa na kikomo. Alipochoka kujificha na kuishi kwa mashaka kama digidigi mbungani akaamua kufunguka. Kupitia uchawi wa kizungu akamfikishia baba ujumbe.

Muda haukupita mfadhili kibanda chake chenye nyasi za kupendeza kikaanza kufanyiwa figisu. Yeye naye mwenyewe na ufadhili wake wote. Hatimaye akatiwa nguvuni na mgambo mkuu. Akajaribu kumtafuta mtoto mtukutu aokoe jahazi. Mtoto mtukutu kamruka pima 20 kwa vipimo vya kielektroniki na makinikia

Mfadhili ana kinyongo, mfadhili ana kisasi. Huyu ndie alikuwa tochi kubwa na punda wa mtoto mtukutu...

Pengine kwa siri ama la pengine baba akiwa na ufahamu. Mtoto mtukutu kupitia mfadhili alijenga kibanda cha ngazi nyingi ambacho urembo mapambo na samani bora kabisa vingetoka huko mji wa nchi ya mbali. Makasha makubwa 20 hakika hicho kibanda kilikuwa cha ngazi nyingi.

Pamoja na mambo mengine yote usaliti wa mfadhili, kisasi. hatimaye kagoma kufadhili makasha yale yanayodaiwa mapene mengi. Muda ukitimia yatapigwa mnanda. Oh sorry mnada... Mnanda ni Ngoma sio UKIMWI lakini

Maswali muhimu....
. Muathirika yuko wapi? Huyu ndio mlipua bomu... Huyu ndie aliyeminya kitufye

. Mfadhili anaendeleaje yuko wapi?

. Nini hatima ya mtoto mtukutu? Je baba ataendelea kumbeba kwa mbeleko kubwa?

. kuna mwingine hakutajwa hapa JICHO LA TAI
 
IMG-20180517-WA0004.jpg
 
Ndugu mmoja wa mshirika kibiashara alifanyiwa kitu kibaya kwenye ujasiriamali wao... Aliyemfanyia hivyo akiwa ni mtu mwenye ushawishi na rafiki mkubwa wa mtoto mtukutu, hakujali kabisa maumivu ya mwathirika... Na mwathirika kila alikopita alikuta tayari Mfadhili keshapita na kufanya yake... Jamaa akawa hana jinsi bali kuishi kama ndezi... Siku zote akitishiwa kuingizwa shimo la Tewa... Kuna wakati alinaswa na kuponea tundu la sindano....
Kila uvumilivu huwa na kikomo... Alipochoka kujificha na kuishi kwa mashaka kama digidigi mbungani akaamua kufunguka... Kupitia uchawi wa kizungu akamfikishia baba ujumbe..

Muda haukupita mfadhili kibanda chake chenye nyasi za kupendeza kikaanza kufanyiwa figisu.. Yeye naye mwenyewe na ufadhili wake wote... Hatimaye akatiwa nguvuni na mgambo mkuu... Akajaribu kumtafuta mtoto mtukutu aokoe jahazi... Mtoto mtukutu kamruka pima 20 kwa vipimo vya kielektroniki na makinikia
Mfadhili ana kinyongo,
Hapa hata nikikaa siti ya mbele mm mtoka Bara hii picha ya Kung fu siambulii kitu
acha wa D'salama mtajatuhadithia kabla haijaisha, ni mara ya kwanza stearling atauawa inavyoelekea
 
Hapa hata nikikaa siti ya mbele mm mtoka Bara hii picha ya Kung fu siambulii kitu
acha wa D'salama mtajatuhadithia kabla haijaisha, ni mara ya kwanza stearling atauawa inavyoelekea
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Naskia alijenga banda la kulala wageni la nyota kadhaa hizoo contena 20 ni za kawaida kwa hiloo banda.


INA semekana kuna nyingine zaja Contena kama tano. Makachero tayari bandari kubaini ukweli kumpelekea baba ushahidi. Labda tuwasiliane na evarist chahal twaweza pata walau mawili matatu.


cocochanel
 
Back
Top Bottom