Kikeke ambana Maalim Seif

Kikeke ambana Maalim Seif

ila BBC rahaa sana kuna yule bint mtangazaji alimuulizaga LOWASA maswali mpaka LOWASA aliomba poo
 
Wacha ukawa washinde bara wajitwalie visiwani hiyo ndio haki na demokrasia mnayoitaka tz??
 
Tupien bas tuone na ss tilioukosa uhondo huo
Hakukuwa na uhondo, sana sana BBC walionesha jinsi gani wana watangazaji wa hovyo. Wewe mtangazaji umeuliza swali, kwa nini usitulie basi lijibiwe? Haya niliyaona hata siku Zuhura Yunusi alipomhoji Edward Lowassa. Mtangazaji anauliza constructive question na anataka jibu liwe kile anachoamini yeye. BBC ni sawa na TWAWEZA...pumba za mchele, hata nguruwe hali
 
Tujiulize kwanza kwanini uchaguzi urudiwe maalimu kama angekubali kurudia uchaguzi maana yake Ingekua amekubaliana na sababu za kufutwa Kwa uchaguzi wa awali sasa swali lina baki pale pale,je kulikua na sababu za msingi za kufuta uchaguzi..?na kama uchaguzi haukua wa haki ni chama gani kililalamika hapo awali kabla ya uchaguzi kufutwa!?
 
Nimefurahishwa sana Salimu Kikeke alivyomuhoji Seif
Kwasababu Seif hakuwa na hoja za msingi kwanini hwakushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar
Kama hakupewa nafasi ya kuongea umejuaje kuwa hakuwa na hoja?
Mtu mwenye akili na uweledi wa kazi, ukiuliza swali sikiliza jibu...sisi tunaotazama na kusikiliza tuhukumu kwa majibu tutakayosikia. Salim Kikeke alikuwa analazimisha yake
 
Hakukuwa na uhondo, sana sana BBC walionesha jinsi gani wana watangazaji wa hovyo. Wewe mtangazaji umeuliza swali, kwa nini usitulie basi lijibiwe? Haya niliyaona hata siku Zuhura Yunusi alipomhoji Edward Lowassa. Mtangazaji anauliza constructive question na anataka jibu liwe kile anachoamini yeye. BBC ni sawa na TWAWEZA...pumba za mchele, hata nguruwe hali
Mlizoea CUF kumtungia Maalim maswali na yeye kuwatungia majibu? Angalia mahojiani ya Tanzania Daima na Annur na Nipashe na Mtanzanzania.
 
Hivi bado kuna watu wanamwangalia kikeke.
 
Tujiulize kwanza kwanini uchaguzi urudiwe maalimu kama angekubali kurudia uchaguzi maana yake Ingekua amekubaliana na sababu za kufutwa uchaguzi wa awali sasa swali kina baki pale pale kuliku na sababu za msingi za kufuta uchaguzi..na kama uchaguzi haikua wa haki ni chama gani kililalamika hapo awali kabla ya uchaguzi kufutwa!?
Mkuu haya unayoyaeleza mtu yeyote mwenye akili timamu atayaelewa...pale kuna agenda ya siri. Kuna kitu Maalim alikuwa anajaribu kukisema, yule mtangazaji feki akawa anamziba mdomo. CCM walitaka uchaguzi urudiwe ili washindwe tena?
 
Waandishi wa BBC siyo wa Tz Daima, kumpamba mtu.
Ukiulizwa swali usitoe hotuba jibu ndiyo au hapana na sababu zake.

Ningependa kumwona na aidha Shein au Jecha kwenye kikaango kama hiki ajibu maswali yahusuyo uchaguzi wa Zanzibar......nione wao watakuwa na majibu gani eti..
 
Simlaumu Kikeke cose wanapangiwaga cha kuongea /remote control zinajulikana
 
Ningependa kumwona na aidha Shein au Jecha kwenye kikaango kama hiki ajibu maswali yahusuyo uchaguzi wa Zanzibar......nione wao watakuwa na majibu gani eti..
Ni kweli mkuu maana katika kuhukumu jambo ni vizuri ukasikiliza pande zote mbili.
 
Ningependa kumwona na aidha Shein au Jecha kwenye kikaango kama hiki ajibu maswali yahusuyo uchaguzi wa Zanzibar......nione wao watakuwa na majibu gani eti..
Mkuu hila ni kitu kibaya sana. Hao unaowataja wakienda studio, watapewa nafasi ya kuongea kuhusu 'amani' na 'usalama' na kamwe hutasikia sauti juu ya sauti. Kile hakikuwa kikaango cha haki...ni kejeli iliyopangwa.
 
Kikeke alikuwa mjanja hakutaka kumpa nafasi maalim aongee, akaishia kumkatiza na kupiga kelele tu utafikiri mtangazaji wa clouds bana, halafu huu utaratibu wa BBC kualika mgeni na kumpa air time ya Dakika moja ni upuuzi kama hawana muda wa kutosha bora waache tu, dk. mtu ataeleza nini? mnagawana sekunde tu mtangazaji na mgeni, hovyo tu.
 
Back
Top Bottom