KIKAO cha SIRI cha WIZI wa KURA Kalenga

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Wakuu hakuna siri chini ya jua!!!!

(Sitataja wapi kilikalika na nani walihudhiria, bali nitamwaga mikakati tu iliyoadhimiwa)


Intelijensia iliyopandikizwa katika kikao maalumu cha ccm leo jioni kinachotafuta ushindi wa hila Kalenga, imenasa mtiririko wa mikakati hii hapa chini,

1. Karatasi za kupigia kura ambazo zimewasili jana na leo kule Kalenga zimetengwa maalumu kwaajili ya kupewa wajumbe wa nyumba kumi na wanaccm waaminifu kila mmoja karatasi (tupu) kuanzia 10-100,

2. Jumapili wajumbe hao watakwenda kupiga kura huku wakiwa na karatasi hizi mifukoni mwao, wakifika watakabidhiwa vitendea kazi vya kupigia kura kama kawaida, wakifika kwenye chumba maalumu cha kupigia kura, watazitoa sasa zile karatasi na kuzipigia zote upande wa ccm na kuzikunja kwaustadi mkubwa sana kisha kuja kuzitumbukiza kwenye sanduku la kura,

Hapo kila mtu wao atakuwa na uhakika wakupiga kura kumi na kuendelea,

Katika kikao hiki wanajisifu kuwa mbinu hiyo imewaokoa sana kwenye chaguzi za madiwani wiki chache zilizopita,

NB

Tume ya uchaguzi mpaka leo hii haijui idadi halisi ya wapiga kura Kalenga, Lubuva ameanza mawenge anasema tayari wanalo daftari la wapiga kura la 2014 hivyo litatumika hilo badala ya lile la 2005/2010 linalotambuliwa na uuma wote, hebu jiulize ni lini yalifanyika maboresho ya daftari hilo kwa mwaka huu wa 2014?

PENDEKEZO LANGU,

Chadema ihakikishe inawaambia mawakala wao wahakikishe wanakuwa jirani kabisa na sanduku la kupigia kura, na kila anaetumbukiza kura waangalie kwa umakini kama kakunja karatasi mbili au moja?

Ama ikiwezekana kila mpiga kura akaguliwe kwa uangalifu kabla ya kuruhusiwa kwenda kupiga kura.
 
Mawakala wa Chadema wa kusimamia uchaguzi wawe makini sana....Maana mbinu zao zinakwenda kujulikana soon hawa manyang'au..
 
looooh, kumbe hi ndo janja ya nyani kila siku, ila jamani tuache utani ccm ni mafia wa kufa sijapata kuona, tukeshe na kuomba ifike mahali hizi hujuma za nje nje ziishe,na haswa kutumia vyombo vya dola kusulubisha raia ndo inauma kuliko kitu chochote.
 
Hadithi zimeshaanza...

BAVICHA kwa uongo wanamzidi shetani..

Kalenga CDM haiwezi kushinda hata kwa dawa.. naona babu ameshaanza kutuma vilamba kucha wake waje wasafishe upepo baada kugundua wanakwenda kushindwa huko kalenga..

Poleni sana mtasingizia mengi lakini hii ndiyo ishara ya mwisho wenu kwenye siasa za Tanzania..

bye bye CDM rest in hell...
 
mhhhh huna lolote ww taarifa yako imekaa kichimbi chimbi na kinafiki kama kweli unadata na sio maneneo ya vijiweni hayo hembu mwaga kitu hazarani hususani ni wapi kirifanyika na akinanani warilatibu na kuhudhuria kikao hicho.??

acha kutuletea maneno ya umbea mbea hapa au mnaanza kutanguliza mane no ya huruma mbele ili mkiangukia pua mkuje kusema ya kuwa mliibiwa kura?
 
good! kazi kubwa ni kukagua kila anayeingia kupiga kura. sijui kama tume ya uchaguzi inautaratibu huu lakini kwa usalama wapiga kura wote ni vyema wakakaguliwa waingiapo chumba cha kupiga kura. Si kudhibiti wizi tu bali hata usalama wa raia na officers wa usimamizi, ughahidi umefundisha mataifa mengi kufanya ivyo...labda tzn.
 
Hii kitu kweli ipo nakumbuka uchaguzi wa mwaka jana iyela mbeya mtu alikamatwa na karatasi zikiwa zimempigia mgombea wa ccm sijui ile kesi iliishia wapi


Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Hadithi zimeshaanza...

BAVICHA kwa uongo wanamzidi shetani..

Kalenga CDM haiwezi kushinda hata kwa dawa.. naona babu ameshaanza kutuma vilamba kucha wake waje wasafishe upepo baada kugundua wanakwenda kushindwa huko kalenga..

Poleni sana mtasingizia mengi lakini hii ndiyo ishara ya mwisho wenu kwenye siasa za Tanzania..

bye bye CDM rest in hell...

Tulia tuendelee kuwaumbua kweupee manyang'au wakubwa kabisa....
 
Wakala wa CDM afanye haya yafuatayo pia:
1. Baada ya kuhakikisha kuwa sanduku la kura lipo tupu na limefungwa seal, ahakikishe anarekodi namba ya seal
2. Wakala ahakikishe kitabu cha leaflets zina makaratasi 50, na anaandika namba ya kitabu walichoanza kuitumia, yaani leaflet ya kwanza hadi ya mwisho, inayofuaya vile vile.
3. Kabla ya kuhesabu kura wakala wa chadema ahakikishe ana idadi ya karatasi za kura zilizotumika, baada ya hapo sanduku lifunguliwe kuhakikisha idadi ya kura zilizopo kwenye sanduku ni sawa na kura zilizopigwa. Akiona idadi ni tofauti na kura zilizopigwa basi waanze kuhakiko namba ya karatasi ya kura kuanzia moja hadi nyingine ili kubaini kura zilizozidi.
 
Back
Top Bottom