Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,861
Tumepata shuhuda mbalimbali za namna ambayo wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali hutokea. Wengine wakisema Maboksi ya kura zilizopigwa tayari uingizwa kwenye vyumba vya kupigia kura kisiri ambapo hutokea endapo waangalizi wa vyama vingine wakiwa hawapo au wametengenezewa zengwe mfano kuambiwa hawana vitambulisho sahihi, hawajavaa vizuri na zengwe la kila aina ilimradi waondoke hili kura ziingizwe.
Na shauri CCTV camera ziwe zinafungwa kwenye vyumba hivi vya kupigia kura nchi nzima ili endapo kuna kasoro basi inakuwa rahisi kwenda kutizama CCTV na kujua nini kimetokea. Hii itasaidia kuondokana na shida ya uangalizi endapo msimamizi atakuwa kashindwa kusimamia vizuri. Mfano Boksi za kura zikiletwa basi inakuwa rahisi kuzifuatilia pia kupitia CCTV kamera endapo zimeongezwa