KIKAO cha SIRI cha WIZI wa KURA Kalenga

KIKAO cha SIRI cha WIZI wa KURA Kalenga

Chadema nimpango wa Mungu mtaumbuka mchana kweupe yale ya Arusha yanaenda Kalenga..... Tumeanza na Mungu tupo na Mungu natunamaliza na Mungu
 
mhhhh huna lolote ww taarifa yako imekaa kichimbi chimbi na kinafiki kama kweli unadata na sio maneneo ya vijiweni hayo hembu mwaga kitu hazarani hususani ni wapi kirifanyika na akinanani warilatibu na kuhudhuria kikao hicho.??

acha kutuletea maneno ya umbea mbea hapa au mnaanza kutanguliza mane no ya huruma mbele ili mkiangukia pua mkuje kusema ya kuwa mliibiwa kura?

Tulia dada ukunwe...Hapa ni nondo juu ya nondo.....Mikakati ya kishetani inazidi wekwa hadharani...

Chadema mpango wa Mungu..
 
hawa maccm hawana mbinu mpya kazi yao ni kubuni mbinu chafu tu za kushinda chaguzi mbali mbali, kuua au kutesa pamoja na mapuuzi mengine, ila mwisho unatimia.
 
Yericko kalenga hata mkiroga mtashindwa vibaya sana ngoja muone moto wake.
 
cdm Kalenga wapeni taarifa hii tume ya taifa. Hakikisha kila anayeingia chumba cha kupiga kura anakaguliwa hadi kwapani, ukiona wanakataa ujui hiyo mission wamepanga nao. Mkibahatika kumkamata mmoja mpe adhabu itakayowapa fubdisho hata makada wengine ovyo kama hao. nchi hiko hivi kwa upuuzi huu wa mda mlefu.
 
hawa maccm hawana mbinu mpya kazi yao ni kubuni mbinu chafu tu za kushinda chaguzi mbali mbali, kuua au kutesa pamoja na mapuuzi mengine, ila mwisho unatimia.
Gongo zinawasumbua vijana poleni sana chadema mshapagawa sana tu.
 
mbona ni rahisi kinachotakiwa ni kujua wapiga kura waliojiandikisha na wapiga kura waliojitokeza siku husika kama kura zitakuwa nyingi kuliko idadi ya wapiga kura itabidi wajieleze kura zaidi zimetoka wake lakini muhimu mawakala kuwa makini
 
Sidhani kama kuna ukweli kwenye hiyo mbinu, wakati huyo mjumbe wa nyumba kumi akikunja hizo karatasi zaidi ya kumi "kiustadi" makamanda wa CHADEMA ambao ni mawakala wao wanakuwa wapi wasione?
 
Yericko haya unayosema unataka kweli tuyaamini? Kila kituo kina idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa daftari la kudumu. Je hizo kura za ziada zitahesabika vipi? Vinginevyo wawe pia na orodha ya watu watakaoshindwa kutokea kupiga kura!
 
Hahahahahhahahahah chadema mumeshaanza kutafuta sababu hahahahahh:sly::sly::sly:
Mpo dorooooooo wananchi wamewatupa haahhaahbaba
 
Wakuu hakuna siri chini ya jua!!!!

(Sitataja wapi kilikalika na nani walihudhiria, bali nitamwaga mikakati tu iliyoadhimiwa)


Intelijensia iliyopandikizwa katika kikao maalumu cha ccm leo jioni kinachotafuta ushindi wa hila Kalenga, imenasa mtiririko wa mikakati hii hapa chini,

1. Karatasi za kupigia kura ambazo zimewasili jana na leo kule Kalenga zimetengwa maalumu kwaajili ya kupewa wajumbe wa nyumba kumi na wanaccm waaminifu kila mmoja karatasi (tupu) kuanzia 10-100,

2. Jumapili wajumbe hao watakwenda kupiga kura huku wakiwa na karatasi hizi mifukoni mwao, wakifika watakabidhiwa vitendea kazi vya kupigia kura kama kawaida, wakifika kwenye chumba maalumu cha kupigia kura, watazitoa sasa zile karatasi na kuzipigia zote upande wa ccm na kuzikunja kwaustadi mkubwa sana kisha kuja kuzitumbukiza kwenye sanduku la kura,

Hapo kila mtu wao atakuwa na uhakika wakupiga kura kumi na kuendelea,

Katika kikao hiki wanajisifu kuwa mbinu hiyo imewaokoa sana kwenye chaguzi za madiwani wiki chache zilizopita,


PENDEKEZO LANGU,

Chadema ihakikishe inawaambia mawakala wao wahakikishe wanakuwa jirani kabisa na sanduku la kupigia kura, na kila anaetumbukiza kura waangalie kwa umakini kama kakunja karatasi mbili au moja?

Ama ikiwezekana kila mpiga kura akaguliwe kwa uangalifu kabla ya kuruhusiwa kwenda kupiga kura.

Itakula kwao, mawakala ni wabunge wa chadema na madiwani .
 
Sidhani kama kuna ukweli kwenye hiyo mbinu, wakati huyo mjumbe wa nyumba kumi akikunja hizo karatasi zaidi ya kumi "kiustadi" makamanda wa CHADEMA ambao ni mawakala wao wanakuwa wapi wasione?

Hiyo ni mbinu kati ya mbinu nyingi mnazotumia kuibia kura.....

Tutazidi kuziweka mbinu zingine hapa jukwaani....Stay tuned..
Tutawaumbua mpaka mshangae..
 
Yericko haya unayosema unataka kweli tuyaamini? Kila kituo kina idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa daftari la kudumu. Je hizo kura za ziada zitahesabika vipi? Vinginevyo wawe pia na orodha ya watu watakaoshindwa kutokea kupiga kura!

Mkuu,

Hukusikia 2010 kura zilikuwa nyingi zaidi ya wapiga kura baadhi ya vituo? Siri hii ya wizi massm walishaiuza hata kenya na zimbabwe. This time around they won't make it!
 
Porojo za kuibiwa kura safari hii zimeanza mapema mno.

Unajua maana ya Intelijensia makini ya Chadema...????

Tulia hivyo hivyo....Hizi ni habari za kiintelijensia.....Kilaza kama wewe ni ngumu kuelewa..
 
Back
Top Bottom