SoC03 Sanduku Maalumu la kupigia kura(Magic BALLOT BOX)-MB2

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
996
1,511
UTANGULIZI

MB2 ni kifupisho cha “MAGIC BALLOT BOX”, ni sanduku maalumu la kupigia kura ambalo litakuwa na sifa za kipekee ambazo zimelenga kuzuia udanganyifu katika zoezi zima la kupiga kura na kuhesabu kura.

Dhana ya uwajibikaji na utawala bora inategeme pia namna ambavyo viongozi wanapatikana, kama viongozi walipatikana kwa udanganyifu inakuwa ngumu kwa wao kuwa na nidhamu na kuzingatia miiko ya uongozi na utawala bora, inaathiri pia uwajibikaji kwa viongozi husika, hasa viongozi wa juu wa serikali ambao hupatikana kupitia sanduku la kura tena lakini kwa udanganyifu.

MUUNDO WA MB2

MB2
litakuwa ni sanduku maalumu kwa ajili ya kupigia kura ambalo litaongozwa kwa mfumo maalumu na halitaweza kuruhusu udanganyifu wa aina yoyote, litaundwa kwa plastiki nzito ambayo ni angavu, litakuwa na kioo kitakachoonesha idadi ya karatasi zilizopo ndani ya sanduku ambazo namba itabadirika kila karatasi inapo ingia, pia kitatumika kuonesha taarifa nyingine muhimu, litakuwa na mdomo wa kuingizia karatasi ambao pembezoni mwa mdomo huo kutakuwa na sensa maalumu kwa ajili ya kutambua karatasi ya kupigia kura ambayo itatengenezwa maalumu kwa ajili ya aina ile ya sanduku, mdomo hautaweza kujifungua na kuvuta karatasi mpaka pale sensa itakapo hakiki karatasi na kuthibitisha kuwa ni sahihi, litakuwa na kivuta karatasi ambacho kitafanya kazi ya kuvuta karatasi baada ya kuhakikiwa na sensa, baada ya karatasi kutumbukia mdomo utajifunga kwa ajili ya kuendelea na zoezi na idadi ya karatasi zilizopo ndani ya sanduku itabadilika mara tu karatasi kuzama.

Sanduku litakuwa na loki maalumu ambayo itafunguliwa kwa kuthibitisha na alama za kidole za karani mkuu kupitia mfumo katika kishikwambi chake katika kituo husika ambaye atakuwa amesajiliwa na Tume ya uchaguzi katika mfumo.

Sanduku litaongozwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kielekroniki ambacho kitafanana na kishikwambi ambacho kitakuwa na mfumo ongozi wa sanduku hilo na uchaguzi kwa ujumla, kishikwambi hicho kitaweza kufanya kazi katika kituo chochote, kupitia kifaa hicho ataweza pia kuona namna sanduku linafanya kazi, na idadi ya karatasi za kura zilizopo ndani.

Wapiga kura watakuwa na kadi maalumu za kielekroniki za kuthibitisha kama wamesajiliwa katika daftari la kudumu la kupiga kura, kadi hii itatambuliwa na kifaa maalumu baada ya kuiswap kadi katika kifaa hicho na kuonesha taarifa zote muhimu, faida ya kutumia kadi hii ni kwamba mtu ataweza kupiga kura kituo chochote kile hususani kwa watu watakao kuwepo mikoa tofauti na kule waliko jiandikisha, karatasi maalumu ya kupigia kura kwa watu walio nje ya vituo vyao vya kupigia kura (Nimeelezea hapo chini namna kura zao zitatambulika katika vituo vyao sahihi).

UTENDAJI KAZI WA SANDUKU.


Tume ya uchaguzi itayatambua masanduku yote kupitia Msimbo baa, ambayo itasajiliwa kupitia mfumo maalumu kwa ajili ya vifaa husika, makarani wote watasajiliwa kupitia mfumo huo ambapo karani mkuu atakuwa na mamlaka kisheria kuongoza mfumo katika kituo cha kupigia kura, kila kituo kitakuwa na kishikwambi maalumu kimoja na idadi ya masanduku ya kupigia kura kulingana na idadi ya wapiga kura walio jiandikisha katika kata husika.

Kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza Karani mkuu atafungua mfumo wa kupigia kura kulingana na mafunzo aliyopea na kuhakiki masanduku yote yaliyopo kupitia msimbo baa moja baada ya jingine na kufanya majaribio kama mifumo ya masanduku yote ipo tayari kwa kazi kwa kupitia kitufe cha mpangilio katika mfumo uliopo katika kishikwambi chake.

kama kila kitu kipo sawa mfumo utamtaka athibitishe kwa kupitia alama za vidole kwa kuweka dole gumba lake katika kitufu kitakachokuwepo katika kishikwambi hicho maalumu kwa ajili ya kuhisi alama za vidole endapo kitaguswa na ambacho pia kitatumika kama kifufe nyumbani.

Wakati huo masanduku yote vioo vyake vya kutolea taarifa vitakuwa vinasoma kura sifuri na ndani hakuna karatasi yeyote.

Mpigakura ataelekezwa namna ya kupiga kura katika karatasi, na namna ya kuikunja, kutakuwa na namna bora ya kuikunja karatasi na kuiweka katika mdomo wa sanduku ili sensa iweze kuitambua kama ni rasmi, kazi ya wasimamizi wa uchaguzi katika kituo itakuwa ni kuwaongoza wapigakura.

Mpiga kura baada ya kuchagua wagombea wake na kuikunja karatasi yake vile inavyotakiwa na kwenda kuiweka katika mdomo wa sanduku, (ikumbukwe sensa za sanduku zitakuwa na uwezo wa hali ya juu ili kuharakisha zoezi), kama karatasi limewekwa tofauti kioo cha kitaonesha nambari ya kosa mfano: :1 yenye maana ERROR 2, utakao ambatana na sauti, msimamizi atasogea kwa msaada na kuisoma kwa ajili ya masahihisho ambapo sanduku litakuwa na uwezo wakujirekebisha na kuendelea na zoezi, endapo sensa itathibitisha kuwa karatasi ni sahihi basi mdomo wa sanduku utafunguka na kivuta karatasi na kulimeza kisha namba itabadilika katika kioo, karatasi ya kupigi kura itakuwa na ufito wenye msimbo maalumu katika upande mmoja kwa kingo wima wake kuanzia juu mpaka chini ndio huoo sensa itatumika kuthibitisha uhalisia wa karatasi, Zoezi litaendelea hivyo mpaka dakika ya mwisho, ikitokea karatasi ni feki basi kioo kitaandika “The ballot paper isn’t genuine”,

Wakati sensa ya sanduku inalisoma karatasi kulitambua pia itakuwa inatambua msimbo uliopo katika ufito huo na kwa wakati huo mfumo utakuwa ukirekodi taarifa zote.

Karatasi watakazo tumia wapigakura nje ya vituo mahususi hazitakuwa na picha za wagombea isipokuwa zitakuwa na sehemu ya kujaza majina ya wagombea kwa kufuata picha za alama za vyama vyao ambazozitakuwepo katika karatasi hiyo, baada ya kuijaza karatasi hiyo karani mkuu atamsajili mpiga kura huyo kwa kupitia kishikwambi chake na kuiskani msimbo baa wa karatasi kisha atampa karatasi akapige kura.

NAMNA KURA ZITAHESABIWA.

Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika karani mkuu atafungua sanduku moja moja kwa kutumia mfumo, kisha karatasi zitachambuliwa, kwa majina ya wagombea na nafasi zao na kupangwa, karani mkuu ataziskani karatasi kwa kuzingatia majina ya wagombea, ambapo kila anapo skani mfumo utakuwa una hesabu, kwa kila mgombea, na mwisho idadi ya karatasi zilizosomwa na sanduku iwe sawa na idadi ya kura jumuishi, itafanyika hivyo kwa masanduku yote.

Kwa kura ambazo zimepigwa nje ya kata husika zitaonekana kwa karani ambaye mpiga kura alisajiliwa kupiga kura katika kituo hicho kupitia karani mkuu huko alipo (akiswap kadi tu taarifa zitakazoonekana zitahusisha na vituo vya kupigia kura hivyo karani mkuu atamuuliza mpiga kura kituo chake), baada ya kumaliza masanduku yote katika kituo husika karani mkuu ataangalia kura jumuishi kwa kila mgombea na nafasi yake kupitia mfumo kwenye kishikwambi chake na hayo ndio matokeo yatakayo jazwa kwenye fomu za kubandika ubaoni, matokeo hayo yatakuwa yanaonekana kituo kikuu cha kuhesabia kura kitaifa.

Kura za urais zitaonekamna pia moja kwa moja kupitia mfumo kwa kila jimbo na jumla kuu.
 
Africa hakuna kinachoshindikana Yani hayo masanduku yanaweza kuwepo na Ushindi wa kishindo ukabaki pale pale Trust Me. Anyway Andiko ni zuri nimekupa Kura Yangu
 
Africa hakuna kinachoshindikana Yani hayo masanduku yanaweza kuwepo na Ushindi wa kishindo ukabaki pale pale Trust Me. Anyway Andiko ni zuri nimekupa Kura Yangu
Ahsante kwa kura yako ndugu,lakini kama Afrika inajinadi kupiga hatua kiuchumi,basi viongozi hawanabudi kuwajibika kukubaliana na mabadiriko ili twende na matakwa ya utawala bora,mwenye akili atachagua jema,mpumbavu ata chagua upumbavu.
 
Back
Top Bottom