Wakati akihojiwa na Mtangazaji wa Azam TV, Haji Bwegege kwenye ofisi za NCCR-Mageuzi, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesikika akisema picha zilizoenea kwenye mitandao ambazo zinawaonyesha viongozi wa CHADEMA na Edward Lowassa siyo halisi na zimetengenezwa (photoshop)
Haya ndiyo mahojiano kati yake na mtangazaji wa Azam TV,
Hizi ndizo picha zinazodaiwa kugushiwa(photoshop)
ANGALIZO:
Kwa kuziangalia tu hizi picha huwezi hata kutumia utaalam kufahamu kama niza kweli.
Kwa nini wanasiasa wetu wanakuwa siyo wakweli?
Our politicians lie through their teeth!
Labda tujiulize maswali machache,
a) Nani alizipiga hizi picha?
b) Kwa nini alizipiga na kuzivujicha bila ruhusa ya wahusika?
c) Kwa nini Mbowe anazikana?
d) Nini kilichoko nyuma ya pazia?