Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

hapo kufuri atapiga kura ambozo haijawahi tokea hapa bongo wachaga wameamua kutuona watanzania ni mazuzu sana Zitto alisema chadema ni cha wachaga tukabisha

mda wote huo slaa anapambwa kua rais dakika za mwisho anakatwa kwa pesa acha tuuu wapigwe hakuna namna.

Lowassa mchaga? unatumia kiungo gani kufikiria?
 
Lowassa akihudhuria kikao Kamati kuu CHADEMA

View attachment 271482
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa, akisalimiana na viongozi na wanachama wa CHADEMA

View attachment 271483
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa akiwa Meza Kuu na viogozi wa CHADEMA
Mbowe: Mazungumzo yameshafanywa hivyo hawezi kuongea na amesema kuhusu picha za Lowassa kuwa kwenye kikao cha CHADEMA zimetengenezwa.
 
Muda ni hakimu Mzuri kila mmoja wetu apitie kwa umakini andiko hili hapa chini



IMEGUNDULIKA kwamba Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) ndiye mfadhili mkuu na mpanga mikakati mkuu wa kundi linalomfuata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambalo limeanzisha chama kipya cha siasa, Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).

Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, makundi ya wanachama, washauri na wapanga mikakati wa Lowassa na Zitto wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam na kupeana mbinu, lengo kuu likiwa ni jinsi ya kumega Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mapande ili kidhoofike kabla ya uchaguzi mkuu 2015.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Lowassa amejiaminisha kwamba ndiye atakayekuwa mgombea urais kupitia CCM. Kazi kubwa anayoona mbele yake ni kuanza mapema kusambaratisha CHADEMA ili kupunguza upinzani wakati wa kampeni utakapofika.

Zitto naye, ambaye uanachama wake kwa CHADEMA umebaki kwenye makaratasi tu, anatajwa kuwa ndiye mwasisi mwenza wa ACT, na amekuwa na uhusiano wa “kikazi” na Lowassa, hata kabla hajaingia kwenye matata ya wazi na chama chake, ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilimvua vyeo vyake vyote vya uteuzi ndani ya CHADEMA kwa tuhuma mbalimbali.

Katika hatua mojawapo, chanzo kimoja kilicho karibu na Lowassa kimesema kwamba mapema mwaka juzi, Zitto alimwendea Lowassa na kumwambia kuwa mustakabali wake kisiasa ndani ya CHADEMA si mzuri, na kwamba alikuwa tayari kumsaidia Lowassa kufanikisha malengo yake, lakini kwa sharti kwamba iwapo mbunge huyo wa Monduli atafanikiwa kupata urais, basi amteue kuwa Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kauli hiyo kwanza ilimstua Lowassa kwa sababu ilimuonesha Zitto kama kiongozi asiye mwaminifu, ambaye yupo tayari kufanya hujuma dhidi ya chama chake, jambo ambalo lilimfanya Lowassa atilie shaka lengo la ombi hilo.

Jambo la pili lililomshtua Lowassa ni cheo kilichopendekezwa na Zitto, maana kwa mujibu wa Katiba ya sasa, Waziri Mkuu lazima atokane na wabunge wa majimbo, na awe kwenye chama chenye wabunge wengi.

Kwa kuwa hoja hiyo ilitolewa katika mazingira ya Katiba ya sasa, na kwa kuwa haikujulikana wakati ule kama Zitto alikuwa bado ni mwanachama na kiongozi wa CHADEMA, Lowassa hakuipata nafasi kauli hiyo, lakini amekuwa anaitumia kujadili sura halisi ya Zitto.

Hata hivyo, taarifa zinasema uhusiano wao umeimarika baada ya Zitto kuchukuliwa hatua na CHADEMA, huku wapambe wa Lowassa wakipita huku na kule kusambaza propaganda kuwa CHADEMA bila Zitto inakufa.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Zitto anatarajiwa kujiunga rasmi na ACT mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, na timu ya Lowassa imedhamiria kumfadhili ili kujenga taswira ya mpasuko ndani ya CHADEMA, na kuipa CHADEMA mpinzani mpya ambaye ataifanya ishindwe kumfuatilia na kumshambulia Lowassa.

Katika kikao cha mwisho kilichofanyika kati ya timu ya Lowassa na “Vijana wa Zitto” kilijumuisha baadhi ya wapambe wakuu wa Lowassa wenye kauli ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM, watu wa karibu kifamilia na Lowassa na washauri wa karibu wa Zitto, akiwamo Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ajenda zao nje nje

Moja ya ajenda zao kuu ni kufadhili na kupandikiza watu ndani ya mfumo wa CHADEMA ambacho kinaendelea na uchaguzi wa ndani, ili wapate nafasi za uongozi, wazitumie kupata taarifa na mipango ya chama, na baadaye wajivue nafasi hizo na kukimbilia ACT, na kuleta msisimko wa kitaifa.

Gazeti hili lina taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa CHADEMA ambao “Vijana wa Zitto” wamekuwa wakiwapigia simu na wakati mwingine kuwatembelea na kuwashawishi ahadi ya fedha na vyeo ili wajiondoe CHADEMA.

Baadhi hao ni viongozi wa majimbo na mikoa ambao katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hawana uhakika wa kuchaguliwa kutokana na upinzani mkubwa unaojitokeza baada ya chama kukua na kuvutia wasomi na wafanyabaishara wenye mvuto katika maneo yao.

Baadhi ya viongozi walioendewa au kupigwa simu wamechukua tahadhari, na wametoa taarifa panapohusika ndani na nje ya chama.

Mbinu mojawapo ambayo imekuwa inatumiwa na “Vijana wa Zitto” kujaribu kuvunja ngome za CHADEMA ni kuwatangazia viongozi hao kwamba ipo idadi kubwa ya wabunge wa CHADEMA wanaotarajia kujiunga na ACT. Wanawataja majina kama njia ya kujenga ushawishi.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi hao wameliambia gazeti hili kuwa wanajua hizo ni mbinu za kipropaganda. Na baadhi ya wabunge wanaotajwa wamesema hizo ni mbinu za Zitto kutaka kuwagombanisha na chama chao na kujitafutia njia mpya kwa kutumia majina yao.

Mmoja wao alisema, “Zitto mwenyewe ameshalikoroga. Sasa hii ni tabia ya kututaja baadhi yetu, mimi na wenzangu kadhaa tumeshasikia, ni ile ile roho mbaya ya tukose wote. Kwa kuwa yeye amekosana na chama, anatafuta watu wa kufa naye.”

Mbali na kupandikiza wagombea nafasi za uongozi na kuvizia viongozi wanaoogopa joto la uchaguzi ndani ya chama, wamekuwa pia na mbinu ya kushawishi baadhi ya “wagombea watarajiwa” katika baadhi ya majimbo, wanaotajwa kuweka nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia CHADEMA.

Makada kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamezungumza na gazeti hili na kutumia kauli zijazofanana. Kwa mfano, makada sita walioweka nia ya kugombea ubunge katika majimbo kadhaa ya kanda ya Ziwa Mashariki na Magharibi, wamekiri kwamba kila wanapojadili mkakati huu na “Vijana wa Zitto,” kila mmoja wa nafasi yake anapewa ahadi ya kupewa pesa zote za kufanyia kampeni.

Vile vile, baadhi yao wamesema kuwa wanaambiwa kwamba iwapo watakubaliana na mpango huo wa ACT, moja kwa moja watakuwa wamepitishwa, maana chama hicho hakina mpango wa kupata wagombea kwa kutumia kura za maoni.

Taarifa zinasema sehemu ya malengo ya vikao ya Zitto na Lowassa ni kutafuta pesa kwa ajili ya mradi huu.

Zipo taarifa zisizothibitishwa kwamba mwezi uliopita Lowassa aliambatana na Zitto katika ziara ya kimya kimya ya Mkoa mmoja wa kanda ya Ziwa ambako anasemekana anataka kujenga ngome nzito ya ACT.

“Ninachojua ni kwamba iwapo ACT itafanikiwa kupunguza makali ya CHADEMA, Mzee atapita kirahisi, maana kikwazo kikubwa alichonacho hadi sasa hakipo ndani ya CCM, bali CHADEMA,” alisema mtoa taarifa wetu aliye karibu na Lowassa, ambaye hakutaka kuthibitisha kama wawili hao walisafiri pamoja kwenda Kanda ya Ziwa

Chanzo: Tanzania Daima
 
Chiwa are you serious

Unaongelea 2025....unaona hali ya uchumi wa nchi yetu ulivyo sasa?

CCM has to go NOW.......Hakuna muda wa kusubiri

Sometimes ni bora kuharibu mfumo uliopo na kuanza kuijenga nchi upya...hAKuna haja ya kusubiri subiri

Sikia ndugu yangu....Viongozi waliopita ni binadamu...sio Miungu...wana madhambi yao pia....na ni hao hao walioifikisha nchi yetu katika hali hii mbaya.

Kwa hio hata wanapotoa maoni yao wanaangalia nani atawalinda

Lowasa ni mtu ambaye hua hana compromise na Ujinga

Tuepuke kuangalia mtu mmoja mmoja...Adui yetu ni CCM

Ni kweli mkuu adui namba moja ni ccm ila na hawa ni maadui
Nape_ mzee wa goli la mkono
Makonda_alimpiga warioba
Riz aka mwanamfalme_ alisema raisi hatoki kaskazini
 
Last edited by a moderator:
Mkuu inauma sana, tena sana... Hii ni aibu kwa kila mpenda Demokrasia na mchukia ufisadi.

Upinzani wa Tanzania utaficha wapi sura yake.?

Before you assume; learn the facts
Before you judge;😇 understand why
Before you hurt someone; feel😞
Before you speak; think
Stay consistent.😁
 
Lowassa akihudhuria kikao Kamati kuu CHADEMA

View attachment 271482
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa, akisalimiana na viongozi na wanachama wa CHADEMA

View attachment 271483
Waziri Mkuu Mstaafu wa JMT Mh. Edward Ngoyai Lowassa akiwa Meza Kuu na viogozi wa CHADEMA

Narudia tena hizi picha ni za kuchongwa.Maccm yanatapatapa kama kuku aliyekatwa kichwa.
 
Mkuu Mudawote sio fununu... ni kweli wewe na mwenza wako ni watanzania. So fununu zako ni kweli. Ninachoweza kuwashauri watanzania wa namna yako ni kuwa kabla ya kujiita kamanda ulipaswa kujua unapambana na nini.... Mtu au mfumo? Pia ulipaswa ujue hali ngumu waliyonayo watanzania imetokana na mtu au mfumo? Na ulipaswa ujiulize kwa nini ulikuwa hum-support Magufuli? Ni mtu asiyefaa?? Nope! Ni mtu anayefaa aliye katika mfumo usiofaa. Adui sio mtu! Ni mfumo.... ni sisiemu!

Kama kweli ni kamanda sitegemei kukupoteza ktk wakt huu muhimu!

Lowassa ni mwizi. Sina maelezo zaidi, tukutane 2015. Ni lazima UKAWA waangukie pua! Hakuna system itakayoruhusu mtu aliyenunuliwa kuingia ikulu. Angekuwa Lipumba au Slaa au Lissu OK. CDM mpaka sasa wapo chini kabisa, siwapi kura yangu. Nitampatia mbunge wangu wa CHADEMA ila rais ni Dr. John Pombe Magufuli!
 
Daaah, chama kineuzwa rasmi ..I can't just believe it, daaah, Mbowe katiwa mfukoni, Mbowe umetusaliti daima hatutakusahau.. kwahiyo majizi yoote yanahamia Ukawa rasmi, inauma sana na itabidi tukuhadhibu Mbowe ..hiyo 10bn utailipaje?
 
Kumpokea yeyote hata Lucifer ni kuonyesha chama hakina agenda, hakina manifesto ya kuwashawishi wapiga kura wakichague kiwaongoze. Shame on CHADEMA kama hii ni kweli.
2 hell with u!! Mission is vry clear!! "Delete CCM by all means" ambacho huelewi hapa kitu gani!!?
 
Lowassa ni mwizi. Sina maelezo zaidi, tukutane 2015. Ni lazima UKAWA waangukie pua! Hakuna system itakayoruhusu mtu aliyenunuliwa kuingia ikulu. Angekuwa Lipumba au Slaa au Lissu OK. CDM mpaka sasa wapo chini kabisa, siwapi kura yangu. Nitampatia mbunge wangu wa CHADEMA ila rais ni Dr. John Pombe Magufuli!

Before you assume; learn the facts
Before you judge;😇 understand why
Before you hurt someone; feel😞
Before you speak; think
Stay consistent.😁
 
Je ataitetea Katiba ya Wananchi aliyoikataa na rafiki yake Chenge akiwa CCM?
 
mfumo uliopo Tanzania ambao unasababisha maendeleo kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa ndo hasa watanzania tunatakiwa kuuangalia na kuupinga kwa nguvu zote, ila kum attack mtu haitasaidia.
 
CDM wasije wakasema hatukuwaonya.Hii ni hatari.Huwezi ukawa chama kinachodai kinasimamia uadilifu na uzalendo ukamchukua fisadi kama huyu Lowasa.Mimi sitakuwa sehemu ya uchafu huu.

Pole usijali sana vipo vyamat visafi vyenye uadilifu kama CCM au ACT nadhani watawafanyia sherehe mkienda, si tunakomaa na CHADEMA yetu na fisadi wetu wa zamani walau hali jadi sisi siku za karibuni, miaka minane walikuwa benchi
 
Ccm hamuwezi kutoa ushauri cdm ili kisonge mbele, tulieni kimbuga kinakuja

kweli bana hatudanganyiiiki!!! huwezi kuwadanganya kwa mbinu zilezile watu wote na mara zote. Watu waliaminishwa kuwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete ni marais tofauti, lakini wananchi wanazidi kugundua kuwa hawako tofauti kwa kigezo cha unafuu wa maisha yao, matumizi ya kodi zao, wizi wa mali zao na upatikanaji wa huduma zao, hivyo wachache pia wataamini kuwa Magufuli atakuwa tofauti na watangulizi wake wa kutoka CCM. Kumbe kigezo sio mtu bali chama chake
 
Back
Top Bottom