Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

kwa na hilo mnalolipitisha kung'ang'ania urais eti hata kama ni kwa siku 2, si ni LICCM sasa nani anayejambajamba hapa kama sio huyo aliyeiuza chadema kwa bil.10 ! Cc: Lizaboni ,

Mafuriko ya bwana mamvi yataicha ccm vipande vipande, cdm hatuna tatizo na lowasa tatizo letu ni mfumo wa ccm ndo unaodumaza maendeleo yeyote mwenye nia ya dhati kulitokomeza hili liccm tutamuunga mkono hata kama ni shetani.
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli CHADEMA kwisha kazi. Wamejipeleka kaburini huku wakiona na kutizama. Inatia huruma kwa Watanzania waliokuwa na matumaini kwa chama chao cha CHADEMA. Watakimbilia wapi??? Sitashangaa wakirudi kwa CCM ambao wameonyesha kuanza vita dhidi ya ufisadi kwa kumuengua Lowasa kwenye kugombea urais wa nchi.

Nyie mtulie tu ccm mwaka huu mshalikoroga mnapata kiwewe sasa
 
ni maajabu sana huku mitaani. Kila mtu anashangilia jambo hili, nimepita mkutano mmoja wa ccm kura za maoni eti nao wanashangilia lowasa kugombea ukawa. Kweli ccm itabaki?
Duh! Huu sasa ni uzandiki wa hali ya juu. Anyway sanduku la kura litaamua
 
Nini Kamanda Edward Lowassa; hata aje Shetani Mkuu, Lucifer, as long as the strategy ni kuiondoa CCM, Chadema au chama kingine chochote kimpe support. Say no to CCM by all means.

This perception is totaly WRONG. lengo ni kuiondoa CCM ama kuikomboa Tanzania toka mikono ya WACHAFU, WALAFI, MAFISADI, WAFIA TUMBO???

Labda kama Lowasa anaingia CDM kama mwanachama wa kawaida na siyo kama mgombea uraisi.
 
Inapotokea popote duniani, kiongozi maarufu kuliko wote katika chama tawala (CCM) akaamua kujiunga na chama maarufu kuliko vyote katika upinzani matokeo yake ni neema kubwa kwa taifa - a golden chance for the nation. Kielelezo cha umaarufu wa Lowasa ndani ya CCM mbali ya mikusanyiko mikubwa ya wananchi kwenye mikutano yake, ni hatua ya CCM kukiuka misingi ya demokrasia kwa kutumia "kitengo" kukata jina lake mapema hivi majuzi ili asipate fursa ya kuwania urais wa nchi. Baadhi ya watu, kwa kuegemea propaganda za kisiasa na tuhuma za ufisadi (unconfirmed) dhidi ya Lowasa, watadhani CHADEMA wamekosea - la hasha! Lowasa kwa kushirikiana na CHADEMA wana fursa ya kipekee kuliko CCM kuweka mifumo mipya, wazi na madhubuti kudhibiti ufisadi na kusukuma maendeleo ya nchi mbele kwa kuchanganya yaliyo mema pande zote mbili - adopt the best STRENGTHS on both sides and discard the WEAKNESSES!

Hatua ya kwanza ni kuandaa katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais na kuimarisha taasisi za utawala (intitutions of good governance) na kupeleka madaraka zaidi kwa wananchi. CCM ni chama cha status quo na kulindana kama tulivyoona katika zoezi la kihistoria la kuandika katiba mpya - hawawezi kuleta mabadiriko. Kwa upande wa CHADEMA yabidi waimarishe uwajibikaji kwa kutumia raslimali za Chama vizuri na kwa uwazi na kuimarisha demokrasia ya ndani -Wasipuuze kukosolewa.

Kwahiyo wana CHADEMA na watanzania wote tusipanic wala kuhofia ujio wa Lowasa CHADEMA- kiongozi huyu kapitia tanuru la joto kali na ndiye anayetufaa kwa kupitia chama chenye uchungu na maendeleo ya watanzania - wanasema "the finest steel must go through the hotest fire".

Let us all embrace this golden chance for the first real change in Tanzania since the Arusha Declaration. God bless Tanzania. God Bless Africa.
 
Picha tuu inakataa , jamani Jaman ukawa mmekosa mgombea msisafirie nyota ya lowasa
 
Acha pesa iitwe pesa.Lowassa ndani ya mwezi mmoja amekaribishwa mpaka chumbani.makada wamepigwa na butwaa. Mtei na Mbowe deal done !!!
 
Sote tunakumbuka kuwa kwenye ile list of shame ya slaa ya watu 11 Lowassa alikuwa mmojawapo.

Leo hii Slaa itabidi aanze kwanza kumtoa kwenye ile list na kuwabakiza 10. Kwamba nilikosea kumtaja Lowassa, kwani majina niliyoletea na vijana wangu yalikuwa 10 shetani akaongezea na la Lowassa, ashindwe na alegee kabisa, hahaaaaa!

Ndugu wananchi nawahakikishia Lowassa ni kamanda na mtu msafi kabisa kuliko mnavyofikiria.

Pipoooooooooooooooz!!! Pawaaaaaaaaaaaaaaaa.
Ramli chonganishi hii! Kwani CCM waliposhindwa kuwavua magamba walitoa sababu gani? Kwanini CCM hawakumfikisha mahakamani mhusika kama walivyomfunga Mramba na mwenzake?
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Hupati Picha ?. Rekebisha camera yako. Sogea karibu na muhusika. Ukishindwa hayo hapo juu. Muone michuzi
 
ni maajabu sana huku mitaani. Kila mtu anashangilia jambo hili, nimepita mkutano mmoja wa ccm kura za maoni eti nao wanashangilia lowasa kugombea ukawa. Kweli ccm itabaki?

Mkuu nakwambia hapa nilipo (Kariakoo) kuna shangwe ya ajabu sijapata kuona, watu wanashangilia vibaya sana. Sasa ukombozi ndio umefika rasmi....

Kwenye vituo vya kujiandikishia ndio usisema watu wanafurahi balaa hasa vijana...
 
Back
Top Bottom