Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Wadau amani iwe kwenu.

Kikao cha Kamati Kuu cha dharura cha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilifanyika jana Kunduchi Beach Hotel kuanzia saa mbili hadi saa tisa usiku. Jumla ya wajumbe 36 walihudhuria kikao hicho akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dr Wilbroad Slaa nk. Aidha, Edward Lowasa alihudhuria kama mwalikwa ambapo aligharamia mkutano huo ikiwa ni pamoja na gharama za ukumbi, chakula, nauli na posho za wajumbe. Kiasi cha fedha alichotoa Lowasa ni milioni 500 ambazo zimetumika kwa matumizi niliyoyataja hapo juu.

Katika kikao hicho, mjadala mkubwa ulitawala juu ya ujio wa Edward Lowasa ndani ya CHADEMA na hatimaye kupeperusha bendera ya chama hicho. Kutokana na tishio alilotoa Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei juu ya kuwafukuza Slaa na Lissu ikiwa hawatakubali Lowasa awe mgombea Urais, wajumbe hao waliamua kuridhia kwa shingo upande maamuzi ya wenye CHAMA. Kutokana na hali hiyo, Wajumbe wote 36 kwa kauli moja waliridhia Lowasa kujiunga na CHADEMA na awe Mgombea Urais.

Taarifa hii inahitimisha minong'ono iliyotanda siku nyingi tangu Lowasa akatwe. Kutokana na maamuzi hayo, uongozi wa CHADEMA umepanga kumtambulisha rasmi Lowasa kesho Jumanne Julai 28 kwenye Hotel ya Kilimanjaro Kempisk iliyopo Dar es Salaam.

Hata hivyo, ni lazima tujiulize kwa nini Lowasa anautaka sana urais kwa udi na uvumba? Je ni kweli ana uchungu wa kutatua kero zinazowakabili wananchi? Kama ndo hivyo, kwa nini akiwa Waziri Mkuu hakutumia nafasi hiyo na badala yake alitumia kufanya ufisadi hali iliyopelekea kujiuzulu kwake kutokana na kashfa za Richmond?

Ni vema tukatambua Watanzania kuwa Lowasa huyu huyu aliyekataliwa na Mwalimu Nyerere ndiye anayejiunga na CHADEMA. Ni Lowasa huyu huyu aliyekataliwa na CCM ndiye anayejiunga CHADEMA. Ni Lowasa huyu huyu aliyesimama kwa tambo nyingi akisema kuwa atakuwa wa mwisho kuondoka CCM na watakaomkataa waondoke wao ndiye anayejiunga na CHADEMA.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyataja mara kwa mara na kusisitiza kuwa ndiyo sifa za Edward Ngoyai Lowasa kutofaa kuwa kiongozi wa watu mambo yafuatayo;

  1. Ni mtu mpenda mali na kujilimbikiza mali kwa kiasi chochote na kwa hali yoyote anayoiweza. Lowasa anamiliki mali ambazo hazina maelezo ya jinsi alivyozipata. CCM waliliona hilo na wakamfungashia virago.
  2. Lowasa ni mtu dhaifu mbele ya mali na fedha kwa sababu hiyo njia na nafasi yoyote iliyo mbele yake anaweza kuitumia kupata fedha zaidi na kujilimbukiza mali.
  3. Ni mtu mwenye 'Pride' na kujitazama yeye tu na kupenda kutambulika kwa mali aliyonayo. Kwa sababu hiyo, anatumia muda na njia nyingi kujijazia mali badala ya kuongoza na kujali nchi yake (hii ndiyo sababu amekutwa na kashfa lukuki za ufisadi na kubwa zaidi ni ile ya Richmond iliyomfanya akaachia ngazi nafasi ya Waziri Mkuu).
  4. Lowasa anashindania zaidi kupata mali kwa njia zozote, ziwe za halali ama haramu. Kutokana na sababu hii ndio maana anajenga chuki na kulipiza visasi kwa watu anaoona kuwa vikwazo kwake katika kupata mali. Rejea jinsi alivyotuhumiwa kushiriki kumtesa Harrison Mwakyembe.
  5. Lowasa huwajali zaidi matajiri kuliko watu wa kipato cha chini. Hii ni kutokana na kulipa fadhila kwa watu wanaomsaidia katika harakati zake. Mathalan, wakati anatangaza safari ya matumaini, Lowasa alikuwa analazimisha wafanyabiashara kuchangia harakati zake kwa ahadi ya kufanya biashara na serikali akiwa Rais.

Kutokana na hoja hizi na nyingine nyingi bila kusahau ugonjwa unaoendelea kumsulubu, Lowasa hana sifa za hata kuteuliwa kugombea Udiwani. CHADEMA wamehadaika na tamaa ya fedha na wafuasi wa Lowasa. Bilioni 10 alizohongwa Mbowe zimefanya chama kitoke kwenye misingi yake na kuamua kumpokea fisadi.

Nawahurumia sana Dr Slaa, Godbless Lema, Tundu Lissu na wengineo ambao walijimaliza kutaja madhaifu ya Lowasa akiwa CCM. Je watafanya hivyo akiwa kwenye chama chao? Tusubiri tuone.

Ila jambo moja tu napenda kuwahakikishia wasomaji. Lowasa hana nafasi ya kushinda Urais. Nasema haya kwa kujiamini. Watanzania wamechoshwa na ufisadi. Watanzania wamechoshwa na viongozi wasiojali maslahi yao kama alivyo Lowasa. Watanzania si wepesi wa kusahau. Wameumizwa sana na hawa mafisadi na mwaka 2015 ni wa kukata mizizi yote ya ufisadi.
Usiwe na wasiwasi fisadi halisi ndio ana kwenda kujulikana na baada ya hapo ni kulipwa ujira wake sawasawa na matendo yake.
 
Kimenukaaaaaaaa...kimenukaaaaaaaa....
jana niliwaambia.... kimenukaaaaa....

CCM byeeeee byeeeeeeeee
 
Maskini CHADEMA, wana hoja zipi za kutuambia Watanzania juu ya ufisadi wa Lowasa?

ccm Walimfungashia virago ? Lini tena ? Lizaboni unaweweseka sana sahv kisa unakaribia kutia nuksi mkate wako wa kila siku. Hatimaye ukombozi wa pili unakaribia kupatikana.
 
wengi wetu tuliichukia ccm sababu ya ufsad Wa akina lowasa,Leo eti lowasa huyuhuyu asaidie kuiondoa ccm,to hell wote waliotusaliti.tutawazomea wote walioshiriki huu uovu.
 
Tanzania political landscape will not be the same again! It was heavily one-sided.
Now it will be different. Thanks UKAWA.
Thanks JK.
 
Nashangaa Watanzania wengi wanaogopa mabadiliko, hivi wanafikiri ni kazi ndogo kuiondoa ccm madarakani iliyokaa kwa miaka zaidi ya 40?
Wanahitajika watu strong kama Lowasa.

Huwezi kuitoa CCM bila kuivunja

Na unahitaji heavy weights kutoka CCM ili waivunje kwanza

Lowasa ni mtu sahihi
laki si pesa...Vaa Gwanda
 
Last edited by a moderator:
Kavumilia sana,sasa kama ni mtu wa visasi ndo hapo,maana kamzungukia vizuri

Na ninakwambia huyu jamaa huku kwetu kanda ya Ziwa anapendwa sana hasa Kahama na Shinyanga kwa inshu ya maji na alivyo na misimamo isiyoyumba.
 
Tanzania political landscape will not be the same again! It was heavily one-sided.
Now it will be different. Thanks UKAWA.
Thanks JK.

JK alishaaandaliwa kuikabidhi nchi Upinzani...Na hiki ndicho kinafanyika

Asante sana Jakaya Kikwete Mrisho
 
quote_icon.png
By AUDITOR OF MAFISADI

Baada ya kuwa kimya muda mrefu ''THE WHITE'' amesema wabunge zaidi ya 150,wakuu wa wilaya ,wa mikoa na viongozi mbalimbali wa serikali nao watanifuata,ndani ya siku mbili kuanzia leo.

Chanzo: Nipo kwenye kikao

Nauliza sasa jee hao wabunge 150, watapewa fursa yo kugombea ubunge kwa tkt cha chadema? Jee wale viongozi wa Chadema ambao wamejitayarisha muda wote huo watalazimika kutoa nafasi, ili Bw Lowassa awapachike watu wake?

Pia ningependa kuwakumbusha kuwa alipokuwa Waziri Mkuu ndipo alipoitumia hiyo fursa ya kujenga mtandao wake, wa kuwaweka watu wake kuwa Viongozi wa mikoa, wilaya na kata nyingi tuu, hii si itamaanisha Jembe Lowassa kuiteka chadema au tusema ameinunuwa so he can deal with it as he sees fit???????????????????

Tuombe Kheri ya Muumba
 
Makamanda wametweta, Baregu kajiinamia kaficha uso asipigwe picha, Slaa kaduwaa, kwa ujumla makamanda wote hawana sura ya furaha hata chembe, jembe ni jembe limetia timu.

Watanzania kweli mna mawazo duni mpaka leo tunaongelea jembe?
 
wengi wetu tuliichukia ccm sababu ya ufsad Wa akina lowasa,Leo eti lowasa huyuhuyu asaidie kuiondoa ccm,to hell wote waliotusaliti.tutawazomea wote walioshiriki huu uovu.
Makamanda mbele ya hela wamelegea kabisa...
 
For real sielewi hatma yangu chadema yaani naiangalia kadi yangu katiba yangu na bendera yangu ya chadema nafikilia mara mbili nivichome moto au!? Wakuu Lowassa simuamini kweli ndio uongozi umemtaka aje chadema!? Ngoja tuone!

Usichome, usichane, chukua hatua. Zamu ijayo gombea uongozi. Anzia chini na upande kwa kasi ya ajabu. Siku moja utapata nafasi ya kutenda unachokiamini. Hiyo ndiyo sababu ya kuwa mwanasiasa, kutenda na kushawishi wengine watende utakavyo. Lakini sio siri inafikirisha sana.
 
CHADEMA mbona hawaeleweki!!! Lowasa fisadi wanamkaribishaje? Basi wamsafishe maana wameimba sana wimbo kuwa Lowasa ni fisadi.

Hata wewe ingawa ni fisadi sana...Unakaribishwa kutubu CHADEMA

Ijapokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama damu...mkija CHADEMA zitasafishwa na kuwa kama Theluji
 
Back
Top Bottom