Kikao cha baraza la taifa la chama cha Walimu Tanzania tarehe 18/6/2023 jijini Dodoma ni mwarobaini wa mtikisiko ndani ya chama

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,368
5,967
Tangu kuasisiwa kwake Tarehe 1 novemba 1993 chama cha walimu Tanzania kimekua kikiongozwa kwa kutumia katiba na kanuni zake. Katiba imekua ikibadilika ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na mengineyo. Hadi kufikia 2014, CWT ilipata katiba ya toleo la 6 ambayo ndio inatumika hadi sasa.

Kadiri changamoto zinavyojitokeza, katiba na kanuni mara zote zimekua zikitoa majibu au mwelekeo. Kutokana na maendeleo ya kuridhisha ya chama cha walimu Tanzania yaliyoonekana kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo huduma kwa wanachama, kuwa na ofisi katika mikoa yote na wilaya zote nchini huku idadi ya wanachama ikiendelea kuongezeka sanjari na mapato yanayotokana na asilimia 2 ya michango ya kila mwanachama wanasiasa nao wamekua wakishawishika kuingilia kati ili kufaidika na uwepo wa chama hiki kimslahi. Walianza kujipenyeza 2018 baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Deus Gracewell Seif kujaza nafasi ya ukatibu mkuu wa CWT baada ya kufariki kwa aliyekuwa Katibu mkuu wa pili wa chama hicho marehemu Yahya Bakari Kilo Msulwa.

Baada ya kuchukua nafasi iliyokuwa wazi Deus Seif ambaye hapo awali alikua afisa elimu wilaya ya Geita na muasisi wa chama pinzani cha CWT kikijulikana kama Umoja wa Maafisa Elimu Tanzania (UMET) kwa kushirikiana na aliyekuwa mwekahazina wa taifa Abubakari Alawi aliamua kukamilisha lengo lake la kuwaibia walimu fedha na rasilimali zao. Alitekeleza kama ifuatavyo,
 1. Yeye na mwekahazina wa Taifa walienda Cape Verde kuangalia mechi ya mpira wa Miguu na kutumia shilingi milioni kumi na tatu na laki tisa wakatiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakapewa kifungo laini na cha kushangaza cha miezi 6 tarehe 28 juni 2022 gereza la ukonga ambapo na gerezani hawakukaa. Wafungwa hawa na Jamhuri wote wakakata rufaa mahakama kuu na mahakama hiyo katika uamuzi wa kushangza ikawafutia hatia kwa kuwapa ushindi dhidi ya jamhuri.
 2. Matumizi ya fedha kinyume na kanuni za fedha za CWT toleo la 2011 kwa kiini macho cha kutoa misaada ya kielimu kama vile saruji, madawati, mbao na fedha kwa kiwango kikubwa kwenye halmashauri na manispaa kadhaa nchini ili kuizuga serikali kwamba Deus ni mtumiaji mzuri wa fedha za chama na kwamba jamii inafaidika.
 3. Aliiba kwa kiwango kikubwa fedha ambazo zilipaswa kutolewa kwa walimu wanaostaafu kama fedha za mkono wa kwa heri(Golden Shakehand) sawasawa na mabati 20 kwa kila mwalimu ambapo alitengeneza majina feki ya walimu wastaafu na akaunti feki na fedha hizo zikaingia mfukoni mwake yeye na Abubakari Alawi. (Majina hayo tunayo ya walimu 8755 na yalikwishapelekwa TAKUKURU cha ajabu ni kwamba TAKUKURU haijachukua hatua hadi sasa.
 4. Mwaka 2021 kwa kulizuga baraza la taifa, alitumia zaidi ya shilingi Bilioni 5 eti kununua tshirts na kofia ambazo katika uhalisia tshirts hizo na kofia zilikuwa takribani laki moja badala ya laki mbili na elfu themanini. Waliosimamia utapeli huo ni Deus Seif, Abubakari Alawi, na Afisa manunuzi Irene Mrabu kupitia kampuni ya Shaa Company Limited ya Dar es salaam ambapo mume wa Irene Mrabu, Enock Nyasulu ni shareholder wa kampuni hiyo, sehemu ya fedha hiyo ikiwa ni mkopo wa Bilion 2 kutoka CRDB (TAKUKURU waliripotiwa kesi hii pamoja na kupewa vielelezo vyote muhimu kuhusu sakata hili hadi leo kimya)
 5. Baada ya kumaliza kifungo katika juhudi za kujaribu kurejea tena madakani Deus Seif na mwenzake wameendelea kuigawa kamati ya utendaji ya taifa ya CWT kwa kuwatumia baadhi ya wajumbe ambao walikuwa wafaidika wakuu wa utawala wa Deus CWT. Pasaka ya 2021 kwa mfano, wajumbe 18 wa kamati ya utendaji CWT walipatiwa shilingi 1,500,000 kila mmoja eti ikiwa ni misaada kwa shida walizokuwa nazo. Cha kujiuliza ni kwa nini walipatiwa kiwango sawa na kwa wakati mmoja. Wajumbe hao hao ndio wametumiwa kufanya vurugu ili kuhakikisha kwamba uongozi wa juu wa CWT hautulii. Deus na wenzake wanamtumia kaimu mwekahazina wa taifa ambaye muda wake unaisha July 4 mwaka huu Protas Magessa kukwamisha uidhinishaji wa malipo ya aina yoyote kwa kutoyasaini. Februari 2023 kwa mfano, malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa CWT yalikwisha idhinishwa na Katibu Mkuu na mhasibu mkuu tarehe 24 ya mwezi huo lakini Magessa alikataa kuyaidhinisha hadi tarehe 28 baada ya wajumbe wa baraza la taifa ambao ni waajiriwa walipotaka kumpiga jijini Tanga. Hadi sasa, Magessa anakataa kuidhinisha fedha za aina yoyote na mfanyakazi mwenye shida ni mpaka amlambe miguu ndipo alipwe kiasi cha baadhi ya wafanyakazi wa makao makuu kutumia fedha zao za mfukoni kuwasaidia walimu wenye shida mfano wagonjwa wanaofika makao makuu kuomba misaada (ushahidi tunao
WAJUMBE WAASI WA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA

Wajumbe 18 wa kamati tajwa hapo juu, wawili wakiwa wamesainiwa bila kuwepo walifanya vurugu makao makuu ya CWT tarehe 6 juni 2023 wakiwa wamefanikiwa kutengeneza mabango na kugawa tshirt na kofia kwa wahuni wa mtaani kisha wakavamia ofisi ya makao makuu huku wakiimba nyimbo za matusi kwa uongozi wa juu wakiwataja bayana tena kwa majina, rais,makamu wake na katibu mkuu wakiwataka kuondoka ofisini. Wajumbe hao wa KUT waasi waliingia kwenye eneo la ofisi ya makao makuu na kufanya kikao chini ya miti wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Mwalimu Joseph Misalaba na mwekahazina Protas Magesa huku Katibu Mkuu Maganga akiwa ofisini bila taarifa. Walialika pia vyombo vya habari lukuki ambavyo viliripoti kwa upotoshaji juu ya taarifa hii.

Kikao hiki hakikua halali na maazimio yake yalikua ni upuuzi mtupu kama ilivyobainishwa na barua ya msajili wa vyama vya wafanyakazi ya tarehe 9 Juni 2023 yenye kumbukumbu namba DA.27/380/12/91 kwa sababu zifuatazo.
 1. Muitishaji wa vikao vya kamati ya utendaji ya taifa, baraza la taifa na mkutano mkuu ni Katibu Mkuu wa chama akishirikiana na rais kwa mujibu wa katiba. Hawa hawakuwa wamehusishwa wala kujulishwa lolote
 2. Wakati baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wanafanya kikao haramu nje ya ofisi ya CWT makao makuu, Katibu Mkuu alikuwepo ofisini na hakujua lolote.
 3. Baada ya kukamilika kwa kikao hicho haramu, Joseph Misalaba alianza kumtumia mfanyakazi wa CWT Makao makuu aliyehamishwa ambaye aliuzuia uhamisho wake halali Alfred Alexander Kusaga kama secretary wake akisaidiana na Buto Masele kusambaza barua kwenye ofisi mbalimbali za serikali na taasisi nyingine kutambulisha kuwa Misalaba ndiye kaimu katibu mkuu wa CWT na Maganga si kiongozi tena jambo ambalo linakiuka katiba na kanuni za CWT. Mbaya zaidi Misalaba ameandika barua MCB kuwaarifu kwamba saini ya Maganga haruhusiwi kutoa pesa. Kwa mujibu wa kanuni za CWT, saini za msingi ni za Katibu Mkuu, mwekahazina na mhasibu mkuu. Hii imekuwa ikiyumbisha kama sio kusimamisha malipo mbalimbali. Misalaba amechongesha mihuri ya chama na anaitumia kughushi nyaraka mbalimbali za CWT huku akijua ni kosa kisheria na ni la jinai. Wajumbe wa baraza la taifa nyinyi ni mashahidi kwamba hata baada ya katibu mkuu kukubaliana na rais wa chama kuitisha kikao cha baraza la taifa cha tarehe 18 Juni 2023, Misalaba naye aliandika barua ya kufuta kikao hicho, hivi kiburi hiki mnakiona? Baraza la taifa linapokutana tarehe 18/6/2023 ni lazima limchukulie kiongozi huyu hatua za kinidhamu kwa sababu hatufahamu katika kutumia mihuri hii na barua anazoziandika kupingana na katibu mkuu ni kwa kiwango gani ameharibu hadhi na taswira ya chama kwa serikali na taasisi nyingine na pia huenda kuna ufisadi amefanya au anapanga kuufanya.
 4. Kiburi cha Misalaba kinaonekana kwenye kukaidi maagizo ya msajili wa vyama vya wafanyakazi kwa kuchongesha mhuri wa katibu mkuu na kuutumia kwa maslahi binafsi, hii ni hatari kama isipodhibitiwa kwani inaashiria uasi na mparaganyiko ndani ya chama unaoendelezwa na kundi la waasi wa kamati ya utendaji ya taifa. Kwa kuukuza mgogoro huu na kukichafua chama, Thobias Sanga, James Asagwile na Jerry Msangi wanatumia vyombo vya habari kila siku kwa kuukashifu na kuutweza uongozi wa juu wa CWT kwa maslahi binafsi tu kama tulivyokwishaeleza kwenye makala zilizopita. Hivi tunapaswa kuwaangalia tu?
JEURI YA WAJUMBE WAASI WA KUT NA MAPAMBANO YANAYOENDELEA INATOKA WAPI?

Kinachoendelea ni muendelezo wa vita tuliyokwisha ibainisha muda mrefu katika maandiko kadhaa. Vita hii inaratibiwa na kufadhiliwa na viongozi wachache waandamizi wa kisiasa ambao wakati wa uasi wa KUT waliingilia kati na kuwafadili wajumbe hao kifedha na kimfumo. Hebu tujiulize, wajumbe wale 18 nani aliwagharamia nauli, malazi ya siku 4 Dodoma, gharama za vikao na kuwalipa vijana wa mitaani kufanya fujo makao makuu ya CWT tarehe 6/6/2023. Kwa sababu kikao cha baraza la CWT taifa cha tarehe 18/6/2023 hakina mamlaka kuwawajibisha viongozi wa kiserikali tuliokwisha kuwabainisha wanaowasaidia Deus Seif na Abubakari Alawi kuendelea kukivuruga chama cha walimu, ni vyema baraza la taifa likafanya yafuatayo
 1. Kuwakemea Joseph Misalaba na Protas Magessa na kuwachukulia hatua nyinginezo stahiki kwa kukiuka katiba na kanuni za chama.
 2. Kuwakemea na kuwachukulia hatua za kinidhamu wajumbe waasi wa kamati ya utendaji ya taifa kama ilivyobainishwa na msajili wa vyama vya wafanyakazi
 3. Baraza la taifa liwakemee na kuwaonya baadhi ya wafanyakazi wa chama hususani wa makao makuu wanaotoa siri za chama na kuunga mkono uasi ndani ya chama kama ilivyobainisha kwenye makala zilizopita na kwamba wakibainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
 4. Wajumbe hao na wafanyakazi wasaini hati ya makubaliano (MOU) baina yao na baraza la taifa kwamba hawatarejelea walichokifanya tarehe 6/6/2023
 5. Baraza la taifa liwalaani watu wote wakiwemo viongozi wa kiserikali wanaochochea chokochoko ndani ya chama.
 6. Baraza la taifa liwaelekeze wafanyakazi wote waliopewa uhamisho kutoka makao makuu na ngazi nyingine kuripoti kazini kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
 
Mpanywungu Village! Tunakusubiri uje uelezee haya madhila ya Chama Chetu cha walimu ambapo wewe ni mdau namba 1.
 
Yani mtu anakatwa asilimia 2% ya mshahara mwaka mzima:
Mfano.
2/100 × 300000= 6000/= × miezi 12 = 72,000/= kwa miaka ya kazi kadhaa.
Faida ya makato:
1.Bundle la bati ukistaafu.
2.Pesa ya pole ukifa
3.T shirt,Kofia,Skafu kila mei mosi.
Kuna mambo yanachekesha sana moja wapo ni hili la CWT.
Walimu dah nawashukuru kwa mchango wenu aa kuinua maisha ya kila mtu.
KUHAMA
Kuhama humo ngumu sana kwa zile halmashauri giza kama vile zile za nje ya manispaa. Kwa mijini wengi wanahama ila manispaa za pembeni ngumu kuanzia afisa elimu hakubari uhame.
CHAMA KIBOVU HIKI.
 
Naomba kwa heshima na taadhima, Mwalimu Mpwayungu naye apewe mwaliko wa kunudhuria.

NB:- Mjiandae kumiliki majengo pekee. Maana walimu wote watawakimbia. Kisa tu ni ule wizi wenu wa kuwakata 2% kwenye mishahara yao kiduchu.
Walimu wanahama ila wanachofanya wanazuia vyama vipya kuanza au kukua wanashirikiana na Baadhi ya maafisa Elimu wapuuzi kutenda hayo
 
Hao SII DABILIU TIII kwa makusudi kabisa wanajineemesha viongozi tu walimu wa kawaida wanahangaika mtaani na kutetewa na watu wenye hasira na wasiopenda upuuzi wanaowafanyia walimu kama akina Mpwayungu Village...

Walimu nao wanachukulia poa wamekaa pembeni kimyaaaa... Nakereka sana.

Why nimeandika hapa...

Ninaye rafiki Mr mwalimu kaajiliwa 2022 "asante mama"... Nimemfahamu kupitia jamaa tunayepiga naye kibarua sehemu moja hivi...

Sasa mwezi wa tano akawa analalamika kuwa alikopa hela ile benki yao sijui ya waalimu na anauza deni NMB na hao NMB wameishalipa hiyo benki hela yao ingawa kwa kuchelewa, ila sasa hao benki ya walimu wanadai pesa imecheleweshwa NMB waiombe irudi kwani wamechelewa kulipa....

Nikashangaaaaa!

Nikamuuliza maswali yafuatayo,

Mimi: Kwa nini unatoka benki hiyo ya walimu ilihali ni ya kwenu walimu?

Mr mwalimu: Kaka, wana riba kubwa sana heri NMB.

Mimi: Hiyo benki si imeanzishwa kwa ajili yenu walimu (najua pia ni ya biashara kwa yoyote) hawana hata bonus yoyote ilihali wameanza na mtaji wa hela zenu...!

Mr mwalimu: Yaani kaka we acha tu!

Mimi: Nenda kwenye chama chenu wakusaidie kuwaambia watu wa benki yenu.

Mr mwalimu: Haya kaka... Ananiaga na kuondoka kinyonge sana

Sijui kama walimsaidia, ila ualimu ni kazi ngumu sana.

Wanangu wakikuwa wakataka kuwa walimu nitawapiga STOP! Kubwa sana.

Nasimama na wote wanaotetea walimu,

Na nyie serikalini hasa wabunge pitisheni sheria kuboresha maslahi ya walimu, wapeni posho ya chakula hata ya 100k... Kila katikati ya mwezi, anzeni na hiyo. Hawa chama cha walimu hakuna wanachofanya...
 
Kila mara CWT ikitajwa humu ni juu ya wizi na ubadhirifu.Hali kadharika Kila mara CCM ikitajwa hautakosa tuhuma za wizi,ufisadi,ubadhirifu,uonevu,uongo utekaji ,fitina ,sheria mbovu,mikataba mibovu,upendeleo,kinga kwa viongozi wasiostahili,ulinzi wa polisi,matumizi mabaya ya rasilimali za taifa,matumizi mabaya ya madaraka,uzinzi,dhuruma na wizi WA kura na maovu mengine ujuayo.HITIMISHO:CWT na CCM ni kopo na mfuniko.
 
Naomba kwa heshima na taadhima, Mwalimu Mpwayungu naye apewe mwaliko wa kunudhuria.

NB:- Mjiandae kumiliki majengo pekee. Maana walimu wote watawakimbia. Kisa tu ni ule wizi wenu wa kuwakata 2% kwenye mishahara yao kiduchu.
Sasa hivi wanashirikiana na maafisa tawala wa mikoa na wakurugenzi njaa wa baadhi ya halimashauri kuzuia walimu wasijiunge na vyama vingine vinavyotetea walimu. Wahuni hao wanatumia ofisi za umma na rasilimali zake kuwatisha/kuwakataza na kuwarubuni walimu wasiondoke CWT. Tulitaraji Hawa wangewaonea huruma walimu wanaoibiwa 2% ya mishahara Yao Kila mwezi badala yake wanawalazimisha kunyang'anywa fedha zao na hayo majambazi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom