Na Maregesi Paul, Chunya
BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Kanga, wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, ambacho baadhi ya wakazi wake walipiga kwa mawe baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, wametishia kumshambulia kwa mawe Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto.
Wanakijiji hao walidai kuwa tayari kumshambuliwa kwa mawe Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini kama asingewahutubia kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.
Walitoa onyo hilo juzi kijijini hapo, muda mfupi baada ya Kabwe kuwataarifu kuwa asingehutubia mkutano wa hadhara katika muda uliopangwa kwa kuwa alikuwa akisubiriwa katika Kijiji cha Mkwajuni, wilayani humo.
Pamoja na kuwaambia kuwa angerudi tena katika kijiji hicho kwa ajili ya kuwahutubia, wananchi hao walionyesha kutoridhishwa na ahadi hiyo na kumtahadharisha kuwa asije akawalaumu iwapo kama asingewahutubia baada ya kutoka Mkwajuni kwa vile wanahitaji kusikia sera za chama chake.
"Sisi tunakusubiri kama unavyotuahidi, lakini kama utajifanya mjanja, basi usije ukatulaumu kwani tutaishambulia gari yako kwa mawe," walisikika baadhi ya wakazi hao wakisema.
Ili kuwatoa hofu, Zitto aliwasisitizia kwamba asingeondoka wilayani humo bila kuwatuhutubia kwa vile lengo la chama chake ni kuzungumza na Watanzania wote ili wajue namna ya kuiondoa madarakani CCM.
"Jamani naomba msinipige mawe kwa sababu nitakaporudi kutoka Mkwajuni, lazima nitawahutubia kwani nisipofanya hivyo nitakuwa siwatendei haki kwani hata nyinyi ni wapiga kura," alisema Zitto.
Akihutubia kijijini hapo baada ya kurejea kutoka Kijiji cha Mkwajuni, Zitto alikemea vitendo vyovyote viovu vinavyofanywa na wananchi dhidi ya viongozi wa kitaifa.
Alisema kwamba, kitendo cha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kuupiga mawe msafara wa Rais Kikwete, kinafaa kukemewa kwa nguvu zote kwa vile historia ya Watanzania inaeleza jinsi wanavyopenda amani tofauti na nchi zingine duniani.
"Nilisikitika sana niliposikia kwamba, msafara wa Rais Kikwete ulipigwa mawe na baadhi yenu kwa sababu hiyo siyo historia ya taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa duniani.
"Hata kama kiongozi amewachosha, njia sahihi siyo kumpiga mawe bali ni kutompigia kura wakati wa uchaguzi kwa sababu yeye anapatikana kwa kura," alisema Zitto.
Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete kuwawajibisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Fatuma Kimario, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kanga na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kanga kwa madai kuwa wameshindwa kutatua kero zilizosababisha wananchi hao kushambulia msafara wa Rais.
Alisema kwamba, watumishi hao wanastahili kuchukuliwa hatua kwa vile chanzo cha wananchi kuurushia mawe msafara wa Rais kilikuwa kinajulikana ingawa viongozi hao kwa nyakati tofauti walishindwa kuwasikiliza wananchi hao.

Last edited by a moderator: