Wananchi wa Mwakitolyo wilayani Shinyanga na athari ya vumbi linalosababishwa na usombaji mawe ya dhahabu

iyokichiku

Member
Oct 30, 2023
36
70
Wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo wilayani shinyanga wanaathirika kwa kiasi kikubwa na vumbi linalosababishwa na magari makubwa yanayosomba mawe ya dhahabu kutoka Kijiji Cha nyaligongo kwenda mgodi was ZEM DEVELOPMENT unaomilikiwa na Wachina.

Viongozi simamieni hilo kwani afya za watu wanaoishi katika Kijiji hichi zipo hatarini sana kwa kupata homa ya mapafu.

Wawekezaji Hawa wanatakiwa kumwaga maji katika babara hii Kama wanavyofanya wanaotengeneza reli ya SGR wanaposomba moramu.

Serikali tumeni wataalamu wa mazingira kuona hili la sivyo afya za watu zitazidi kudhoofika.

Hiyo picha inaonyesha baadhi ya magari hayo
 
suala hili limefika ofisini tunalifanyia kazi kupitia vikao
Na mtakaa vikao vitano kila wiki kuhakikisha mnapata ufumbuzi wa suala hili. Vikao hivi vitachukua wiki tatu mfululizo hivyo katika kipindi hicho mtakuwa mmetumia siku 15 tu.

Ili msichoke mapema fedha za vikao zitakuwa zinalipwa kabla ya vikao vyenyewe kuanza kila asubuhi. Tunawatakia kila la kheri katika majukumu yenu hayo mliyojipangia.
 
Wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo wilayani shinyanga wanaathirika kwa kiasi kikubwa na vumbi linalosababishwa na magari makubwa yanayosomba mawe ya dhahabu kutoka Kijiji Cha nyaligongo kwenda mgodi was ZEM DEVELOPMENT unaomilikiwa na Wachina.

Viongozi simamieni hilo kwani afya za watu wanaoishi katika Kijiji hichi zipo hatarini sana kwa kupata homa ya mapafu.

Wawekezaji Hawa wanatakiwa kumwaga maji katika babara hii Kama wanavyofanya wanaotengeneza reli ya SGR wanaposomba moramu.

Serikali tumeni wataalamu wa mazingira kuona hili la sivyo afya za watu zitazidi kudhoofika.

Hiyo picha inaonyesha baadhi ya magari hayo
Na madereva wa hizo gari walivyo na dharau, hawapunguzi mwendo hata sehemu yenye watu, sisi bodaboda tukikutana nao inabidi tupaki pembeni kwanza wapite
 
Hii ni hatari kubwa kwani Kila baada ya dk 5 magari makubwa yanapita happy huku yakiacha vumbi kubwa.
Watu wa eneo hili kikohozi na mafua haviishi.
IMG_20231204_095248_1.jpg
 
Back
Top Bottom