Nimeangalia picha ya huyu Kijana wkenye jeneza [ITV] ,he was too youg to die,ameniuma sana na hadi nimetoa machozi,kazaliwa 1988,gone too soon. Japo imeniuma sana nimeanza kutafakari matukio yanayolikumba jeshi la polisi yakiwemo kuvamiwa vituo ,kujiua nk na kujiuliza yafuatayo:
1.Nini kazi ya walinzi wa kituo ,au wanakuwa wapi hadi vituo vinavamiwa?
2.Zamani tulizoea kuona polisi warefu,wenye vifua na wenye nguvu,hivi awa askari wa siku hizi wana ajiliwa kwa vigezo gani,sasa hivi utakutana na vi-askari vidogo,vifupi ambavyo hata kuwambia mtu kama mimi niliyepanda kuwa huko chini ya ulinzi vinaogopa,sasa hata kama ni haki za binadamu za kutakiwa kuajili bila ubaguzi hivyo kupokea vi -askari vidogovidogo mbona kwenye Ma-TV hao waliotuletea hizo haki za Binadamu [Wazungu] huwezi kuona vi-askari vya Kizungudesign hiyo? askari wa Kizungu tunaowaona kwenye TV wote wameshiba na wamepanda,nadhani kwa ranks fulani it is ok kuajili vi-askari vidogovidogo lakini kwenye rank za mituringa tuwe tuna angalia na maumbile ya askari tunao recruit otherwise hii trend ya vibaka kuwaona askari watu wa kawaida sana itaendelea.
3.Huyu Marehemu wakati kapigiwa simu ya kuitwa kwenye tukio kwanini hakuwa accompanied na askari mwenzake,kwanini aende peke yake?hii trend ya askari kwenda mmoja mmoja kwenye tukio inaweza pia kuchangia kwa askari kushambuliwa kwa urahisi,hao aliokuwa nao ni raia wasingewza kumsaidia lolote,sana sana walitimua mbio walipoona kimenuka.
4.Yule askari aliyejipiga risasi Singida,nimejiuliza sana kwanza Utaratibu wa kutoa silaha,kama huyo askari hakuwa kwenye doria na hakukuwa na maagizo yoyote ya OCD iweje aend tu bila reference yoyote na kukabidhiwa bunduki?hapa nadhani kuna uzembe ulifanyika.Pili kwa miaka mingi sasa sijawahi kuona polisi wakiwa doria au Kazini na bunduki za SAR [semi automatic rifle,hizo navyofahamu ni silaha za mgambo au polisi jamii au ni silaha za parade,iweje askari huyo akabidhiwe bunduki ya aina hiyo kwenda nayo safari na OCD? nadhani hapa pia kuna tatizo
5.Hivi vituo vnavyovamiwa kila siku walinzi wa vituo wanakuwa wapi? pia huko nyuma watu kupitia JF walitahadhalisha juu ya mazoezi makali ya karate nk yanayofanyika kwenye baadhi ya nyumba za ibada na walizitaja baadhi nyumba hizo,je police mlichukua hatua gani kufuatilia hao vijana wanaopewa mafunzo makali kupitia mgongo wa dini fulani fulani?