Kiingilio cha madhabahu za giza

Kiingilio cha madhabahu za giza

Kuna yule alienda kwa mtu mzito nadhani amekuelewa.
.

Halafu huwa nashangaa hivi kuna msomi Wa siku hizi anaenda kwa waganga
Wew acha zako bhna wakubwa wa nchi wanakalishwa kwenye vigoda unazania ni mchezoo
 
Unapoenda kwa mganga wa kienyeji unaenda kutengeneza maagano
Ukifika pale lazima yatatokea haya
1. Atavaa mavazi rasmi ya kazi (inaitwa kuvaa miongozo)
2. Mtakuwa kwenye chumba chenye madhabahu inayoendana na shughuli zake(kilinge)
3. Utajieleza ama atakueleza matatizo yako!
4. Utatoa pesa na kuiweka kwenye chombo maalum kilichopo madhabahuni ama karibu na hapo! Hupangiwi kiasi(hapa unatoa kiingilio bila kujua)
Ukishatoa yatafuata matibabu utatumwa vya kuleta, lazima damu itahusika in most cases! Kwanini damu? Kwakuwa ni chakula cha kuzimu! Na hapa baada ya kuingia kwa kutoa kiingilio sasa unaanza kutumikia, unaanza kuhudumia
Yatakayoendelea yote ni utumwa, utaelekezwa ya kufanya na utaambiwa ufuate masharti la sivyo hutafanikiwa! Unatii bila kujua kuwa tayari umeshaingia kwenye milki na maagano mabaya kabisa
Kwa kiasi kidogo kabisa cha pesa, unaharibu mchoro wako wa maisha kwa kuingiza visivyotakiwa! Yani unajaribu kuiedit asili! Unataka kuusahihisha uumbaji!
Utapata utakacho lakini kwa masharti utatumikia maagano na mamlaka za kuzimu! Utakuwa ni MTU wa kutoa makafara ya damu kwenye madhabahu za giza... Utapata mafanikio lakini ni ya muda,..
Kadiri muda unavyoenda utaanza kuchoka na kuanza kugundua ukweli kwamba huna amani tena huna furaha tena na unaishi kwenye utumwa wa maagano na masharti mengi! Unajiona tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo! Unaikumbuka asili yako(ukibahatika)...sasa vita kamili huanzia hapa! Kutaka kufuta yale marekebisho uliyofanya tena kwa kiingilio na kafara!
Ushirikina haujawahi kumuacha mtu salama! Kuwa makini unapotafuta suluhisho la matatizo yako!!!!
Asante sana mkuu haya ni zaidi ya mahubiri au mawaidha .na kufanya hivyo ni chukizo kubwa kwa mungu wetu na ndio chanzo cha mateso mengi/mapigo mengi ya wana wa Israeli.Ubarikiwe sana mkuu
 
Asante sana mkuu haya ni zaidi ya mahubiri au mawaidha .na kufanya hivyo ni chukizo kubwa kwa mungu wetu na ndio chanzo cha mateso mengi/mapigo mengi ya wana wa Israeli.Ubarikiwe sana mkuu
 
Tofauti kati ya sadaka na kiingilio
Sadaka ni tendo la shukrani na haitolewi mwanzoni... Kinachotolewa mwanzoni ni kiingilio.. Hivyo unapoenda kwa mganga kile unachotoa ni kiingilio sio sadaka
 
.
tapatalk_1575869678125.jpeg
 
.
hqdefault-5.jpeg
 

Attachments

  • cc3ec245ef7ba6df4409a801a170c153.jpeg
    cc3ec245ef7ba6df4409a801a170c153.jpeg
    10 KB · Views: 16
Back
Top Bottom