Kiingilio cha madhabahu za giza

Kiingilio cha madhabahu za giza

Ulichoniudhi mimi umechelewa sana kuipost, uwe unazipost kuanzia saa tano na nusu mpaka saa nane na nusu usiku,tena uwe unazinogesha na ile mipicha picha ya kutisha maana mi bila kutazama horror movie huwa kausingizi hakanogi
 
Ulichoniudhi mimi umechelewa sana kuipost, uwe unazipost kuanzia saa tano na nusu mpaka saa nane na nusu usiku,tena uwe unazinogesha na ile mipicha picha ya kutisha maana mi bila kutazama horror movie huwa kausingizi hakanogi
 
kwahiyo mkuu zile sherehe za mwisho wa mwaka kule milimani za kuchinja Mbusi zaweza kuwa ndiyo haya mambo
Haya maagano ya koo na families zetu nayo ni mabaya mno! Yani mnatengeneza roho na kuilisha nanyi mnashiriki ile ibada kwa kula ile nyama bila kujua
Na ili hii roho iendelee kupata uhai inabidi kila wakati ipate damu, si kama chakula as such bali lile tendo
 
Unapoenda kwa mganga wa kienyeji unaenda kutengeneza maagano
Ukifika pale lazima yatatokea haya
1. Atavaa mavazi rasmi ya kazi (inaitwa kuvaa miongozo)
2. Mtakuwa kwenye chumba chenye madhabahu inayoendana na shughuli zake(kilinge)
3. Utajieleza ama atakueleza matatizo yako!
4. Utatoa pesa na kuiweka kwenye chombo maalum kilichopo madhabahuni ama karibu na hapo! Hupangiwi kiasi(hapa unatoa kiingilio bila kujua)
Ukishatoa yatafuata matibabu utatumwa vya kuleta, lazima damu itahusika in most cases! Kwanini damu? Kwakuwa ni chakula cha kuzimu! Na hapa baada ya kuingia kwa kutoa kiingilio sasa unaanza kutumikia, unaanza kuhudumia
Yatakayoendelea yote ni utumwa, utaelekezwa ya kufanya na utaambiwa ufuate masharti la sivyo hutafanikiwa! Unatii bila kujua kuwa tayari umeshaingia kwenye milki na maagano mabaya kabisa
Kwa kiasi kidogo kabisa cha pesa, unaharibu mchoro wako wa maisha kwa kuingiza visivyotakiwa! Yani unajaribu kuiedit asili! Unataka kuusahihisha uumbaji!
Utapata utakacho lakini kwa masharti utatumikia maagano na mamlaka za kuzimu! Utakuwa ni MTU wa kutoa makafara ya damu kwenye madhabahu za giza... Utapata mafanikio lakini ni ya muda,..
Kadiri muda unavyoenda utaanza kuchoka na kuanza kugundua ukweli kwamba huna amani tena huna furaha tena na unaishi kwenye utumwa wa maagano na masharti mengi! Unajiona tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo! Unaikumbuka asili yako(ukibahatika)...sasa vita kamili huanzia hapa! Kutaka kufuta yale marekebisho uliyofanya tena kwa kiingilio na kafara!
Ushirikina haujawahi kumuacha mtu salama! Kuwa makini unapotafuta suluhisho la matatizo yako!!!!
mshana jr hivi inakuwaje unaenda kwa mganga halafu anaanza kukuelezea matatizo yako yote ???? huwa wanafanyaje fanyaje?
 
Iko hivi wale waganga wa kweli wanaona kivuli chako chenye marks ambazo kila moja inatafsiri yake
Hivyo anazisoma na kuzitafsiri katika ulimwengu wa matatizo
 
Back
Top Bottom