Kiingilio cha madhabahu za giza

Kiingilio cha madhabahu za giza

Kwa maelezo zaidi zipo madhabahu 3 maarufu hapa ulimwenguni

Madhabahu ya giza:
Nguvu yaa madhabahu ya Giza huwa ni ya muda tu na yenye masharti makali mno; inahusisha kununua ama kufuga mapepo ambayo yatakupatia kila utakacho as long as unatoa kafara kama mlivyokubaliana - hii madhabahu ni mbaya sana sana - once your in there is no way out - unapata shinda mno kujitoa - hapa kafara utaambiwa umtoe baba ama mama yako mzazi, mtoto unayempenda, mke nk ili ufanikiwe - Madhabahu hii inahusika na Uchawi - kiasi cha upendo ulichonacho kwa umtoaje kafara ndiyo nguvu ya madhabahu hii inakuwa kubwa !!

Madhabahu za kiukoo: (Matambiko ya kiukoo)
Hizi madhabahu za kiukoo hazina masharti magumu sana, na si uchawi - kifupi ni kuisujudu mizimu ya kwenu tu ili ifurahi - kuiomba ikutakase wewe na wana ukoo wote yaani itende miujiza yake hasa hasa kuondoa laana na mikosi inayokuja kuukabili ukoo, yaani kusafisha njia yako kwa kila jambo unalolikusudia kufanya- hiii madhabahu huwa haina masharti magumu kama ya kumwaga damu ya mtoto, mke, baba ama mama hapana kafara hapa yaweza kuchinja kondoo, mbuzi, kuku na inaliwa na wanaukoo wote yaani siku ya matambiklo ni furaha tu mwanzo mwisho - hii ndio madhabahu maarufu iliyotumiwa na mababu zetu kabla ya ujio wa wamisionari, kuna baadhi ya koo bado wanaitumia hadi leo

Madhabahu ya Kiroho
Madhabahu yenye nguvu kulizo zote ni hii, hapa unamsujudu Mungu Mwenyezi muumba mbingu na nchi - madhabahu hii ilikuwepo tangu uubwaji wa ulimwengu huu - ipo mifano mingi ambayo manabii wa kale waliitumia madhabahu hii na kuziona nguvu za Mungu zikishuka mawinguni , mifano ni manabii Daniel, Mussa, Elia, na wenagineo - Hii madhabahu imekuja kupata nguvu zaidi baada ya Damu yake Mwana wa Mungu kumwagika pale msalabani kama ondoleo la dhambi na msamaha kwetu wanadamu bure

Binadamu wa sasa nakushauri tumia No 3 - haijalishi wewe huna dini ma una dini ila no 3 is the best - kwanza ni free pia ni ya kudumu kiazi na kizazi - Ukiamini uwepo wa Mungu Mwenyezi basi unakuwa na roho mtakatifu ndani yako ambapo ndimo uzima ulimo - hakuna shetani ama chochote kitakudhuru hapa duniani - its 100% protection free my friend
 
Unapoenda kwa mganga wa kienyeji unaenda kutengeneza maagano
Ukifika pale lazima yatatokea haya
1. Atavaa mavazi rasmi ya kazi (inaitwa kuvaa miongozo)
2. Mtakuwa kwenye chumba chenye madhabahu inayoendana na shughuli zake(kilinge)
3. Utajieleza ama atakueleza matatizo yako!
4. Utatoa pesa na kuiweka kwenye chombo maalum kilichopo madhabahuni ama karibu na hapo! Hupangiwi kiasi(hapa unatoa kiingilio bila kujua)
Ukishatoa yatafuata matibabu utatumwa vya kuleta, lazima damu itahusika in most cases! Kwanini damu? Kwakuwa ni chakula cha kuzimu! Na hapa baada ya kuingia kwa kutoa kiingilio sasa unaanza kutumikia, unaanza kuhudumia
Yatakayoendelea yote ni utumwa, utaelekezwa ya kufanya na utaambiwa ufuate masharti la sivyo hutafanikiwa! Unatii bila kujua kuwa tayari umeshaingia kwenye milki na maagano mabaya kabisa
Kwa kiasi kidogo kabisa cha pesa, unaharibu mchoro wako wa maisha kwa kuingiza visivyotakiwa! Yani unajaribu kuiedit asili! Unataka kuusahihisha uumbaji!
Utapata utakacho lakini kwa masharti utatumikia maagano na mamlaka za kuzimu! Utakuwa ni MTU wa kutoa makafara ya damu kwenye madhabahu za giza... Utapata mafanikio lakini ni ya muda,..
Kadiri muda unavyoenda utaanza kuchoka na kuanza kugundua ukweli kwamba huna amani tena huna furaha tena na unaishi kwenye utumwa wa maagano na masharti mengi! Unajiona tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo! Unaikumbuka asili yako(ukibahatika)...sasa vita kamili huanzia hapa! Kutaka kufuta yale marekebisho uliyofanya tena kwa kiingilio na kafara!
Ushirikina haujawahi kumuacha mtu salama! Kuwa makini unapotafuta suluhisho la matatizo yako!!!!
Sasa kwanini unafanya haya Mshana Jr huoni kama unamkufuru Mungu, kingine....hivi wateja wako wengi ni kina nani wabunge au mademu machangu?
 
Hataki kuelewa kila siku anabadilisha waganga wa kumzindikia nyumba yani ni very addict in witch issue imagine nyumba ndani ya miez 6 inaweza kupitiwa ata na waganga 3 sasa naona ata hizo nguvu za waganga zinaanza kupingana zenyewe
Soma hii

Usitoe kafara kupita kiasi utaishia kuwa sugu
 
Kwa maelezo zaidi zipo madhabahu 3 maarufu hapa ulimwenguni

Madhabahu ya giza:
Nguvu yaa madhabahu ya Giza huwa ni ya muda tu na yenye masharti makali mno; inahusisha kununua ama kufuga mapepo ambayo yatakupatia kila utakacho as long as unatoa kafara kama mlivyokubaliana - hii madhabahu ni mbaya sana sana - once your in there is no way out - unapata shinda mno kujitoa - hapa kafara utaambiwa umtoe ni baba, mama, mtoto unayempenda, mke nk ili ufanikiwe - Madhabahu hii inahusika na Uchawi - kiasi cha upendo ulichonacho kwa umtoaje kafara ndiyo nguvu ya madhabahu hii inakuwa kubwa !!

Madhabahu za kiukoo: (Matambiko ya kiukoo)
Hizi madhabahu za kiukoo hazina masharti magumu sana, na si uchawi - kifupi ni kuisujudu mizimu ya kwenu tu ili ifurahi - kuiomba ikutakase wewe na wana ukoo wote yaani itende miujiza yake hasa hasa kuondoa laana na mikosi inayokuja kuukabili ukoo, yaani kusafisha njia yako kwa kila jambo unalolikusudia kufanya- hiii madhabahu huwa haina masharti magumu kama ya kumwaga damu ya mtoto, mke, baba ama mama hapana kafara hapa yaweza kuchinja kondoo, mbuzi, kuku na inaliwa na wanaukoo wote yaani siku ya matambiklo ni furaha tu mwanzo mwisho - hii ndio madhabahu maarufu iliyotumiwa na mababu zetu kabla ya ujio wa wamisionari, kuna baadhi ya koo bado wanaitumia hadi leo

Madhabahu ya Kiroho
Madhabahu yenye nguvu kulizo zote ni hii, hapa unamsujudu Mungu Mwenyezi muumba mbingu na nchi - madhabahu hii ilikuwepo tangu uubwaji wa ulimwengu huu - ipo mifano mingi ambayo manabii wa kale waliitumia madhabahu hii na kuziona nguvu za Mungu zikishuka mawinguni , mifano namii Daniel, Mussa, Elia na wenagineo - Hii madhabahu imekuja kupata nguvu zaidi baada ya Damu yake Mwana wa Mungu kumwagika pale msalabani kama ondoleo la dhambi na msamaha kwetu wanadamu bure

Binadamu wa sasa nakushauri tumia No 3 - haijalishi wewe ni huna dini ma una dini ila no 3 is the best - kwanza ni free pia ni ya kudumu kiazi na kizazi - Ukiamini uwepo wa Mungu Mwenyezi basi unakuwa na roho mtakatifu ndani yako ambapo ndimo uzima ulimo - hakuna shetani ama chochote kitakudhuru hapa duniani - its 100% protection free my friend
Dah FUSO Asante sana kwa ufafanuzi huu..umedadavua kwa kina na kutoa ufafanuzi wa kina na maelezo yanayoeleweka vizuri sana...SHUKRANI _
 
Sasa kwanini unafanya haya Mshana Jr huoni kama unamkufuru Mungu, kingine....hivi wateja wako wengi ni kina nani wabunge au mademu machangu?
Ya kaisari tunampa kaisari..tuko chini ya mkuu wa anga na sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wake Mungu ..kati yetu sote HAKUNA MKAMILIFU LA HATA MMOJA..
 
Soma hii

Usitoe kafara kupita kiasi utaishia kuwa sugu
Nimeisoma vizuri kumbe yeye yupo begginer😄😄level kila mwisho wa mwezi anajicha kuku pale mwezi ukitoka pia mbuzi mara moja moja lakini kwangu kula vitu ninavyojua ni kafara hakunipata
 
Ya kaisari tunampa kaisari..tuko chini ya mkuu wa anga na sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wake Mungu ..kati yetu sote HAKUNA MKAMILIFU LA HATA MMOJA..
Kwa hiyo wewe unajijuwa unatenda madhambi kwa makusudio, sasa kama unajijuwa si uache tu?
 
Nimeisoma vizuri kumbe yeye yupo begginerlevel kila mwisho wa mwezi anajicha kuku pale mwezi ukitoka pia mbuzi mara moja moja lakini kwangu kula vitu ninavyojua ni kafara hakunipata
Kama hana nalengo makubwa ataishia kwa hao hao lakini haya mambo yalivyo anaweza kuja kuambiwa sasa ni wakati wa kutoa kafara kubwa ..
 
Kama hana nalengo makubwa ataishia kwa hao hao lakini haya mambo yalivyo anaweza kuja kuambiwa sasa ni wakati wa kutoa kafara kubwa ..
Sasa hivi akili yake haipo vizuri yani kuvaa kulishabadilika yani ni kama semi-mganga bado ajawa full mganga
 
Sasa hivi akili yake haipo vizuri yani kuvaa kulishabadilika yani ni kama semi-mganga bado ajawa full mganga
Kama unaishi naye hiyo nyumba imwagie chumvi ya mabonge kuizunguka ndani na nje kisha nipe mrejesho
 
Mshana wakati wa kumaliza mazishi niliambiwa nisubiri kufanya mila, nikapuuzia na kuondoka maana hadi nakuwa mtu mzima sikuwahi kufundishwa hayo maswala ya mila na mambo ya mizimu....ninachojua nilifanya mafundisho nikabatizwa tukawa tunaenda kanisani kila jumapili na wenzangu. Swali langu ni je, hizo mila huwa ni kitu gani? na je, kuna watu ndani ya ukoo wenye uelewa wa hayo mambo na wengine wasiojua lolote ingali ni watu wazima?
 
Sio lazima utoe pesa.
Yuko kafir mmoja amekwenda mbele zaidi.
Ukitii masharti yake anakupa Kama 30 mpaka 50 M ukaanzie biashara Ila utatejesha ukifanikiwa. Acheni jama kufuru ipo..
Ila mwisho wake utakapo karibia kufa Cha Moto utakiona hapa duniani kabla ya Moto wa milele.
Sharti la kwanza Ni rahisi sana. Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mkeo ukishindwa oa hata wanne.
Ila hayo mengine.......
Kumbe maji yaliyooshea maiti Ni dili sana, sikua nimejua.
Siku hizi umegundua wakati wanakwenda kuzika maiti ya kiislamu wanateuliwa kabisa watakaoingia kaburini kupokea maiti? Kumbe mle ndani wakati kaburi limefunikwa ukiwa makini Kama umeingia mle ndani unaweza kuinuka na kitu unachoweza kuwauzia waganga kwa Bei utakayotaka.
Tz Kuna matajiri wengi sana wanaotumia ushirikina.
 
Mshana wakati wa kumaliza mazishi niliambiwa nisubiri kufanya mila, nikapuuzia na kuondoka maana hadi nakuwa mtu mzima sikuwahi kufundishwa hayo maswala ya mila na mambo ya mizimu....ninachojua nilifanya mafundisho nikabatizwa tukawa tunaenda kanisani kila jumapili na wenzangu. Swali langu ni je, hizo mila huwa ni kitu gani? na je, kuna watu ndani ya ukoo wenye uelewa wa hayo mambo na wengine wasiojua lolote ingali ni watu wazima?
Ungesubiri tu... Mila ni zile za kugawa vitu vya marehemu na mambo mengine ya kindugu, uangalizi na kutakiana kheri
 
Ungesubiri tu... Mila ni zile za kugawa vitu vya marehemu na mambo mengine ya kindugu, uangalizi na kutakiana kheri
Je, hizo mila haziwezi kurithisha roho za mauti zinazohusisha makafara ya kiukoo ya mizimu, uchawi na uganga. Je, mikoba inayorithiwa endapo babu au bibi kafariki kwenye ukoo huwa ni kitu gani na inalenga nini?
 
Back
Top Bottom