Kiingilio cha madhabahu za giza

Kiingilio cha madhabahu za giza

Mshana Jr kuna ile wanasema kutambulisha watoto kwenye ukoo...!
Mbuzi anachinjwa nyama inaliwa na wanaukoo wote, kama MTU atagoma kufanya hivyo basi wanae watakuwa na shida mbali mbali. Mfano uncle wangu amegoma ila wanae wa kwanza wa kiume na kike wana shida kubwa sana ya macho,
Niliwahi kumsikia bibi akisema ni kwa sababu baba yao amekataa kuchinja mbuzi ya kuwatambulisha kwenye ukoo. Nadhani haina tofauti na mganga wa kilingeni. Ile mizimu inakuamdama popote uendapo lazima itataka uje utukuze mizimu kwa mbuzi labda uwe tasa
madhabahu za ukoo hizo ndugu,zivunje
 
Uko vzr kutujuza....! tatizo hili ni kubwa kiasi gani huku kwetu Afrika v Ulaya/USA? Kuna uhusiano wowote kati ya elimu (contemporary education), dini za mapokeo na imani za maagano?
Tatizo ni kubwa lakini halifikii kwa wenzetu ambao wamefika pa kuhalalisha kabisa na kutengeneza maroho ya ajabu kweli
Pamoja na elimu lakini bado Afrika kuna hofu ya Mungu
 
Sala na maombi tu hakuna namna nyingine.....ila lazima kujiandaa vema kwakuwa kutakuwa na vita ya kiroho kubwa tu
Yeah nakubaliana nawewe...vita lazioma viinuke,na hapo usipokuwa makini uatapotea,lakin sadakani muhimu sana katika vita hii ili ``kulainisha`` process ya ushindi
 
mkuu ufafanuzi kidogo juu ya kuelewa,kwani kuzimu watu wanakula!
 
ipo njia ya kutoka katika mateso ya kutumikia mamlaka za kuzimu nayo ni moja tu:

YESU KRISTO! YEYE NDIE UZIMA NA WOTE WAENDAO KWAKE HUPATA UZIMA WA MILELE

katika ushuhuda mmoja, kuna mtu mmoja ambaye ni msomi mzuri mwenye mafanikio makubwa hivi sasa baada ya Kumpokea na Kumkiri YESU KRISTO Kuwa Bwana na Mwokozi Wake. mtu huyo alikuwa na tamaa ya kupata utajiri wa haraka (pesa za mashetani) hivyo akaenda kwa mganga wa kienyeji ambaye makao makuu yake ni mkoa flani kusini mwa tanzania.

mwanzoni kila kitu kitu kilikuwa kizuri na mganga yule alimuahidi kuwa angekuwa tajiri sana na yule mtu alijiona ya kuwa ni mwenye bahati sana kukutana na yule mganga. lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda, hali ya yule kijana kijamii na kiuchumi ilizidi kuwa mbaya sana.

ilifika hatua zile mamlaka za kuzimu alizokuwa anazitumikia BILA KUJUA, akifikiri atapewa utajiri, zilivyoona kuwa ameishiwa zikambadilikia na kuwa wakali kabisa wakimshurutisha awe analeta sadaka kwa lazima na kumtishia kuwa watadhuru familia yake. ilipotokea kuwa yule mtu anakosa hela basi alikuwa akiadhibiwa vikali sana na falme hizo za kuzimu.

hiyo hali alidumu nayo kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu na alikuwa na hali mbaya sana na hakuwa na Amani ya roho kabisa.

katika kusikiliza mahubiri katika kanisa fulani, akiongozwa na kuelekezwa na Roho Mtakatifu anenaye kwa vinywa vya watumishi wake, akatoa sadaka ya fungu la kumi (10% ya pato lake) na akaisemea maneno kuwa, nanukuu, "kwa sadaka hii ninabatilisha kila agano na apizo niliyofanya na yaliyofanywa juu yangu kwa kujua ama kutokujua na mamlaka za giza kwa Damu ya YESU kwa JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH ALIYE HAI, AMEN"

Baada ya kutoka hapo ndipo alipofunguka akili na kurudiwa na ufahamu wake na kujiona kuwa amepoteza na anaendelea kupoteza mengi sana kwa kukubali kutumikia madhabahu za giza kwa tamaa ya utajiri wa pesa ulio na madhara makubwa sana kwa nafsi ya binadamu. Akatubu na kumrudia Mungu Mwenyezi na ndipo alipoanza kufanikiwa kwani Mwenyezi hashindwi na neno lolote!

MY TAKE:
BWANA YESU KRISTO ndiye Mfalme wa Milele, na Uzima hutoka Kwake tu! Yeye ndiye aokoaye kutoka kwenye kinywa cha adui shetani, ni kwa kumuamini BWANA YESU KRISTO tu na kumtolea sadaka ya kweli iliyo kamili itokayo rohoni!

Malaki 3:7-12

7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?

8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
 
Tena hizi roho zinatengeza uhalali na umiliki kwa njia hiyo ya maagano na sadaka kwenye bible hizo roho zinatembea kizazi cha kwanza hadi cha nne asante mshana jnr kwa somo
 
Inakuwa kama hivi
people_walking_off_a_cliff1.dsgm3ysneego0skwkg008o844.6ylu316ao144c8c4woosog48w.th.jpeg
 
Back
Top Bottom