Kigugumizi cha CHADEMA juu ya akina Halima Mdee kinatokana na nini? Sikilizeni Rufaa na mtoe uamuzi wa mwisho

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.

Mamlaka za kibunge zinasubiri uamuzi wa CHADEMA juu ya rufaa ya akina-Halima Mdee ili ziweze kuchukua hatua stahiki. Spika Tulia ameshasema Bunge linaendeshwa kidemokrasia na kisheria. Unasubiriwa uamuzi tu wa CHADEMA.

Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho...
We ni mwanasheria kweli au wale makanjanja? wewe mtu akihukumiwa kifungo gerezani lakini akakata rufaa hataenda gerezani mpaka rufaa yake isikilizwe?

Tulia mwenye kaingia bungeni kwa nguvu ya dola unategemea atasimama upande upi? pale bungeni wabunge walioingia kihalali hawazidi wanne lakini na wewe unajitoa ufahamu .
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho...

Hauna akili kabisa! Kama watu walipora uchaguzi in day light, mpaka Leo siamini!

Mbowe yupo magerez Na hata Chakula hapati; how do you deal with these kind of people?
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho...
Nadhani kwasasa CHADEMA ina more serious issues kuliko hiyo rufaa ya covid 19.. Na usidhani CHADEMA ni ma layman kiasi cha kutojua wanafanya nini..!
 
Hv ukihukumiwa jela huku umekata rufaa unatoka kwenda kula bata co???kwa Tz hii kila kitu kinawezekana ikiwa tu mhimili uliojichimbia chin zaid una baraka zake
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho...
 
We ni mwanasheria kweli au wale makanjanja? wewe mtu akihukumiwa kifungo gerezani lakini akakata rufaa hataenda gerezani mpaka rufaa yake isikilizwe? Tulia mwenye kaingia bungeni kwa nguvu ya dola unategemea atasimama upande upi? pale bungeni wabunge walioingia kihalali hawazidi wanne lakini na wewe unajitoa ufahamu .
Mkuu, hoja yangu inahusiana vipi na uanasheria wangu?
 
Mkuu, hoja yangu inahusiana vipi na uanasheria wangu?
Mkuu wewe kama mwanasheria tunategemea uwe mfano bora wa kusimamia katiba, sheria, kanuni na taratibu, unaona katiba inavunjwa kwa makusudi unawasukumizia mzigo CHADEMA, CHADEMA walishasema wale siyo wanachama wao, kama chama hakiwatambui nani mwingine anaweza kuwatambua?

Lipumba alifukuza wanachama wake wabunge mbona waliondolewa na wakati walikuwa wamekata rufaa Ndugai hakusubiri rufaa yao? Sophia Simba alifukuzwa mbona Ndugai hakusubiri rufaa yake lakini anasubiri rufaa ya CHADEMA pekee?
 
Wakili leo umeacha akili zako ofisi ndogo ya Lumumba.

Hivi huwa mnasubiri Rufaa isomwe ndiyo wahusika waanze kutumikia adhabu yao iliyotolewa na chombo cha awali???

Yani mtu hajateuliwa na hajatambulishwa na chama chake kaingia bungeni kwa mlango wa gereji alafu leo wakili unataka maamuzi ya kumtoa hapo bungeni yasubiri rufaa wakati tayari officially maamuzi ya kuwatimua yalishafanyika na taarifa ilishafikishwa bungeni!

Comrade Petro give yourself a minute and think like a laywer, not like kiazi cha lumumba.
 
Back
Top Bottom