Kifo cha Polycarp Pengo hakijanigusa. Alitakiwa afe miaka ya 90 huko. Sababu alizuia Katiba mpya

Kifo cha Polycarp Pengo hakijanigusa. Alitakiwa afe miaka ya 90 huko. Sababu alizuia Katiba mpya

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,662
Reaction score
59,100
Huyu Polycarp Pengo alikuwa mnafiki sana.. Na amekuwa kikwazo katika mapambano ya Katiba mpya. Tangu awageuke Maaskofu wenzi nilimdharau sana..

Ukiongea naye, alikuwa anaonekana hata kwwa kauli kutokuguswa na Watu kupotea wala kutekwa.

Tangu amewageuka Maaskofu wenzake wakina Gwajima, Pengo sikumuheshimu tena. Aligeuka Kibaraka wa Watawala walio madarakani.

Pengo alisema Wananchi Wanataka Matibabu, afya na Elimu ndio kipaumbele sio Katiba Mpya. Na akashawishi Watu wapigie kura Serikali Mbili badala ya 3. Aliishi kwa kibaraka wa Watawala...

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba Mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba Mpya."

Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba," alisisitiza Kadinali Pengo.

Hayo yote alisema pengo wakati tupo kwenye Mijadala ya kilele cha kupata katiba Mpya.

Je, sasa hao wananchi wanapata madawa?

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge, Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi aliposema umuhimu wa Katiba mpya kuwa ndiyo kipaumbele cha kwanza cha Watanzania, Pengo kwa kushirikiana na Serikali walimletea Msukosuko kwwa kutumia Polisi na Uhamiaji.

Baba wa watu hadi kanisani akawa anachezewa zengwe kisa Kitiba.

Kwa ufupi, ni kifo kama vifo vingine tu

Askofu Niwemugizi alisema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.

"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."

Baada ya hiyo Kauli, Huyo Pengo alokufa akaita vyombo vya habari vikiongozwa na TBC kwamba aliyoyasema Niwemugizi sio Msimamo ya Kasani.. Hiyo taarifa ya Pengo ilikuwa inarudiwarudiwa kila siku na TBC kwa Mwezi mzima. Na wale waliotangaza na kuchapisha taarifa ya Niwemugizi wakapata misukosuko.

Ndugu Watanzania, mimi nipo pamoja na wale wanaotaka Katiba Mpya, suala la Katiba si la mtu mmoja. Mapambano ya ufisadi na rushwa yanapaswa kutambulika na Katiba na wananchi wanataka Katiba kwa nini wasipewe Katiba yao? Tunataka Rais awe kushitakiwa, Vyeo vya ukuu wa Mikoa na Wilaya watu waombe kazi wafanyiwe interview. Tunaitaka Tanganyika yetu,Tunataka Uraia pacha nk.
 
wabongo bhana,yani kila mtu kitengo!
Sasa kama kila mtu kitengo wananchi wa kawaida ni wakina nani??.!
 
Back
Top Bottom