Kifo cha Mh Mzee Sitta na maswali kadhaa

Kifo cha Mh Mzee Sitta na maswali kadhaa

Kama kuna kitu nachukia chini ya jua ni uongo haswa wa kizushi. Nasema, Akheri nikufume unaniloga kuliko kukufuma unanizushia, nitakachokufanya utaomba nchi ipasuke.
Katika karne hii, na kizazi hiki ambacho hata bibi kizee anajua kupiga picha, Wewe Lemuntuz unayeleta umbeya wako hapa ati uliona, ulishuhudia watu wakisherehekea kifo cha Sita, picha ulochukua ziliungua??? Weka hata moja hata ya photo shop basi kuwaonesha hao mafirauni???? Jamani, sitishii ila, miongoni mwa wale waliomnenea mabaya huyo unayemnenea hawapo nasi. Sijasema weshakufa wote ila weshatangulia wengine na kale kazee kalikokuwa kanangojea kufa bado kapo na tunategemea ashiriki kugombea tena 2020. Upooooo.
Yawezekana ulitegemea akutendee jambo flan alipokuwa matawi ya juu ka dingi wako akakusahau, Usilipizeeee kwa kumnenea mabaya. Poa tu ndg, endelea kujikomba kwa wenye meno, lakini usiuue utu wa mtu.
 
Kati ya yote kuna kimoja kiko wazi sana japo hujakitaja FIRST LADY wetu hapewi heshima anayostahili popote ,
Naona mkuu umeamua sana kuhusu first lady, kuna uzi wako pia umetoa maoni yako nimebaki natafakari nini hasa tatizo. Kimsingi niseme neno, first lady wala sio msaidizi wa rais, ni mkewe tu na hata protokali zinaweza kusema hilo. Kazi kubwa ya first lady ni kumtunza mkulu na sio kuchukuliwa kama rais msaidizi. Itoshe tu kusema first lady anaheshimiwa sana ila sijui wewe kama wewe ulitakaje.

Pangu Pakavu.
 
Ndugu zangu hakuna propaganda mbaya kwenye maisha kama uzushi na uongo! Yote yanayoongelewa hapa ni emotional but emotional hizo zaweza pelekea ufanye vizuri au vibaya! Mbaya zaidi kuna watu watatumia msiba wa mtu kujitafutia umaarufu na kujijenga kisiasa!

Kama kuna anayefurahia kifo cha adui yake hana tofauti na mnyama anayekuta mwenzie kafa na kuanza kumla nyama!

Nasema tuache propaganda chafu kama kweli kuna sherehe inafanywa na watu sababu ya kifo cha Mzee wetu sitta naomba picha au video zenye mabango yanayobeba content ya sherehe hiyo tofauti na hapo ni majungu na uhafidhina! Sisi ni wasomi jamani japo sijui viwango vya kielimu na uelimikaji uliobebwa na kila mwana jamvi!

Siko upande wowote wa chama kama raia mwema napenda kusimamia ukweli na kukosoa kitu kiitwacho propaganda hasa ninapogundua kitu! Over!!!?
Kwanini alaumiwe Eddo, anapoenda mazikoni mnamsubiri njiani kumzuia na kumrejesha, leo kaamua kukaa kwake mna msema nynyi vipi, huyu ni binaadamu mnafikiri yeye anafurahia ayo munayomfanyia, acheni izo kesha fahamu sasa kaamua kutulia ,kama lengo lengo kumuadhirisha hamumpati tena kesha fahamu
 
Sio Ngeleja hakuwahi kuwa waziri mkuu

Pia... Salim Ahmed Salim hakuwepo
Cleopa David Msuya hakuwepo
Augustine Lyatonga Mrema hakuwepo (naibu waziri mkuu mstaafu)

Ngoja niishie hapa kwanza
Ngeleja aliwakilisha bunge kwenye mazishi ya mbunge mwenzao Zanzibar akiwa na akina zungu.
Salim A. Salimu alikuwa kwenye mazishi hayo ya Zanzibar
 
Jibu la swali lako lenye vipengele vitatu ni hili Mkuu,
1024px-Padlock.svg.png
 
le mutuz unazeeka vibaya kwani kumzika mtu ni lazima? au bila EL marehemu asingezikwa au angeongeza nini uko msibani
 
Mtoto wa mkulima kastaafu siasa na kwa sasa anaishi Dodoma akijishughulisha na kilimo na ufugaji. Wakati wa kuaga mwili Bungeni alikuwepo. Acha kuandika hisia badala ya uhalisia.
Tena hata akiona hiyo taarifa ya msiba anabadili Chanel anaweka National Geographic .
 
Mabifu ya wanamtandao na pollonium 310, watamalizana sana ........mwanzo wote walimuwinda Lowassa ....mwaka 2008 Lowassa alipopita pale VIP kuelekea ujerumani ....kwa matibabu...muda mfupi baada ya kutolewa uwaziri mkuu...kila mtu aliyemuoana alilia machozi ...alikuwa haoni na hajiwezi ..
Haikuwa ajabu wenzake kuendelea kuimba litania za hafiki kesho ,hafiki kesho ,ilipofika 2015 wakawa wanasema hafiki mwenzi wa nne ...hata wakapeleka mbele uteuzi ndani ya chama wakiamini yeye atakuwa ashakufa ....mara hafiki mwezi wa sita ....
Mara hamalizi kampeni , mara atafia Ikulu ........hakika Lowassa ana moyo wa kusamehe ..

Sitta mwanamkakati asiyechoka baadaye ikaonekana kuwa aliendelea kulipiza kisasi kwa Jk ,analaumiwa sana kwa kuwapa wapinzani nguvu bungeni na pia kwa kuweza kuwa chachu ya Katiba ya wananchi -ukawa .na msamaha wake ulikuwa mgumu..ikidaiwa aliendesha lile bunge kwa malengo yake ya urais ....
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Ila ile ongea yake duuh, kwani hakuwahi kabisa kuishi Urambo? Au swaga tu

Ni mapozi tu yale. Si unajua hawa watoto wa siku hiz wakipewa maisha na wazazi wao wanaona tuliobaki huku Africa ni malimbukeni.
 
Tangu yule mwanamuziki Wa twanga pepeta akupige ngumi kwa kumpost mke wake IG, akili yako haijakaa ikatulia wewe lumutuz...
 
Ni mapozi tu yale. Si unajua hawa watoto wa siku hiz wakipewa maisha na wazazi wao wanaona tuliobaki huku Africa ni malimbukeni.
watoto wa wakubwa wengi wao mabwege....na wana mawazo kuwa hii nchi ni ya kifalme ....wakati Mwalimu hakumpa hata mwanaye mmoja kazi
Mzee mwinyi naye maskini katuhumiwa sana lakini kwa uadilifu anamfuatia Mwalimu , mkubali mkatae .....yeye hakumpa mwanaye yeyote kazi ...huyu Hussein mnayemuona amatoka Turkey enzi hizo Muhimbili wana bifu na Mwinyi wakakataa kumuajiri ...wala hakuwa na neno akamuomba mzee Kairuki ...kijana akawa anapiga day worker pale ..na akafanya na masters .......Hussein miaka yote ya utawala wa baba yake amefanya kazi private ...na akitoka kazini anaangalia Tv tu home hakuwa speed ..sana ...Aliyekuja kumkumbuka Hussein na watoto wa Mwalimu ni Mkapa ..ambaye naye wanaye hakuwapa kazi ..
lakini sasa tunao viongozi watoto wao ni "wakimbizi" ulaya na bado wanataka kufanya chama ccm cha kuridhishana .....
 
Anaishi marekani, kutokujua kiswahili ni mbwembwe tu maana baba yake na mama yake ni Samuel na Magreth kwahiyo anatakiwa kukijua vizuri tu, mbona Agnes anaongea vyema?
John Sitta hakuwepo , kwa nini hakuja ? maana nae anaishi Marekani
 
Back
Top Bottom