Registered_jf
JF-Expert Member
- Nov 27, 2024
- 1,271
- 2,204
Simulizi la kifo chake kutoka kwenye Biblia na kutoka kwa mwanahistoria Josephus.
1) Matendo 12 inatusimulia kuwa Herode Agripa aliwatesa wakristo, alivyoona wayahudi wamefurahia hilo akaanza kumuwinda kumuua Petro. Petro akakamatwa akafungwa gerezani akisubiri kuuawa siku ya Pasaka.
Usiku kabla ya Pasaka, Petro alitoroshwa gerezani na malaika. Humo alikuwa na wafungwa wengine, yeye kafungwa minyororo na ulinzi mkali huko nje: vikundi vinne vya askari wanne wanne.
Asubuhi askari wanahaha wafungwa wameenda wapi, minyororo imebaki gerezani. Herode akaagiza askari wauawe.
Siku za baadaye Herode akatoka kuhutubia watu, watu wanamsifia wanasema ni sauti ya Mungu! Na Herode akazikubali sifa hizo. Ghafla akaugua akafa!
"Katika siku iliyochaguliwa Herode Agripa akavaa mavazi yake ya kifalme, akaketi kwenye kiti chake cha utawala, akawahutubia watu.
Watu waliokuwa wamekusanyika wakapaza sauti, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu!”
Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Bwana akampiga, naye akaliwa na chango, akafa."
Matendo.12.21-23.NENO2025
2) Flavius Josephus naye kwenye maandiko yake Antiquities of the Jews anatusimulia:
"Katika moja ya sikukuu hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika, wakiwemo watu mashuhuri na wenye vyeo katika jimbo lake lote.
Siku ya pili ya maonyesho hayo, alivaa vazi lililotengenezwa kwa fedha tupu, lenye ufundi wa ajabu sana, kisha akaingia ukumbini mwa michezo mapema asubuhi.
Wakati huo, mwanga wa jua la asubuhi ulipolipiga vazi lake la fedha, lilimetameta kwa namna ya kushangaza. Mng'ao wake ulikuwa mkali sana kiasi kwamba uliwatia hofu wale waliokuwa wakimtazama kwa makini.
Mara moja, watu waliokuwa wakimsifu kwa kujipendekeza wakaanza kupaza sauti kutoka kila upande, ingawa hawakuwa wakimtakia mema, wakisema: "Huyu ni mungu!"
Wakaongeza kusema: "Uwe na rehema kwetu. Ingawa mpaka sasa tumekuwa tukikuheshimu kama mwanadamu tu, kuanzia sasa tutakukiri kuwa wewe ni mkuu kuliko mwanadamu wa kawaida."
Mfalme hakuwakaripia wala kukataa sifa hizo za kumkufuru Mungu.
Lakini muda mfupi baadaye, alipoinua macho yake juu, alimwona bundi akiwa ametua juu ya kamba fulani iliyokuwa juu ya kichwa chake.
Mara moja alitambua kwamba ndege huyo alikuwa mjumbe wa habari mbaya, kama vile hapo awali alivyokuwa mjumbe wa habari njema kwake. Jambo hilo likamwingiza katika huzuni kubwa sana.
Pia, maumivu makali yalianza tumboni mwake na yakazidi kuwa makali sana...
....Aliposema hayo, maumivu yake yalikuwa yamezidi sana. Kwa hiyo akabebwa hadi ikulu. Habari zikaenea kila mahali kwamba bila shaka angekufa muda mfupi baadaye.
Lakini mara moja umati wa watu ukaketi wakiwa wamevaa magunia, pamoja na wake zao na watoto wao, kulingana na desturi ya nchi yao, wakimsihi Mungu amponye mfalme.
Kila mahali palijaa maombolezo na vilio.
Mfalme alikuwa amelala katika chumba cha juu. Alipowaona watu waliokuwa chini wamelala kifudifudi ardhini, naye mwenyewe hakuweza kujizuia kulia.
Baada ya kuteswa na maumivu ya tumbo kwa siku tano, mwishowe akafariki dunia.
Alikuwa na umri wa miaka hamsini na minne, na alikuwa katika mwaka wa saba wa utawala wake."
Antiquities of the Jews 19.8.2
Kitabu cha Matendo ya mitume kinakadiriwa kuandikwa kati ya mwaka AD 58-62.
Kitabu cha Antiquities of the Jews kiliandikwa mwaka AD93.

When was Acts written? | GotQuestions.org
When was Acts written? Was the book of Acts written in around 60 AD?
www.gotquestions.org