KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA SITINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TATU: “hapana Jesse, ukionyesha kiburi watazidi kunichukia, cha msingi wewe bakia kwanza mpaka wageni watoke” nilimshauri Jessenia, ambae sasa alinielewa nia yangu, “hapo sawa, kuwa kile alicho kielewa, aikuwa nia yangu harisi, nia yangu ilikuwa ni mpaka nitakapo kamilisha kazi yangu, niangalie kama bado nitakuwa katika mapenzi na Jessenia, na kama yatakuwa katika kiwango hiki basi nifanye taratibu za kumbeba jumla jumla, tena kwa kumtumia huyo huyo Mangeu, “usijari Jesse, kila kitu kitaenda sawa” nilimjibu kabla ya kukata simu tukikubaliana tuwasiliane kesho asubuhi. ….…. ENDELEA..
Naam nilizima taa na kuiingia kitandani, kisha nikaaanza kuwaza mambo kadhaa, matatu yakiwa makubwa zaidi ya mengine, la kwanza lilikuwa ni kuhusu ugeni ambao ulikuwa unakuja nyumbani kwa kina Jessenia, je una husiana na Jessenia ndio maana wame muambia asitoke nyumbani kuwasubiri wageni, na kama ana husiana na Jessenia, na kama ni ndio je unahusiana kivipi, na vipi kuhusu Mangeu anaufahamu ugeni huo, maana ile nyumba ipo chini yake na kila kinachofanyika anakifahamu, au anatakiwa akifahamu, kama anafahamu mbona hakunieleza, je unaweza ukawa ni ugeni wa kawaida ndio maana hajaniambia, au hakukuwa na ugeni wowote ila walikuwa wanamzuga Jessenia ili abakie nyumbani asikutane na mimi.
Hakika ilinipa wakati mgumu kupata jibu, lakini niliamini kuwa jibu nitalipata kesho kama sio kwa mzee Mangeu, basi kwa Jessenia mwenyewe, jambo la pili nililo hitaji kulipatia jibu, ni sababu gani ambayo ina mfanya Ussi na baba yake wa fanye mauwaji kuzuia Jessenia kuolewa, ni kweli Ussi na baba yake ndio waliokuwa wanahusika, naweza kulithibitisha hilo, kwa sababu kadhaa, moja na ya kwanza ni kuhusika kwa vijana wa Ussi katika mauwaji na dalili za wazi ambazo Ussi anazionyesha, hasa zile za kunikunjia uso kwa hasira akionyesha kunichukia, la mwiso ni kwamba mtu ambae nilimueleza insp Aroub akamueleze wazi wazi kuhusu ugunduzi wa kuwa muuwaji sio jini ila ni mtu na wanaotakiwa kuhojiwa ni wafanyakazi wa Ussi ni mzee Juma, ambae aliposikia hayo akamtua mtu kwenda kumuua Mabusi, ambae alikuwepo usiku wa jana ambao walinishambulia, baada ya kuliwaza hilo na nilianza kuwaza kuhusu kama naweza kumtumia babu Mangeu kupata ushahidi ambao utaniwezesha kulimaliza swala hili, niliwaza kwa masaa mawili pasipo kupata jibu, maana kila nilicho kiwaza kilipingana na ushirika huu mpya, saa sita za usiku ndipo nilipokumbuka kuhusu HDD, yaani Hard Disc Drive iliyoibiwa kwenye PC ya nyumbani kwa marehemu Vuai, iliyokuwa ina tunza kumbu kumbu za matukio yanayo naswa kwenye camera za ulinzi, (security camera) usiku wa tukio la mauwaji, hata kama iliibiwa na mtu mwingine yoyote, lazima itakuwa kati ya sehemu mbili hizi, yani kwa wale wavuvi au nyumbani kwa kina Jessenia, yaani chumbani kwa Ussi, hapo kunahitajika kitu cha haraka kufanyika, ni upekuzi wa haraka kwenye vifaa vya wakina mrehemu Mabusi na kama ikikosekana basi atumiwe mzee Mangeu kupata ushahidi huo, lakini kila nilipowaza atafanyaje ili kupata hyo HDD, niliona wazi kuwa asinge weza kuipata kirahisi, mwisho nikapata wazo la kumtumia Jessenia, sasa swali likabakia, je nita mtumiaje Jessenia kuipata hiyo HDD, kwamba itakuwa vyema kumtumia mwenyewe JJ, yaani babu Mangeu kuomba ushauri au nikomae mwenyewe.
Hilo ndilo nililoliona linafaa, maana ilikuwa ni lazima habari nyingi nianze kuzipata mwenyewe, ikiwa sasa ninavyanzo vya habari vya ziada vitatu, yaani Jessenia, insp Aroub na Mangeu, niliamua kuwa nitakabiliana na Jessen mimi mwenyewe ili kumkabili juu ya HDD, wakati huo nikimpigia simu babu Mangeu ili achunguze juu ya wageni ambao wanatarajiwa nyumbani kwa kina Jessenia, na wanahusiana na nini, japo sikuwa nimemuweka wazi kuhusika kwa rafiki yake Juma Mohamed, katika mauwaji ya wanaume wanao kuwa karibu kushiriki mapenzi na Jessenia, lakini ilikuwa lazima nimtahadharishe kuhusu kukurupukia mambo, asije kuuwawa na yeye, mara watuhumiwa wetu watakapo gundua kuwa amesha gundua jambo kuhusu wao, na ilitakiwa nimtahadhalishe pasipo yeye kujuwa shuku langu moja kwa moja.
Sikutaka kusubiri, moja kwa moja nikapiga simu kwa Mangeu, ambayo iliita kwa muda mrefu sana kabla hajaipokea, “vipi tena kijana kumesha kucha?” aliuliza Mangeu kwa mshangao na mshtuko, akionekana ametoka usingizini, “tulia basi we mzee, mbona kama unaonekana hufai kufanya kazi ya upelelezi, yaani umefika tu na kulala, wakati kuna mambo ya kufuatilia” nilisema huku nacheka kidogo, ilikuwa njia ya kumtuliza wenge mzee Mangeu, “umeiharibia sana we kijana, ujuwe mwenzio nilikuwa naota ndoto nzuri sana” alisema Mangeu akionekana kweli nilimkatiza ndoto yake nzuri ambayo alitamani aendelee kuiota, nilichekea tumboni, “achana na ndoto we mzee, sasa unatakiwa uishi maisha halisi, hebu sikia nikuambie kitu” nilimuambia mzee Mangeu, ambae alitulia kunisikiliza, “sikia mzee Kesho kuna wageni nyumbani kwa kina Ussi, na Jessenia ameambiwa lazima awepo hapo nyumbani, sijajuwa ni kwaajili ya nini, je unaufahamu huo ugeni?” nilimuuliza Mangeu, ambae alivuta pumzi ya kichovu na kuitoa kwa uvivu, “sijui lolote, siku zote Juma amekuwa akifanya mambo bila kuniambia, hasa yanayo muhusu mwenyewe, we unadhani inaweza wageni hao wanahusiana na kitu ambacho tuka kichunguza?” aliuliza mzee Mangeu, kwa sauti ambayo ilionyesha kuto kuamini kama ugeni huo unahusiana na kile ambacho mimi na yeye tuliamua kukifanya, “sikia mzee, katika swala kama hili hutakiwi kupuuzia jambo lolote, hata kama ni ndogo kiasi gani, vinginevyo kale kamsemo ka mdharau mwiba katathibitika kwetu” nilimueleza mzee Mangeu, ambae baada ya kufikiria kidogo akakubaliana na mimi, “sawa hakuna shida, nitafuatalia kuhusu hao wageni, je kuna jingine?” aliuliza mzee Mangeu ungesema anaona nina mchelewesha kulala, pengine alitaka kuiwahi ile ndoto yake, “jingine ni kwamba wakati unafuatilia hicho kikao asijuwe mtu yoyote kama unafuatilia, pili lolote utakalo lipata kwenye kikao hicho usije ukamueleza mtu yoyote zaidi ya mimi mwenyewe, yaani usifanye chochote mpaka tukutane na kujadili la kufanya juu ya chochote utakacho kisikia” nilimsisitiza Mangeu ambae alionekana kunielewa, japo hakuhitaji maelezo mengine maana alikuwa na hamu ya kulala na kuota ndoto yake aliyoianza, ilinishangaza sana, sikufikiria mzee kama huyu, anaweza kuitamani ndoto kiasi cha kuwaza kwamba inaweza ikaendelea toka pale alipoishia, hakika inahuzunisha sana, mzee kama huyu kuishi maisha ya ndoto ilihali ana mali nyingi sana, ambazo sikujuwa amezihifadhi wapi, angeweza kuishi maisha anayo yataka, lakini alikuwa anahofia ubaya wa sura yake, iliyoharibia na makovu makubwa makubwa, ni wazi hakujuwa siri ya mafanikio ni kuwa na fedha, pengine hata ange mpata mschana mmoja ambae ange mwambia, Baby napenda ngeu zako zimekaa vizuri, (natania tu)******
Naam siku ya pili ukweli ukiachilia sauti za makamanda waamrishaji wa gwaride, zilizokuwa zinasikika, toka upande wa uwanja wa kwata wa Al khamis camp, pia niliamshwa na mwalimu Aisha ambae aliamua kujipa kazi ya kuniamsha kila siku, na kama kawaida yake pua zake ziliponusa harufu ya manukato ya Jessenia, hakuweza kukaa kimya, “mh! jana ulijifanya anaomba ruksa ya kwenda mjini, kumbe una mambo yako, we haya tu, utamjaza mimba mtoto wa watu” alisema Aisha kama vile ananisimanga, lakini katika hali ya utani, maana alimaliza kwa kicheko, “kwani kuzaa ni dhambi” na mimi nilimjibu kikauzu, lakini ya kiutani utani, na wakati huo huo iliingia simu ya Jessenia, niliipokea na kuongea nae kwa namna ambayo sikutaka Aisha ajuwe kama ninaongea nae.
Jessenia alikuwa ananijulisha kuwa, nyumbani kwao kulikuwa na maandalizi makubwa sana, kuanzia mapema ile, ilionyesha kulikuwa na ugeni mkubwa sana, “yaani sijui tutaonana saa ngapi, mwenzio nina hamu ya kukuona” alisema Jessenia, ambae nilishindwa kumjibu mbele ya Aisha, na mimi kuishia kucheka tu, “lakini wakiondoka tu, nitakupigia uje unifuate” alisisitiza Jessenia, na hapo na mimi nikamsisitiza jambo, “usisahamu kunijulisha kila kinachoendelea, hata kwa sms” nadhani ndicho kitu pekee ambacho Aisha alikisikia toka kwangu, Jessenia aliahidi kunijulisha kila kinachoendelea.
Pia wakati tuna toka Green House, niliona wanajeshi wana fanya usafi wa mazingira na kufanya parade mbali mbali za gwaride la miguu mchanga nyiko, ilionyesha ni maandalizi fulani ya maonyesho au tukio la kiserikali, lililokuwa lifanyike siku chache zijazo, Mangeu nae akanipigia simu na kuniambia jambo kuhusu ugeni, “mashaka yako yanaweza kuwa ya kweli, maana naona dalili za maandalizi fulani, lakini ni wazi kuwa yanafanywa kwa siri, wacha kwanza nifuatilie” alisema Mangeu, na mimi niliitikia kwa kauli za makato mkato, ili Aisha asielewe kitu, “hivi Ussi amekubaliana na swala hilo? maana ninavyo mjuwa yule kaka ana wivu” aliuliza Aisha, wakati tunatoka pale Green House, “ukweli sijawahi kuongea nae tena, ila naona kama hajapenda, maana ananitazama kwa macho fulani hivi” nilimjibu Aisha na wote tukacheka kwa pamoja.
Siku ile sikuwa na mpango wa kuomba ruksa yoyote, labda kama ninge pigiwa simu ya kuhitajika mjini na Jessenia, insp Aroub au Mangeu, nilikaa shuleni, nikiongea na mwalimu Aisha, ambae kuna wakati alienda darasani, kwenye kipindi chake, na kunifanya mimi nizuge nasoma kitabu, huku nawaza ili na lile juu ya kazi yangu ambayo niliona ndio kwanza imezidi kukolea, na sasa nilitakiwa niipeleke mwisho.
Nakumbuka mida ya saa nne kasoro, nilipigiwa simu na insp Aroub, ambae nililazimika kutoka nje ili nikaipokee, “asalam aleykum mzee” nilimsalimia mzee Aroub, maana hii ndiyo salam pendwa na ya kipekee kwa huku kisiwani, “waalaykum salaam bwana Eric, upo wapi saa hizi, tunaweza kuonana?” aliuliza insp Aroub akionyesha kuwa alikuwa na jambo muhimu sana la kuniambia, “nipo shuleni mzee, vipi kuna jambo lolote?” nilimuuliza insp Aroub, ambae nilijuwa tu lazima ata niambia kila hatua anayo ipitia.. ….…. ENDELEA..